Tuko kwenye Dunia ambayo Mwananchi anaweza kuwa na Taarifa nyingi zaidi na sahihi kuliko Kiongozi.
Mtoto ana Taarifa nyingi zaidi na sahihi kuliko Mzazi, Msikilizaji ana Taarifa nyingi zaidi na sahihi kuliko Mtangazaji.
Ni muda wa kusikiliza zaidi kuliko kuongea.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 Tawi la Maharo, Kata ya Makiidi wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro kimemtaka mwanachama wa chama hicho Joseph Selasin kujieleza ndani ya siku 14 kuwa kwa nini asichukuliwe hatua za kinidhamu kutokana na kukiuka misingi ya katiba ya chama hicho.
Barua iliyoandikwa kwenda kwa Selasin leo Julai 15, 2026 imeeleza kosa lake ni kutoa matamko ya shutma kupitia vyombo vya habari dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Bara John Wegesa Heche.
“Imebainika kuwa wewe ndugu Joseph Roman Selasin umeonekana kupitia vyombo vya habari ukitoa matamko na shutuma dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa (Bara) bila kufuata taratibu rasmi za Chama za kuwasilisha malalamiko au hoja zako kupitia vyombo vinavyotambulika na katiba na kanuni za Chama.” Imesema barua hiyo.
Anadaiwa kukiuka Ibara ya 10.1(iv) na 10.1(v) ya katiba ya CHADEMA ya mwaka 2006 toleo la 2019. Huku akipewa nafasi ya kujieleza tangu tarehe atakayopokea barua hiyo huku akizuiwa kushiriki, kuongoza wala kutekeleza shughuli zozote za chama hadi atakapokamilisha utaratibu wa
Ikumbukwe Jana Julai 14, 2026 Selasin alionekana akizungumza na kuviomba vyombo vya CHADEMA kuchukua hatua na kuchunguza tuhuma dhidi ya Heche.
Dear Tanzanians,
@TunduALissu, @HecheJohn na @ChademaTZ2 wanamkosesha Rais @SuluhuSamia usingizi kwa sababu kwa mara ya kwanza, @ccm_tanzania inaweza kuona uongozi halisi wa chama cha kitaifa ukiundwa nje ya udhibiti wake. Huu sio aina ya upinzani ambao CCM inafurahia. 1/2
Wamezoea vyama vilivyogawanyika, sauti na harakati zilizotawanyika ambazo zinaweza kusimamiwa kwa propaganda. Lakini kwa sasa Chadema imeanza kuonekana tofauti, inajenga na kuimarisha muundo wake. Inavutia wanasiasa makini. Inazungumzia maumivu ya Watanzania. Cc. @BrendaRupia
“SERIKALI HII YA AWAMU YA SITA” 🤣🤣🤣
Well, ndugu zangu wanachekesha sana. Kwanza wamefanya show ya Miaka 30 ya Bongoflava (Hili nitaliongelea vizuri after this post), wakidhania wanaokuja kwenye show ni GEN Z! Then wametumia tactic za kitoto, kufikiri wanaweza kufanya sinema zao za kuchomeka siasa katikati… alafu Washangiliwe; unaweza kukuta walimpanga mama yao standby ili apige simu baada ya kuona kuna nyomi!!
Hawakujua wengi walikuwa ni Millenials & Gen X… ambao ni watu wazima sasa na wanajielewa. Na ni watu ambao Serikali Hii Ya Awamu ya Sita imewaua Wenzao na Wadogo Zao, na Watoto Wao!! Ni Watu ambao Wanajua kabisa hawakwenda kupiga kura ila Serikali Hii Ya Awamu ya Sita ikadai imepigiwa kura asilimia 90% plus by 30 million people. Ni watu ambao waliona aliyoyafanya Bashite wakati wa Magufuli, na wameshangaa bado ni Waziri sasa! Ni watu ambao wanaona jinsi rafiki zao kina Humphrey Polepole, Mdude Nyagali, Deusdetius Soka, wanatekwa na kupotezwa bila Serikali Hii Ya Awamu ya Sita kufanya lolote na kuwafanya wahisi pengine ni kazi ya mikono yao! Waliokuja kwenye Concert, ni watu ambao wameshuhudia Tundu Lissu akimiminiwa risasi 20 na, nusura kufa, na amerudi kufanya siasa na mkambambikia kesi na kumuweka ndani takriban mwaka sasa!
Waliokuja kwenye show ni Madaktari na Wauguzi walioona Maiti za Oktoba 29, kisha kuja kusikia Serikali Hii Ya Awamu ya Sita inakana!
Waliokuja kwenye show ni Wahasibu, Auditors & Bankers, ambao wanajua ukweli wa hali ya kiuchumi. Na wanajua viongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita wana kiasi gani bank, huku mtaani wananchi wakifa njaa.
Walikuja kupata Burudani & to experience nostalgia!! Hawakuja kupewa “Danganya Toto” wala kuwa “Solitical Stooges”. Waliokuja sio watu wenye njaa, wala sio watoto!! So mbinu za kitoto za Babu Tale na Makonda, haziwezi kufanya kazi!! Na hao Wasanii wenye njaa hawawezi kuwasaidia…
Sababu nia yenu ilikuwa Siasa na sio kuenzi Muziki, mmeishia kuboronga vyote viwili.
WANANCHI UKWELI WANAUJUA, HATA KAMA HUTOWAONA KWENYE MAANDAMANO AU SOCIAL MEDIA WAKIPOST!
Serikali ni HARAMU, hatuitaki na hatuitambui!! Ila sababu nyie ndio mna BUNDUKI, ndio maana watu WAMENYUTI tu.
The Leader
Hoja ya Kupinga Tamko la Serikali kuhusu Makala ya BBC Africa Eye
Na Rev Peter Simon Msigwa
Tamko la Serikali linaibua maswali muhimu kuhusu namna nchi ya kidemokrasia inavyopaswa kushughulikia tuhuma nzito zinazotolewa dhidi yake.
Kwanza, ikiwa Serikali inaamini makala hiyo ina makosa ya ukweli, njia bora si kutishia kuchukua hatua dhidi ya chombo cha habari, bali ni kujibu hoja kwa hoja na ushahidi kwa ushahidi. Ukweli hauhitaji kulindwa kwa vitisho; unahitaji kuthibitishwa kwa vielelezo vinavyoweza kuchunguzwa na umma.
Pili, Serikali inasema BBC haikutoa nafasi ya kutosha kwa upande wake kujibu. Ikiwa hilo ni kweli, basi Serikali ina haki ya kueleza ni lini iliombwa maoni, ni maelezo gani iliyatoa, na ni sehemu zipi ambazo haikuridhika nazo. Hata hivyo, hoja hiyo pekee haiondoi wajibu wa kujibu tuhuma zilizomo kwenye makala yenyewe.
Tatu, kauli kwamba Serikali “itachukua hatua za kulinda heshima ya nchi dhidi ya mashambulizi kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii” inaweza kutafsiriwa kama ishara ya kutishia uhuru wa vyombo vya habari. Heshima ya taifa hailindwi kwa kuzuia uchunguzi wa waandishi wa habari; inalindwa kwa kuhakikisha taasisi za dola zinawajibika, sheria zinaheshimiwa, na madai yoyote yanayohusu ukiukwaji wa haki za binadamu yanachunguzwa kwa uwazi.
Nne, Serikali imeelekeza nguvu nyingi katika kuhoji BBC kuliko kujibu tuhuma zilizowasilishwa. Wananchi wanahitaji majibu kuhusu madai yaliyotolewa, si mjadala kuhusu nani aliyaripoti. Kinachopaswa kujadiliwa ni ukweli wa yaliyomo kwenye makala, si utambulisho wa mtoa taarifa.
Tano, katika demokrasia zilizo imara, uchunguzi wa vyombo vya habari hauchukuliwi kama shambulio dhidi ya taifa bali kama fursa ya kuboresha uwajibikaji. Serikali yenye kujiamini hujibu kwa uwazi, huruhusu uchunguzi huru, na ikiwa madai si ya kweli, ushahidi huonyesha hivyo.
Watanzania wana haki ya kupata taarifa kutoka pande zote. Vivyo hivyo, Serikali ina haki ya kujibu. Lakini haki ya Serikali kujibu haiwezi kuwa sababu ya kuzuia au kutisha vyombo vya habari vinavyoibua maswali kuhusu maslahi ya umma.
Mwisho, heshima ya Tanzania duniani haitajengwa kwa kupinga kila taarifa ya uchunguzi. Itajengwa kwa kuonyesha kwamba nchi ina taasisi zinazoweza kuchunguza madai kwa uhuru, kuwawajibisha wanaokosea bila kujali nyadhifa zao, na kulinda haki za wananchi pamoja na uhuru wa vyombo vya habari. Huo ndio msingi wa taifa lenye nguvu na linaloaminika kimataifa.
ASANTENI WATANZANIA! MPAKA JIONI HII TUMEFIKISHA TSH. MILIONI 40 ✌️
Tunawashukuru kwa dhati Watanzania, wanachama, wapenzi na marafiki wa CHADEMA kwa mwitikio wenu mkubwa katika Marathon ya kufikia TSh. Milioni 334.
Mpaka jioni hii, tumefanikiwa kukusanya TSh. Milioni 40, hatua muhimu inayotupeleka karibu zaidi na lengo letu la kufanikisha Baraza Kuu la Umma.
Mafanikio haya ni ushahidi kwamba nguvu ya umoja na mshikamano wa Watanzania inaweza kutimiza malengo makubwa. Kila mchango unaotolewa ni sehemu ya kujenga CHADEMA imara na kuwezesha Baraza Kuu la Umma kufanyika kwa mafanikio.
Safari bado inaendelea. Tunaendelea kuwaalika Watanzania wote wenye imani na matumaini makubwa kwa CHADEMA kuendelea kuchangia kwa kadri ya uwezo wao na kuwahamasisha wengine kushiriki.
Asanteni kwa kuendelea kuandika historia pamoja nasi. Tuendelee kuchangia hadi tufikie lengo la TSh. Milioni 334. ✌️