HABARI:
Katibu wa CHADEMA Jimbo la handeni Mjini, Kombo Mohammed Ali Matunda, ameeleza kuwa ana mashaka kuhusu msimamo wa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, hasa katika suala la mwenendo wa kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Taifa, Tundu Lissu.
Amesema Lissu amekutwa na kesi ya kujibu kutokana na matamshi yanayohusishwa na uchaguzi, huku akidai kuwa baadhi ya kauli hizo pia zimewahi kutolewa na Makamu Mwenyekiti wa chama.
Kombo amemshauri Makamu Mwenyekiti kukubali meza ya mazungumzo na mihimili inayohusika, akiamini kuwa mazungumzo yanaweza kusaidia kupatikana kwa suluhu na hatimaye Lissu kuwa huru na kuungana na familia yake.
Amesema ana wasiwasi kwa kuwa Lissu anaendelea kukaa ndani, huku akiomba viongozi wa chama kuweka nguvu zaidi katika mazungumzo, akisisitiza kuwa ushindi wa chama haupaswi kutenganishwa na juhudi za kutafuta suluhu.
Taarifa kwa Umma.
Leo ndugu yetu @malisa_gj alikuwa anarejea nyumbani kutokea Nchini Marekani, alikokuwa amekwenda kwa Program maalum ya wamarekani kupeleka viongozi vijana, nitaeleza kesho kwa kina
Malisa alishukia Nairobi na kisha kubook ndege nyingine ya Shirika la Flightlink iliyokuwa itue uwanja wa ndege wa kimataifa Kia majira ya saa Sita mchana.
Wafanyakazi wa uwanja wa ndege wa Jomo Kenyata airport wana mgomo ulioanza siku ya jana na mgomo bado unaendelea hali iliyopelekea mashirika ya ndege yanayotumia uwanja wa Kenya kufungwa kutokana na mgomo huo.
.
Sasa ndugu yangu alinipigia simu na kunielezea hali hiyo tukashauriana kwasababu Kenya siyo mbali nikamshauri kwasababu hatujui mgomo utakwisha lini nikamwambia achukue Bolt aje mpaka Count ya Kajiado ambapo na mimi niliendeshq gari kutoka Moshi mpaka Kajiado, nikamchukua tukaanza safari ya kurudi nyumbani tukafika Namanga majira ya saa 10 jioni akafanikiwa kugonga passport upande wa Kenya na alipofika upande wa tz wakachukua passport yake na kumwambia aingie ndani kwasababu passport yake haionekani kwenye mfumo.
Nimekaa nae pale mpaka majira ya saa tatu kasoro ambapo maafisa uamiaji kwa kushirikiana na watu wengine ambao hawakuwa na sare walimchukua Malisa wakasema wanampeleka kituo cha Polisi Longido, nikaenda mpaka Longido, nilipofika pale nikamuulizia kwa askari aliyekuwa zamu akasema pale hajapelekwa, lakini akaniambia gari ilyokwenda kumpakia aina ya Hillux double cabin ilipita kituoni wakati wanakwenda Namanga walivyorudi hawakusimama gari ilipitiliza ikiwa kwenye mwendo Mkali. Nimefika kituo cha Polisi Arusha wamesema hajaletwa hapa, nimeondoka naelekea kituo cha polisi Moshi,
Ni wito wangu kwa Askari wa Uamiaji watueleze ndugu yetu yuko kituo gani ili tuweze kumpatia Chakula, Jeshi la uamiaji ndio watu pekee wanaojua alipo ndugu yetu maana wao ndio waliomshikilia mpaka anachukuliwa Namanga.
.
Malisa ni mtu mwema sana sana hanaga shida na mtu hakustahili haya anayotendewa.
‼️Alert‼️
Nimejulishwa kwamba waliomuweka Emmanuel Nchimbi chini ya ulinzi, wamempeleka Dodoma na sasa wanaandaa hafla ya makabidhiano ya ofisi so siku yoyote kuanzia kesho, ataonekana hadharani akimkabidhi ofisi kijana wa Nduli Idd Amin Mama.
Wameamua kufanya hivi kwasababu wameona kelele zimekuwa nyingi kwenye mitandaon kuhusu.
#WhereIsNchimbi #FreeEmmanuelNchimbi
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, pamoja na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Godbless Lema, wamelitaka Jeshi la Polisi kutoa taarifa kuhusu alipo mwanaharakati na mwanachama wa chama hicho, Godlisten Malisa pamoja na sababu za kushikiliwa kwake.
Malisa anadaiwa kukamatwa Agosti 31, 2026, muda mfupi baada ya kuwasili katika eneo la Namanga akitokea Kenya, huku taarifa za awali zikidai kuwa alichukuliwa na gari aina ya Double Cabin isiyokuwa ya Jeshi la Polisi.
Akizungumzia suala hilo leo, Septemba 1, 2026, kupitia ukurasa wake wa Instagram, Heche amehoji mazingira ya kukamatwa kwa Malisa na kutaka kufahamika kituo cha Polisi alichopo ikiwa anashikiliwa na Polisi ili ndugu, marafiki, mawakili na wanachama wenzake waweze kumfikia kwa mujibu wa sheria.
Heche amesema Malisa alikuwa akisafiri kutoka Marekani ambako alikuwa amekaa kwa zaidi ya miezi tisa, na kwamba baada ya kukwama Nairobi kutokana na mgomo wa wafanyakazi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, alisafiri kwa njia ya barabara hadi Namanga ili kuingia Tanzania kupitia Arusha.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Wakili Dickson Matata, Malisa alipofika Namanga alifika katika ofisi za Uhamiaji kwa ajili ya taratibu za kuingia nchini, lakini maafisa walimweleza kuwa hati yake ya kusafiria haikusomeka kwenye mfumo na kwamba walihitaji kusubiri mkuu wao ili kutatua changamoto hiyo.
Wakili Matata alidai kuwa baadaye Malisa alichukuliwa na gari jeupe aina ya Double Cabin, ambalo alisema halikuwa gari la Polisi. Taarifa hiyo ilisema simu za Malisa zilizimwa na hadi wakati wa kutolewa kwa taarifa hiyo haikufahamika alikokuwa.
Akitoa maoni yake kupitia mtandao wa X, Lema amemlenga Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), akimtaka kutoa taarifa ya wazi kuhusu alipo au sababu za kushikiliwa kwake.
Lema amesema kushikiliwa kwa Malisa kunaweza kuongeza taharuki, kuvuruga imani ya wananchi kwa Jeshi la Polisi na kuitia taasisi hiyo katika mazingira ya kukosolewa na umma.
Amesema Jeshi la Polisi linapaswa kuwa chombo cha kutuliza hofu na kujenga imani kwa wananchi, badala ya kuacha wananchi wakibahatisha hatma ya mtu aliyekamatwa.
Kwa mtazamo wake, usiri usio na sababu unaweza kuongeza mashaka miongoni mwa wananchi, huku akionya kuwa mashaka yakiachwa kukua yanaweza kuwa na gharama kubwa kwa Taifa.
Kauli za Heche na Lema zimekuja wakati suala la Malisa likiendelea kuzua mjadala kwenye mitandao ya kijamii, huku wito mkubwa ukiwa kwa mamlaka husika kutoa taarifa rasmi kuhusu alipo, sababu za kushikiliwa na hatua za kisheria zinazochukuliwa dhidi yake.
Iko hivi MALISSA ana kesi ya makosa kimtandao alishaitwa Polisi kupitia wakili Matata na walijibu yuko nje, Matata alimuwekea dhamana ila Malissa alikaa nje kupitiliza muda. Matata akajitoa kumdhamini so leo karudi Kinyemela kupitia mipakani ndo Polisi wakaomba AKAMATWE AHOJIWE
KATUGA BABA 🔥🔥🔥
⚫️Katuga: Ulisema, “Tutasababisha matatizo,” “tutasimamisha uchaguzi,” na “tutachochea uasi”, kauli ambazo zilirekodiwa kwenye video.
Je, uliwahi kusema katika ushahidi wako kwamba kauli hizo si zako na kwamba video hiyo yote ilipaswa kutazamwa ili kuzifahamu?
🔴Lissu: Kwa mujibu wa maneno ya mashahidi wako…
⚫️Katuga: Siwezi kutumia maneno hayo yako. Una akili timamu. Ulisema hayo si maneno yako, sivyo?
🔴Lissu: Siyakanushi, na hakuna tatizo.
IGP, mantiki gani hii ? Mnamkamata mtu, hamtoi taarifa ya wazi alipo wala sababu ya kumshikilia, mnaacha hofu na tension isambae kila kona, halafu baadaye mnatokea kusema, “Ndiyo, sisi tunamshikilia.”
Hii ni calculus gani? Inasaidia nini kwa Nchi zaidi ya kuongeza taharuki, kuvuruga imani ya wananchi na kulitia aibu Jeshi la Polisi ?
Jeshi la Polisi linapaswa kutuliza hofu, si kuizalisha. Linapaswa kujenga imani, si kuacha wananchi wabahatisha hatma ya mtu aliyekamatwa.
Kama mtu amekamatwa kihalali, semeni yuko wapi, kwa kosa gani na hatua gani za kisheria zinaendelea. Usiri usio na sababu huzaa mashaka, na mashaka yakiachwa yakue, gharama yake ni kubwa sana kwa Taifa.
POLISI WAHESHIMU SHERIA:
Ukamataji wa Watuhumiwa unapaswa kufanyika kwa KUZINGATIA SHERIA. Mara kadhaa POLISI wamekuwa WAKIWANYIMA HAKI watuhumiwa wanaokamatwa. Jambo hili ni KINYUME na SHERIA na UBINADAMU. Asante kwa kuwa MALISA,G.J yupo SALAMA.🙏
Kuna mtu anasema maumivu ya hawa watu ni kwasababu ya Nongwa ya Rais kutoka Zanzibar!!!!
Kwamba hawa watu wanalia kwasababu tu ya Nongwa sio?
Na huo ndio msimamo wa taasisi yenu?
Magufuli tuliempinga kwa udikteta a ukatili wake mpaka akafanya jaribio la kumuua Lissu alikua anatoka Zanzibara pia au?
Tunazidi kufahamiana.
#FreeNchimbi#FreeEmmanuelNchimbi
Still no sign of Nchimbi and no communication
Kama makamu wa Rais anafanyiwa hivi sasa nyie machawa kajamba nani mnavyotutukana mnajiona moo salama? Yatawafikia na kwa matusi na kejeli mnayomwaga tutabaki kuwaangalia tu!
Mmekosa hata utu!?
Eniwei Nchimbi mwachieni - mmeshapigwa - take it on the chin
#SamiaMustGo
Tundu Lissu: Mtu akisema ‘msimamo huu unaashiria uasi’ anakuwa ametenda kosa gani la jinai kwa mujibu wa ufahamu wako?
John Mnyika; Hakuna kosa analokuwa ametenda
Job Mrema; Waheshimiwa Majaji hilo swali linauliza ushauri tunaomba liondolewe
Tundu Lissu; hiyo hoja haina maana yoyote Waheshimiwa Majaji
Jaji; Hebu rudia swali
Tundu Lissu; Mtu akisema msimamo huu unaashiri uasi kuna kosa?
John Mnyika; sioni kosa kwa sababu Mwl. J.K. Nyerere aliwaambia vijana “Tunataka vijana waasi dhidi ya mifumo kandamizi, ubwana na ufisadi katika Taifa” na hakukamatwa
John Mnyika’s answer is the real chef’s kiss.👏
HAKI KWA MALISA,G.J:
Ukamataji wa watuhumiwa ambao HAUFUATI Sheria, ni UTEKAJI. Kwa namna zote, MAMLAKA za Serikali ZINAWAJIBIKA kuhakikisha MALISA,G.J anakuwa HURU na SALAMA kwa kuzingatia misingi ya SHERIA na UTU.
Wadhifa wa Makamu wa Rais kwa Dk Emmanuel Nchimbi, ulikoma rasmi Agosti 26, 2026 baada ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutangaza kumfukuza uanachama, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Hamza Johari amelieleza Bunge.
#mwananchiupdates#tunawezeshataifa
Mheshimiwa EMMANUEL KINGU (Mbunge) ni mmoja wa MANABII wa kweli WACHACHE SANA ambao Tanzania IMEBAHATIKA kuwapata. Angalia UNABII huo 👇 ULIVYOTIMIA. 😂😂
Leo 26 Agosti 2026 mahakamani:
Katuga: Ulisema kuna mambo yamekukuta kwenye mapambano yako? Nitakuwa sahihi nikisema kuwa wewe ni mtu mwenye chuki dhidi ya serikali.
Tundu. Lissu: Nina chuki na serikali ya nchi hii kwasababu imeonea watu wengi.
Katuga: Kwahiyo ulisema yote hayo una chuki na serikali?
Tundu Lissu: Nina chuki dhidi ya uonevu wa serikali. Ninayo chuki dhidi ya serikali sahihi kabisa. Wanaonea sana watu.
Huyu ndo Tundu Lissu ✊🏽🔥
#FreeTunduLissuNow
VIDEO:
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinachokutana leo, Agosti 26, 2026, kinafanyika wakati mjadala kuhusu hatma ya Dk. Emmanuel Nchimbi ukiwa umechukua sura mpya, baada ya jana, Agosti 25, kutangaza kujiuzulu nafasi ya Makamu wa Rais pamoja na kustaafu siasa na utumishi wa umma.
Uamuzi huo unakuja wakati ambapo historia yake ndani ya CCM imewahi kuhusishwa na hatua za kinidhamu.
Mwaka 2017, Nchimbi ambaye wakati huo alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Balozi wa Tanzania nchini Brazil, alipewa onyo kali na NEC baada ya chama kumtuhumu kwa makosa yaliyohusishwa na mwenendo wake katika mgogoro wa uteuzi wa mgombea urais wa CCM mwaka 2015. Aliagizwa pia kuomba radhi kwa wanachama na uongozi wa CCM, jambo ambalo Katibu wa Itikadi na Uenezi wakati huo, Humphrey Polepole, alisema alipaswa kulifanya akiwa Brazil.
Katika hatua hiyo ya kinidhamu, Nchimbi pia alifungiwa kwa kipindi cha miezi 12, hali iliyomfanya kukosa sifa za kuwania uongozi ndani ya CCM kwa kipindi hicho. Polepole alieleza wakati huo kuwa adhabu hiyo ni kutokana na mwanachama huyo kurudia kosa lilelile bila ya kujirekebisha.
Jina la Nchimbi pia liliingia kwenye mjadala huo pamoja na la Sophia Simba baada ya wote kuhusishwa na kutoridhishwa na uamuzi wa Kamati Kuu wa kumuondoa Edward Lowassa katika mchakato wa uteuzi wa mgombea urais wa CCM mwaka 2015. NEC ya Machi 2017 ilimvua Simba uanachama, huku Nchimbi akipewa onyo kali.
Historia hiyo inarejea pia katika mazingira ya taarifa zilizozagaa siku chache zilizopita kwamba Nchimbi aliitwa mbele ya Kamati ya Maadili ya CCM. Hata hivyo, si mara ya kwanza jina la Nchimbi kuhusishwa na vikao vya maadili, kwani hata mwaka 2017 mjadala wa hatua za kinidhamu ulihusisha vikao vya juu vya chama na tuhuma za kukiuka maamuzi ya chama.
Sasa, wakati NEC ikikaa leo, kujiuzulu kwa Nchimbi kunafungua ukurasa mpya katika safari yake ya kisiasa na kuibua maswali kuhusu hatua zitakazofuata ndani ya CCM. Kinachosubiriwa ni iwapo kikao hicho kitajadili moja kwa moja uamuzi wake wa kujiuzulu na mustakabali wake ndani ya chama, huku historia ya adhabu aliyowahi kupewa, ikiwemo kufungiwa kwa kipindi cha miezi 12, ikifanya suala hilo kuwa moja ya masuala yanayofuatiliwa kwa karibu katika kikao cha leo.
ALERT: Hakija fahamika kilichomuua, lakini mpishi wa makamu wa Rais alilazimishwa kumuwekea Sumu makamu wa Rais Dr. Emmanuel Nchimbi kwenye chakula, kitendo ambacho mtumishi huyo alikikataa, na baadaye yeye mpishi kufa katika mazingira yasiyoeleweka.