@MarekaMalili Ukiwa na site ya ujenzi, utakutana na chupa nyingi sana za energy drink, pia maeneo ya shule za boarding, stand na masokoni wanatumia sanaa. Hii ni aina mpya ya ulevi. Ichunguzwe.
Mbona kama tume inaendelea na kazi, au mpaka maamuzi yatolewe.
Hii case haifanani na case ya chadema, mpaka wakasimamishwa kufanya mikutano ya hadhara?
@judiciarytz imepanga kusikiliza kesi ya Kupinga Uteuzi wa tume tarehe 10/02/2026 baada ya muda wa Tume kuisha.
Bila kujali maslahi mapana ya kesi na kuzingatia hati ya dharula, Wakati wa likizo kuna Jaji huwa anabaki kwa kesi za dharula kama hizi.
Wenye akili wanaelewa! ๐๏ธ๐๏ธ
Inawezekana ikawa ni kweli. Lakini mbona tukiwapeleka hawa tunaowajua, tunaowaona mambo hayo hayajawahi kutokea na kutendeka kwao.
Ina maana utukufu, utimilifu, fadhili, huruma, rehema, neema na kudra za Mungu wetu ni za upendeleo?
Alisoma Peramiho girls na Chuo cha Ualimu Korogwe. Akafundisha Songea Girls na VETA kisha akaingia kwenye siasa. Akawa Mbunge kwa takribani miaka 25 akiwakilisha jimbo la Peramiho, pia akahudumu kama Waziri na Naibu waziri wa karibu Wizara 5 tofauti. Jenista Mhagama amefariki.
Huwezi kuwa msanii wa watawala wakati huo unataka soko la wananchi. Haiwezekani. Hii ni kanuni ya kawaida. Msanii anachagua hadhira yake mwenyewe. Kama watawala na Serikali yao ndiyo soko lako lilipo, wauzie bidhaa zako. Wananchi watawatafuta wasanii wao, watanunua bidhaa zao.
@PMadeleka Moja kati ya wizara hewa ni hii ya aweso. Nadhani panatakiwa mabadiliko ya mfumo ya uendeshaji wa mamlaka za maji. Hakuna kitu zinafanya.
Wamerundikana kama kondoo kwenye ofisi za umma na hakuna output yeyote. Nchi haina hata jangwa lakini maji ni shida.