Hii posti ndio ilikuwa mwanzo wa mimi kuanza kutofautiana na kimama. Yani hii posti niliiandika huku natetemeka kwa uchungu na hasira ila bado nilikuwa nataka kumpa chance kimama so nikajitahidi nikaiandika kwa heshma na kumuita “Mama Samia”.
Nilishindwa hata kumlaumu yeye nikawa najaribu kulaumu watu waliomzunguka ili apate message bila mimi kumchafua yeye au kumwaribia kwa wananchi au kumvunjia heshima.
Ila kama baada ya kuona hii posti haikubadilisha chochote ndio nikajitoa akili na kubadili gia hewani mazima, nikamchamba,nikawambia anarembua macho kama changu huku nchi inauzwa na wahuni. Niliweka posti double double nachamba.
Hii issue ya bandari ndio ilifanya mwanae Abdul akapanda ndege mpaka Los Angeles kuongea na mimi face to face maana kwenye WhatsApp alishindwa kuni convince ili niwasapoti uuzaji wa bandari. Yani Abdul alitaka nifanye kama kina Maulid Kitenge na machawa wao walichokuwa wanafanya, kudanganya wananchi kuwa it’s a good deal for the country.
Nilimwambia siwezi kufanya hiko kitu unless mbadilishe mkataba uwe na kikomo tena kikomo cha miaka michache hapo labda nitaweza kuunga mkono, ila kusema kwamba niende kwa Watanzania nikawadanganye juu ya hili hiko kitu siwezi , hata mnilipe nini siwezi, akaniuliza “really huwezi no matter what? Nikamwambia siwezi sababu nimejijengea imani kubwa kwa Watanzania siwezi kuiharibu.
Tukaagana kuwa nijifikirie zaidi. And I never changed my mind ndo kwanza nikazidisha kupinga.
Hawakuamini wanachokiona.
SOMO: Kwenye maisha usikubali kuuza utu wako au kuwauza watu wanyonge wanaomlilia Mungu, watu waliokuamini na kukutegemea uwatetee eti kisa pesa. ITS NEVER WORTH IT. Si hiyo pesa yao niliikataa ila Mungu akaniletea hiyo pesa kwa njia ingine, kaniletea mwanaume mwenye hiyo pesa na sasa naishi vizuri sijui shida inafafanaje. GOD WILL ALWAYS PROVIDE..Nimepoteza biashara yangu na kila kitu ila Mungu akasema nope nakuletea mtu wa kukustiri, una roho nyeupe sitoruhusu udhalilike. Na inawezekana kama ningefanya ushetani kwa Watanzania kisa pesa leo labda ningekuwa nimekutwa hata na laana au balaa kubwa.
Sijui kama ni mapema sana ila, tunahitaji mbinu za kidigitali za kudumu za namna ya kuwaadhibu watu (influencers, socialites, musicians, & celebrities) wote wanaolipwa na serikali kueneza uongo, uzushi, na kusifia udhalimu
We need to cancel them.
Nikielezea umuhimu wa #NoReformsNoElection kama kijana msomi nilieamua kutumia elimu yangu kuchangia maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa katika taifa langu.
Follow me🙏 support movement 💪
#Tutashinda
Natangaza kuwa kesho Nitasali kanisa la UFUFUO NA UZIMA UBUNGO.
Ibada itaongozwa na ASKOFU GWAJIMA.
Karibuni sana WAPENDA HAKI WOTE.
REPOST 200🔥🔥
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Do your best and God will do the rest 🙏🏽
Napambana kadri ya uwezo wangu, mi ni binadamu dhaifu, ila kwa yote ninayopambana nayo atanivusha Mungu
Nawashukuru wa upendo wenu
Thank you all for your love and support ❤️
For now we push
#NoReformsNoElection#FreeTunduLissu
#FreeAllPoliticalPrisonersinTanzania
#StopAbductionsTz
Na #TutaelewanaTu
Polisi, usalama, mahakama, msajili michezo..
Nini hawajatumia kujaribu kufifisha nguvu ya wananchi kudai mabadiliko kwa kutumia #NoReformsNoElection .
Nimezunguka mikoa karibia yote ya Tanzania, tumepata shida nyingi, majaribu na hata kuumizwa lakini tumeona kiu kubwa ya wananchi kutaka mabadiliko.
Tabora tulinyimwa uwanja, ukaruhusiwa kutumika saa tano, mkutano jioni saa nane, mkutano umetangazwa masaa mawili na uwanja ukatapika watu.
Tunawashukuru Watanzania kwa michango yenu tumeweza kusafiri, kula na kulala.
tutaongea na nyie mda sio mrefu.
Chama chenu kiko imara zaidi, tutaishida vita hii dhidi ya udhalimu, dhuluma, utekaji, uporaji wa mali za umma, umasikini na ufisadi. Tutashinda na tutashangilia pamoja.