Watu wanapitia mengi, magumu na hawasemi. Wengine unakutana nao, unafikiri wako sawa kwa vile hawakuambii kinachoendelea. Wengine, kwa vile walivyo, hukabiliana na maumivu yao wenyewe kwa kupunguza mawasiliano na wewe wapate faragha ya kujiuguza bila kukusumbua na kukubebesha mzigo. Hawa wanapopitia magumu hujificha, saa nyingine, wakiogopa kuhukumiwa, kulaumiwa na kueleweka vibaya.
Kabla hujamlaumu mtu kwa kutokukutafuta, kukupita bila kukusalimia, kushindwa kukufanyia vitu vidogo vidogo kama kupokea simu zako, inapendeza kuamini mtu anaweza kuwa na sababu za msingi na hazikuhusu wewe. Unaweza kujiumiza sana ukitumia uzoefu wako binafsi na mambo uliyowahi kukutana nao kuelewa maamuzi ya mtu bila kumsikiliza.
Kuna yule ‘wewe’ wa hadharani unayemtengeneza aonekane na kukubalika na watu—‘wewe’ mkamilifu, usiye dhaifu, unayejua unachotaka, unejipata na kujitosheleza; ‘wewe’ mkarimu, mwenye upendo, usiye na matatizo na watu; ‘wewe’ mwenye utu na huruma na watu, ‘wewe’ mcha Mungu, anayemtanguliza Mungu kwa kila jambo; ‘wewe’ msomi, mjuzi wa mambo, mwenye busara na maarifa; ‘wewe’ anayejituma, mwenye bidii ya kazi.
Halafu kuna yule ‘wewe’ wa faragha usiyependa afahamike sana na watu—‘wewe’ dhaifu, usiyejiamini, mwoga, usiyejua kwa hakika unafikaje unakokwenda; ‘wewe’ usiyejipenda, usiyejisamehe, unayejichukia na unayetafuta huruma; ‘wewe’ mbinafsi, anayeweza kufanya chochote kupata anachotaka; ‘wewe’ anayeteseka na tamaa, asiyeweza kupenda, anayehangaika kupokea upendo na asiyeacha kugombana na watu wema.
Tofauti kubwa kati ya ‘wewe’ wa faraghani na huyu ‘wewe’ unayetuletea hadharani ndiyo inayochangia matatizo yako mengi kitabia. Huna amani na uhuru kwa kuishi maisha yako kwa vile unajua fika kuwa ‘wewe’ unayetuletea hadharani hafanani na wewe unayemjua sirini. Una hasira na kisasi na watu wema wasio na shida na wewe, unagombana na watu ambao kimsingi walipaswa kuwa rafiki zako, kwa vile watu hawa saa nyingine bila kujua wanamchokoza ‘wewe’ asiyependa afahamike na watu.
Ukishaona unalazimika kujitambulisha sana huenda unaziba ombwe—unajua fika unapwaya kwenye nafasi yako. Hutoshi. Hujakidhi vigezo.
“Mimi ndio mume wa familia hii. Unasikia?
Mimi ndiye kichwa cha familia. Kwenye hii familia baba ni mimi.”
“Mimi nimesoma. Mimi ni professional hasa. Najua ninachoongea. Sibahatishi.”
“Mimi ndio kiongozi wenu. Nina nguvu za kusema ruka na ukaruka bila swali. Mmesikia? Hapa mnaongea na Mwalimu wa Zamu. Sijajileta. Nimeletwa.”
“Sisi sio wajinga. Sisi mnaotuona hapa tuna akili zetu timamu. Msituone kama hatuna elimu. Tumesoma dini tukamaliza na elimu dunia tunayo.”
Utambulisho huwa haulazimishiwi. Unafanya vitu vinavyolingana na nafasi yako wanajua huyu ni baba, huyu ni mume, huyu kweli kasoma, huyu ndio mwalimu, kweli wiki hii zamu imepata mwenyewe. Ukitosha hulazimiki kuwakumbusha watu wewe ni nani. Kazi zako zinakutambulisha.
Unatoa ulichonacho. Unawatendea wengine kile unachojitendea mwenyewe. Ukishagombana na nafsi yako, mathalani, utagombana na kila anayekukumbusha ugomvi wako na ‘wewe’.
@tweetbylegendy Ratiba ya kuzima umeme,asee yule mama ni zaidi ya Nduli.
Umeme unazimwa saa 3asbh na kuwashwa saa 12 jioni.
Saa 5:00 usiku amazima na kuwasha tena saa 12:00 asbh.
Miezi 6 ilikiwa mingi sana 🙌