Nadhani kibongobongo hakuna shule inayowatreat vizuri ma head prefect wao kama Tosamaganga sekondari wale jamaa head prefect anaheshimika sana na anaishi kitaikuni sana anapatiwa mpaka ulinzi na misosi anapelekewa anapoishi kiufupi anakuwa ana headquarter yake kabisa na inaheshimiwa ajabu😁🙌🏾
Shout out kwa wote wanaopigania mabadiliko na ku~run hii movement online 💻 📱 kwenye social media, mnafanya kazi ya kitume na ya kutukuka mno, do not stop….
Let’s keep pushing💪
BUT‼️
Ni muhimu sana sana sana tuwaheshimu na kuwatia moyo na kuwalinda kwa wivu mkubwa wenzetu wanaofanya kazi hii hii
ON THE GROUND!!
Hawa walioko kwa ground wanakutana na changamoto nyingi na kubwa mno, na wengi wamepitia mateso,shida na vita kali dhidi ya watawala na dola!!
Ukiona hadi leo wako kwa ground and they are still representing the movement…… give them some applause, waombee,waheshimu,watie moyo!!
Usiwavunje mioyo na kuwakatisha tamaa!!
Wapo watu wanaishi Posta, ni dakika 8-10 tu kufika mahakamani alipo TAL, Lakini ukiwaambia wawe kila siku asubuhi wanahudhuria tu hii kesi ya TAL….hiyo kazi itawashinda mapema kabisa na wataona ni kama adhabu na mateso kuamka asubuhi kwenda!
Na hapo ni kwenda tu court, sio hata kama umemwambia kaandamane udai katiba!
Hii kazi sio rahisi sana kuifanya kwa ground, wengi ambao hawajawahi ku~experience zile mbilinge mbilinge za ground kwenye maisha yao ndio wanaweza chukulia poa tu coz haijawahi kuwakuta….they can’t feel it!!
Lakini kwa sisi ambao tuliwahi kukutana nazo….Kuna namna we can relate!!
Kupambana kwa ground nishai jamani, kuna muda ground inahitaji pesa hata ya nauli tu from point A to point B kuingia field na mtu hana.
Na mtoa nauli unakuta ni mbogamboga lialia, unafanyaje apo!?
Unatema kushoto, Unafukia Kulia Twenzao!!
Na hiyo ni nauli, sijaongelea kuumwa,kodi na fees za madogolasi!
Yupo mtu kwenye hizi movement hajawahi hata kudakwa na manjagu akalala Lockup for 12hrs!!
Mtu huyu akidakwa akakaa ndani 72hrs tu, akitoka hutamuona tena kwa ground akiongea the same tone!
Na akiongea atakwenda kuiongelea mbali nje ya minyau 🐈 ya nchi!!
Kwahiyo hawa walioko kwa ground na bado wana stick to the course kuna namna tuwatazame na kuwalinda kwa wivu!!
YES‼️ Kuna wakati wanateleza, ajali za kisiasa zinatokeaga, ajali za kiharakati zinatokeaga…
Tuwe na uwezo wa kupima yapi ni makosa madogo na yapi ni makubwa!
Na reactions zetu, adhabu zetu, hukumu na attack zetu ziendane na aina ya kosa na sacrifice aliyofanya mtu huyo!
Haya mambo ya umeona picha tu ya mwanaharakati wako kapiga na kada wa mbogamboga
Wewe tayari unaichukua unaipost twitter kwenye magroup ya whatssap na insta…..tayari unaanza kuandika makala ndefuu
-🗣️ Huyu kashanunuliwa, kafika bei
-🗣️He is a traitor Unfollow him
-🗣️ Huyu alipokuwa mahabusu polisi walimpiga miti akili zimeshahamia matakoni
-🗣️Huyu alipotekwa walimkaza
-🗣️Ms3ng3 kashakua chawa promax
Picha tu na kada wa mbogamboga lakini utatukaniwa Maza ako post buku, utaitwa mngese,watafukua makaburi yako,watakubully etc!
HII SIO SAWA!
Hatujengi, tunabomoa ngome!
Tujifunze kupima mzani wa kosa kabla ya hukumu jamani!
Tukiishi hivo si tutakuwa kama wao tu sasa, wanaoangua papai kwa kutumia gobole!
Sasa hapo tunatofauti gani na wao ambao wanaweza kumteka na kumpoteza dogo kama Chaula ambaye hakuwa hata na followers 2000 out of watu 70millions….means alichopost hata hakikuonekana na watanzania Milioni!
Tuna tofauti gani na wao ambao wanampa mtu adhabu kubwa ya uhaini mtu aliyetamka tu TUTAKINUKISHA!
Nakubali yapo makosa makubwa wanafanya wanaharakati na viongozi tunaweza tukawaadhibu, hasa tunapojihakikishia 100% kuwa huyu hayuko upande wetu!!
Lakini makosa madogo yana handling yake ambayo sio lazima mvuane nguo hadharani na kuingiliana maungoni na kumtoa mates wako mchezoni
LABDA KAMA NAWEWE UNA AGENDA NA MASLAHI NA INTENTION YAKO BINAFSI🤷♂️
Na pia tujifunze kujishikilia, sio kila taarifa tunayopewa au kila kinachokuja kichwani kuhusu mtu fulani tunawahi harakaharaka kukipeleka mtandaoni!!
Tutakuwa hatuna tofauti na ma~content creator sasa
ndio siku ukikosa content au attention unalipika la kulipika hata kama la uwongo!
Politics is a numbers game.
Harakati inahitaji pia watu
na ushawishi.
Siri ni namba so tuwe wengi online na ground‼️‼️
Wizara ya mambo ya ndichi ina~deal na petty issues….badala ya ku~deal na vitu serious.
Waziri una deal na mashalove & Pipitilda
badala ya kulinda mipakani huko zinaingia pombe feki daily zinaenda kuua figo za maelfu ya mahomeboys na dada zetu, ajira zenyewe hamuwapi vijana wanashindwa kumudu dialysis gharama wanapoteza maisha!
Halafu hapo utasema wizara inalinda raia na mali zake!!?🤷♂️
Unazungumzia maadili ya kuongea lugha chafu mitandaoni, USA 🇺🇸 Rais Trump anatukanwa na raia ile F****word tena public kabisa kwenye press na raia haguswi na ndio nchi ina mahospital bora,shule na vyuo bora, umeme & maji havikatiki,barabara safi, na ajira za kutosha!!
Wewe maadili yamekusaidia nini mtu nina bachelor ya Architecture GPA 3.5 na naendesha boda tena ya mkataba mwaka wa nne huu kazi hamna, kwa siku naingiza elfu saba, utasema kuna maisha hapo?
Wewe unaekazania maadili una population ya watu milioni 70, unatangaza ajira elfu 45!!
Sasa kuna taifa hapo?
Simaanishi kama taifa tusiwe na maadili au utamaduni, lakini ni petty issues….. kundi la wale mates wangu walipaswa kuitwa hata basata tu wakamalizana nao chaap kwa, kama wazazi/walezi……easy tu, lakini sio waziri wa wizara!!
Kama tunataka kukemea maadili, tukemee maadili ya utekaji na ufisadi na mauaji ya ndugu zetu, hayo ndio maadili ya msingi na uwaite wahusika uwakemee live tuone kama tulivyoona kwa wale wasanii!!
Unaacha kuwaita askari walioua ndugu zetu october 29 uwakemee na kuwawajibisha, unamuita yule sista du anayeuza jeans, unamuita Nicole….kisa anaonyesha kifua!!?
Nini kifua babu, nchi za wenzetu unakuta striper anacheza uchi kabisa usiku club na mchana ni daktari / nurse anatibu watu na ndio ajira yake na analipa kodi na hela anayotengeneza humgusi….na ana degree kasoma na husikii kaitwa na waziri wala Mkuu wa mkoa! Dunia ndio ipo huko!!
CAG kila mwaka anasoma report wizi wa Billions of bags 💰 na huoni mtu akiwajibishwa…..sasa hayo ndio maadili ya kukemea public tena, sio mtuambie tunamalizana kwenye vikao vya kamati sijui za halmashauri…NO!!
Watu wanatekwa kiholela, wanapotea wanakufa….kila kiongozi anayehojiwa anakataa kuwa hakuna utekaji….husikii hata mmoja akikemea…..then leo wizara ya mambo ya ndani head liner unakaa kikao na GiGi money, Anko T unawakemea na mnalazimisha kabisa iwe news kubwa!!
Yani hukemei mtu anaua watu, unakuja unamkemea gigi kavaa mpasuo!?
Hivi tuna taifa kweli hapa jamani!?
Hii nchi ina maigizo sana!!
Nimekumbuka Dingi alikua na tabia siku ya kulipa ada, anakushikisha vibunda vyako mkononi mnaenda benki kufanya deposit. Yuko radhi akaidraw hio pesa aje nayo home asubuhi uibebe wewe mkononi mkaipeleke benki. Hio ndo lecture yake, hakuongeleshi tena kuhusu kusoma kwa bidii.
1. CDM imeruhusiwa kufanya siasa
2. TAL atatoka soon!!
3. Then watakaa mezani
4. Tume ya J.Chande itakabidhi report.
5. Report itakuwa iko balanced,
Itaipiga gavoo kimtindo(Kwa mbali)
6. Mchakato wa katiba mpya utatangazwa kuanza rasmi!!
Lengo kuu ni 👇🏻
Let’s buy time till 2030!!
Miaka mitano ni mingi sana lazima tuwe na activities za kuwaonyesha matumaini hawa raia hadi tufike 2030!!
Sasa unajua mchawi ni nani?
Mchawi ni ile namba 3 pale juu 👆
Pale kwenye kukaa mezani pale
ndio panaenda either
kusupport au kuvuruga hii plan!!
Trilioni 1 na bilioni 400 ya kuijenga/kuikarabati muhimbili.
Fedha hizi tukisema tusizipeleke tu Muhimbili, bali tuzigawe kwa kila mkoa nchi nzima kwenye sekta ya afya!!
1trilioni 400 bilioni
gawanya kwa mikoa 31
= 45,161,290,322
Kila mkoa utapata Bilioni 45 na milioni 160 kusaidia sekta ya afya!!
Kipi bora?
Ujenzi mpya wa muhimbili pekee?
Au fedha zikasaidie kila mkoa!?
Nikitazama calendar yangu
from
Nov 3rd, 2025 — Leo Feb 11th 2026
Zile siku 100 zimetimia leo!!
Vipe zile ahadi za siku 100 za kwanza kuna iliyotimia!??
Ile mikopo mmepewa??
Nyie bodaboda mliokuwa mnajazana kwenye kampeni zao mmepewa mitaji tayari?? mmeongeza hata boda ya pili?
Wasomi ajira mmepata?
Walimu/Manesi Mmeajiriwa?
Mishahara mmeongezewa?
Nyie mapolisi mnaotutesa na kutuua wamewaongezeeni mishahara??
Vipi hali ya maisha kiuchumi wameweza kuibadilisha? Kuna unafuu kidogo sasahivi eti ee?
Mahospital vipi huduma za matibabu na dawa zimepungua gharama?
Michango ya shule ya watoto wetu wameipunguza au bado mnalipia zaidi ya ada?
@KennedyMmari Stock ni miezi 3 na je utitiri wa kodi na tozo zilizowekwa je?maana sasa tunachangia hai hela za kupambana na Ukimwi na Bima ya afya kwa wote zinatoka kwenye mafuta
Mnaposema vijana wa kitanzania (Gen Z) wanashawishiwa na watanzania walioko nje inamaana nyie mmepoteza ushawishi (Influence)
Inawezekana vipi washawishiwe na watanzania wachache walioko nje ambao hawazidi hata 10!!
Hamuoni kama nyie ndio mna shida hapo?
TATUENI HIYO SHIDA KWANZA, TAFUTENI HUO MZIZI NA KIINI CHA TATIZO!!
Na sio kutafuta excuse za kudanganya watu kuwa ushawishi unatoka nje!!
Kwanini nyie mnashindwa kuwashawishi wakati mna wapiga kura Milioni 32?
Hawa watu milioni 32 ni wengi sana kuzidi watu 10 walioko nje ya nchi….kwanini hao wasiwashawishi vijana?
Nyie mnamiliki na kucontrol media house karibu zote (Radio,Tv, Online) hadi media za watu binafsi kubwa na ndogo nchini, na watangazaji wake na waandishi wake wote ni wa kwenu!! Vipindi vyao vingi wana wanadi nyie na sera, ilani, na miradi yenu.
Kuna chombo chenye ushawishi kuzidi media? Kwanini Gen-Z wasisikilize hizo media zenu wachague kuwasikiliza hao watu 10 walioko nje?
Wasanii wooteee wa muziki na filamu A list, B list hadi legends & Undergrounds ni wakwenu na mnawamiliki na kuwatumia nyie mnavyotaka!!
Kila wakati mnawatuma cha kupost, cha kuimba, cha kuigiza, na wengine hufanya press mnawaelekeza nini cha kuongea.
Kwanini Gen Z wasiwasikilize hao wasanii na kuwafatisha wanachowaagiza!!
Hawana influence au?
Mna police, jeshi ni la kwenu, usalama wa kwenu, magereza,
mahakama, uhamiaji, takukuru vyote vyenu. Hivi ni vyombo nyeti sana.
Kwahiyo hivi vyombo vyote vinazidiwa ushawishi na watu 10 walioko nje?
Unadhani kwanini
Gen - z & watanzania wachague kutovisikiliza hivi vyombo na kuamua kumsikiliza na kumfatilia Sativa?
MNAKOSEA WAPI? KWANINI MMEPOTEZA USHAWISHI?
Mna wabunge nchi nzima, bunge lote limejaa wanachama wenu……hapo sijasema serikali za mitaa wala madiwani!!
Kwanini bunge live linapata watazamaji 200, wakati mange dashboard yake IG inasoma views 130M kwa mwezi!!
Kwanini watu hawalisikilizi bunge wanaenda kumsikiliza Mange?
MNAKOSEA WAPI?
Nyie si mna watu milioni 32, hao watu hawana bando? hawana tambo?
Taasisi za dini nyingi mmezinunua zihubiri mnachotaka nyinyi na kila siku wanatoa matamko na kuhubiri kile kinachowafurahisha
Kwanini Vijana wanazi-ignore na kuchagua kumsikiliza Recho dangwa!?
MNAKOSEA WAPI?
CCM na Serikaki mna power lakini hamna INFLUENCE!!
Chama na uongozi hauna watu wenye infuence tena mbele ya vijana (GEN-Z)
NA HILI NDIO ANGUKO LENU!!
Wiki nzima tangu niachiwe na polisi, nimekua nikidai Paspoti yangu ili nisafiri kwaajili ya kupata matibabu bila mafanikio.
Hakuna sababu yoyote ya vyombo vya dola kuendelea kushikilia paspoti yangu.
Nafanyiwa haya kwasababu ya msimamo wangu wa kisiasa, nimeona ni muhimu niwajulishe Watanzania na dunia kuhusu huu unyama wa kujaribu kuninyima haki ya kupata matibabu.
Mtu aliyekwambia hakutakuwa na NYWINYWI wala NYWI NYWI NYWI!!
Leo anakwambia amesikitishwa na ataunda tume ichunguze hayo mauaji!!
You had a chance ya kuzuia haya mauaji!
But you didn’t, in stead you choose to remain silent and bless them to continue.
Perhaps if you had made the decision on the first day before the 30th, you would have saved a lot of blood from our brothers.
Lakini uliacha namba iendelee kuwa kubwa huku ukijiapisha!!
On your inauguration ceremony ulitupa speech ya kuzidi kutuumiza na kututisha na sio kutuponya machungu ya ndugu zetu!!
Ukasema vurugu hupelekea kujihami na kupimana nguvu!!
So mlikuwa mnapimana nguvu na kile kichanga hakina hata mwaka?
Mlipimana nguvu na wale mabinti wa miaka 19-23 tena wakiwa kwenye makazi yao mkamwaga damu zao?
Mlipimana nguvu na watu waliofatwa kuuliwa majumbani?
Kwanini hukutoa tamko nyakati hizi?
Siku ya kuapishwa yule mzee wa kipentekoste na yule father wa Roman Catholic ndio walionyesha concern.
Lakini wewe speech yako haikutu-comfort, zaidi ya kutuongezea Trauma!!
Sasa mnakuja na story zile zile za kuundwa Tume!!
Tume which? Tume what? Tume who!?
Tume ya shambulio la Lisu ilileta majibu gani? Miaka 8 now ishapita!!
Tume ya mauaji ya mzee Kibao imeleta majibu gani hadi leo?
Tume za sisi tuliotekwa miaka 8 imepita zimewakamata wahusika gani so far?
Utekaji umeisha?? Si bado unaendelea hadi sasa!! Means watekaji wapo mitaani still!! Sasa Tume imefanya nini?
Mnatengeneza tatizo makusudi, then baadae mje kuwahadaa wananchi kwa huruma za uwongo!! ❌❌❌❌
You won the millennials generation
BUT NOT THIS #GEN_Z
Nilipokuwa lockup Osterbay, sero ya pembeni yangu kulikuwa na wasichana wengi wadogo wa kike walikuwa wanaomba na kuimba.Nafikiri waliimba na kuomba usiku kucha na asubuhi pia. Nami nikajikuta nasema moyoni , hata kama Mungu yuko busy sana huko aliko , lakini nina uhakika kuwa haya maombi ya hawa watoto atakuwa ameyasikia. Nafikiri sijawahi kufikiri kuwa kuna watu wanaweza kuomba muda mrefu hivyo , nami nikakumbuka neno hili “
2 Mambo Ya Nyakati 7:14
“ ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekesha, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao”
Walioharibiwa mali wanapewa media coverage waongelee uharibifu huo!!
Waliouliwa ndugu zao na wanaodai
miili ya ndugu zao na majeruhi wanaouguza vidonda wanakuwa silenced wasiongee wala kulalamika popote!!
Binafsi nuangana na waliopoteza mali zao, na sisupport uharibifu na uwizi wa mali za wapambanaji wenzetu, Na haipaswi kuwa hivyo!! Mungu awafanyie wepesi🤲
Lakini haswa naungana zaidi na waliopoteza ndugu zao!!
Uhai una thamani zaidi ya mali!!
Mali zinatafutwa lakini uhai ukitoka umeondoka!!!
Men,
Name your best barber and barbershop.
Where is he located?
Do you have his contacts and address?
Comment in the replies.
Promote him.
Retweet widely.
A barber shop is a masculine space.
#MasculinitySaturday