Wanangu wa Kigamboni Jumamosi kiwanja cha bata ni kimoja tu THE BROSKIES LIQUOR 🍻🥩🍖
📍: Kisota road
Dressing code: 90’s
Kuanzia saa 6 mchana
Njoo tuimbe na kusikiliza nyimbo zetu zamani huku tukitengeneza connection
Tangazo,
kwanza ukiona posti hi wewe mzalendo Reposti 🪱
wa Tanzania wote napendekeza tuchange pesa kwaajili ya wapambanaji hawa hawatakiwi kuteseka wakiwa gerezani wapo kwaniaba yetu tuungane nao
-Nguo
_Subuni
na mahitaji mengine
tupate mtu wakupokea na kusambaza,
Ujumbe kutoka gerezani wa Mh. @TunduALissu
Jaji Hamidu Mwanga ni Jaji wa Samia, na kwasababu hiyo ni Jaji wa CCM na anafanya kazi ya CCM. Jaji Mwanga alikuwa kwenye Tume ya uchaguzi Zanzibar (ZEC) ya Jecha Salimu Jecha ambayo ilifuta uchaguzi wa Zanzibar wa 2015. Jaji wa namna hii tutatarajia aipende CHADEMA inayosema No reforms No election?????
Maamuzi yake yanathibitisha kauli yangu kwamba Majaji wengi ni Ma-CCM na wanafanya maamuzi kuipendeza CCM na yule anaeweza kuwapandisha madaraja kwenda Mahakama ya Rufani.
Kuhusu kuzuia shughuli za Chama; Chama ni wanachama, sio majengo, hata kama majengo ni muhimu lakini chama ni wanachama na wanachama waendelee na mapambano katika majukwaa yote yanayopatikana hasa katika mitandao ya kijamii isipokuwa katika jengo la Makao Makuu.
Wanachama wakumbuke historia ya mapambano ya aina hii. Chama cha ANC kilipigwa marufuku na serikali ya makaburu kwa miaka 30, viongozi wake wakuu ama walifungwa maisha Robben Island kama Mandela na wenzake au walikimbilia uhamishoni kama Oliver Tambo, Thabo Mbeki na wengine.
Hayo yote hayakuzima mapambano ya ukombozi kuendelea na hayakuiua ANC. Uamuzi wa Jaji Hamidu Mwanga hautazuia mapambano kuendelea wala kuiua CHADEMA.
ALUTA CONTINUA
-Admin
CCM wamevunja katiba yao kwenye upatikanaji wa mgombea wa urais mnqjichekesha tu ila msajili anataka kuipangia CDM nani wawe viongozi, sio CDM hii kudadeki.
#Mei28 ni mojawapo ya siku muhimu katika kuanzishwa kwa @ChademaTZ2 . Siku ya kwanza ni siku ya Chadema kupata usajili kamili 21 Januari 1993, hii ndio Chama kimeichagua kuwa rasmi ya kuadhimisha kuzaliwa kwa #Chadema .
Siku ya pili ni tarehe ya Mkutano Mkuu wa Kwanza kupitisha rasmi kuanzishwa kwa Chadema na kupitisha Katiba ya kwanza ya Chadema. Hii ni tarehe 28 Mei 1992. Nitashukuru ikiwa kuna ambaye ama alikuwa katika mkutano mkuu huo au anafahamu masimulizi ya mkutano mkuu huo akatuandikia hapa kwa ajili ya kukumbusha historia ya tulipotoka.
Siku ya tatu ni ile ya kikundi cha watu wachache kilipokaa na kuja na wazo la kuanzisha Chama cha siasa na kuanza mchakato wa kujadiliana majina na hatimaye kuja na jina la Chadema. Kamati ya wachache iliundwa kwa ajili ya kuanza kuandika katiba na kuanza kuandaa mkutano mkuu. Mwenye historia ya mchakato huo naye nitashukuru akituandikia.
Mkutano Mkuu wa tarehe 21 Januari 2025 ulipitisha maazimio mawili muhimu kwa historia ya Chadema: 1. Kuwaenzi waasisi 2. Kuwaenzi waliomwaga damu kwa ajili ya Chadema.
Katika orodha ya waasisi kwa maoni yangu majina matatu nayaona yenye kustahili kuenziwa: Edwin Mtei, Bob Makani na Freeman Mbowe. Mwasisi gani mwingine kwa maoni yenu anastahili kuenziwa?
Kwenye orodha ya mashujaa waliomwaga damu wenye kustahili kuenziwa kwa maoni yangu nawaenzi: Ali Kibao, Alfonce Mawazo na Daud Mwangosi. Nani wengine wanastahili kuenziwa?
Kumbukumbu ya kuanzishwa kwa Chadema haiwezi kukamilika bila kuitaja pia tarehe 13 Agosti 2006 siku ya Chadema kuzinduliwa upya. Siku hiyo pamoja na mambo mengine tulizindua katiba mpya, bendera mpya, mabaraza mapya, itikadi mpya na mpango mkakati mpya. Nayakumbuka maneno yetu siku hiyo Ukumbi wa PTA: tulizindua #TumainiJipya . Tulitamka kuwa Chadema ni imani, matumaini na mwelekeo.
Tarehe 21 Januari 2025 iliendeleza historia hiyo. Chadema is spirit. Chadema spirit haiwezi kuuwawa kwa viongozi kuzuiwa au kunyimwa ruzuku na watawala. Chadema ni #NguvuYaUmma #PeoplesPower #ToneTone #NoReformsNoElection #StrongerTogether
Ruzuku ambayo MSAJILI amesitisha kwa CHADEMA ni kiasi cha Tsh. 107 Milioni kila mwezi. Ni wastani wa watu 10,700 kila mwezi wakichangia Tsh. 10,000 au watu 50,000 wakichangia Tsh. 2,140 kila mwezi. Tuweke nguvu katika #ToneTone tuachane na masimango ya MaCCM na DOLA. ASITUTISHE!
Kama CDM haina mvuto,imesambaratika,haipendwi, sisiemu mnaogopa nini kufanya reforms ukafanyika uchaguzi wa huru na haki mkaithibitishia dunia maneno hayo? mnaogopa nini?