Mbogamboga yoyote anaweza kuwa VP, kwa sababu hakuna aliyewachagua, hata Chalamila au Magoti wanaweza kuwa! Mbogamboga yoyote anaweza wala sio lazima uwe na akili!!!
Hata nabii Tito kama ni mwanachama anaweza tu!!!
Niliandika hii posti kuhusu Nchimbi miaka 2 iliyopita. Niliwaambia Watanzania miaka 2 iliyopita kuwa CCM lazma watamuondoa Nchimbi….
I was 100% sure kuwa yoyote ambae ni old school CCM nikimaanisha wenye mentality kama za kina Mzee Kingunge hatokubali hizi siasa zinazoangamiza nchi na wananchi wake…..
MaCCM wa zamani walikuwa ni wadokozi tu ila kuna sehemu ya mioyo yao ilikuwa ina bleed Tanganyika and no money in the world could make them sell out.
Hawa vijana wa CCM ya leo ni mambwa koko, wanaangalia nchi inapukutuka wao wanajali vyeo tu…
Watanzania ile CCM tuliyokuwa tunaijua haipo tena. Ukimuona Mtanzania bado anavaa nguo za CCM, mpeleke Mirembe ana matatizo ya akili huyo….
CCM imekata moto…..
Mahakama haipaswi kuhitaji ujasiri wa ajabu kusema kwamba Mkti Tundu Lissu hana kesi ya kujibu. Kwa ushahidi uliowasilishwa mahakamani, hakuna msingi wa kimantiki na kisheria wa kusema kwamba ushahidi huo umejenga kesi ya kujibu. Kilichoshuhudiwa mara nyingi ndani ya Mahakama kilionekana zaidi kama vituko kuliko ushahidi wenye mashiko unaoweza kumfanya mtu awe na kesi ya kujibu.
Katika mazingira kama haya, kusema kwamba Mkti Tundu Lissu hana kesi ya kujibu hakupaswi kuonekana kama ujasiri wa Mahakama. Inapaswa kuwa matokeo ya kawaida ya kutenda haki kwa kuzingatia sheria, ushahidi na dhamira njema.
Mahakama inapaswa kushinda jaribu hili, si kwa ajili ya CHADEMA, si kwa ajili ya Serikali, wala si kwa ajili ya Tundu Lissu. Ni kwa ajili ya Tanzania na mustakabali wake.
Haki inapowekwa mbele ya maslahi ya kisiasa, Taifa hushinda na Mahakama inayoaminika ni nuru ya Taifa. Na nuru hiyo haipaswi kuongozwa na hofu, shinikizo au maslahi ya upande wowote, bali na sheria, ushahidi na dhamira ya haki.
Kwa sababu mwisho wa yote, Mahakama inapolinda haki, hailindi mtu mmoja bali inalilinda Taifa.
Nchi hii inaendeshwa kama duka la mtu binafsi.
Wanaamua nani afe nani aishi, wakati gani ufe wakati gani uishi.
Kuna vipeperushi vinamilikiwa na chawa wa serikali hii.
Vinaitwa magazeti, vinatukana watu, vinatuhumu watu kwa uongo na uzushi. Kama ilivyokua wakati wa Magufuli Msiba alitumika na sasa na wao wanatumika.
Lakini wanalindwa, wanapewa fedha na nguvu kufanya uovu huo.
Chombo chochote cha habari ambacho kinaweza kusema na kuandika ukweli kiko mashakani kwa mfumo huu wa kidkteta.
Usalama kwa chombo cha habari au mtu au online tv ni kuimba na kuabudu mama!!!
Kama hautafanya hivyo @gersonmsigwa anapewa amri ya kukufuta au kukufungia kwa furaha yake na jinsi anavyoona inafaa yeye.
Kwenye haya mazingira Msigwa anakua.
1. Malalamikaji
2.Mpelelezi
3. Hakimu/Jaji
Je chombo cha habari kitapata wapi haki?
Kama serikali inalalamikia chombo cha habari kwanini wasifungue kesi mahakamni ili mahakama ndio iamue?
Katiba mpya ni sasa.
Watanzania tusikubali ujinga huu.
Uko wapi Uhuru wa habari?
‼️TUWEKE KUMBUKUMBU SAWA‼️
Huyu kwenye picha anaitwa Mohammed Mirambo ndo alikuwa OCCID wa TEMEKE.
Yeye ndo alimpigia simu Deusdedith Soka na kumwambia aende kituo cha Polisi Chang’ombe kuna pikipiki ya wizi imekamatwa ambayo wanadhani ni Mali ya Soka so aende kuitambua (Pikipiki ya Soka ilikuwa imeibiwa so alikuwa amefungua jalada Chang’ombe Polisi)
Soka aliogopa kwenda Peke yake ikabidi amuombe Katibu wetu wa Chadema Wilaya ya Temeke Jacob Mlay na Frank Mbise ambae ni dereva wake ili wamsindikize.
Soka na wenzake walifika kituo cha Polisi Chang’ombe ila tangu siku hiyo hadi leo ni miaka miwili hawajawai kuonekana popote.
Huyu Mohamed Mirambo aliyefanikisha zoezi la kumteka na kumpoteza Soka na wenzake, alipandishwa CHEO kutoka kuwa OCCID sasa hivi ni RCO wa KINONDONI.
Leo #MariaSpaces tunajadili: Je tugawane mbao, Tanganyika kama Zanzibar mamlaka kamili?
Msemo wa “tugawane mbao” imetumika sana na Wazanzibari hasa wa upinzani wanaodai mamlaka kamili ya Zanzibar. Watanganyika tunasemaje? Tugawane mbao na sisi tupate mamlaka kamili?
Leo saa 2 uck
BADO TSH. MILIONI 41.2 PEKEE TUFIKISHE LENGO LA MILIONI 334.
Bado Milioni 7.2 kufika Milioni 300 .
CHANGIA BARAZA KUU LA UMMA
M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ
NMB
Bank Namba: 22606600140
Jina: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Juzi baada ya kumpost Bibi yake @DEUSDEDITHSOKA , watu wengi mliomba tufanye jambo kwa ajili ya Bibi yake Soka.
Sasa, jana Mwenyekiti wa Bavicha Kanda ya Pwani @JohnNgutiCDM pamoja Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Kilimanjaro @AchibodM walienda Kijijini kumtembelea Bibi yake Soka baada ya kuzungumza nae, kuna vitu vya muhimu ambavyo Bibi anahitaji ikiwemo ni Bima afya.
Hivyo tunaomba kila mmoja aliyeguswa na jambo hili atume mchango wake kwenda kwenye-;
Mpesa : 0740498941
Jina: Theresia Soka.
NB. Tunakusudia kukusanya milioni tano.
REPOST 200
Jiunge leo na sauti za mamilioni ya Watanzania wanaotaka historia mpya.
Wakati wa kuondoa mifumo kandamizi ni sasa hivi na sio kesho tena.
Chukua hatua, paza sauti yako kila mahali ili mchakato uanze. #KatibaMpya
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uenezi wa chama Mh.@BrendaRupia na Mkuu wa idara ya habari @IamLyenda wamekuandalia LIVE STREAMING ambapo watafanya mahojiano na viongozi, wanachama na wadau muhimu wa CHADEMA
Subscribe YouTube Channel ya CHADEMA ili usipitwe https://t.co/oLumCl5hSv
MWENYEKITI KWEMA? Tunaomba utupazie SAUTI sisi watu wa MWANZA(wa hali ya chini) maana CHADEMA ndo imebaki kua sauti yetu, MWENYEKITI huku mwanza ni mwezi na nusu sasa MACHINGA wananyanyaswa sana, hata ukiwa unatembeza hata kijiko unakamatwa unapelekwa jiji unapigwa UNAPIGWA unaumizwa ad unashindwa kutembea, af unawekwa ndan(wana kalokapu) pale jiji af unaambiwa ili utoke hpo unatakiwa ulipe faini ya laki3 kama huna ikifika jioni unapelekwa CENTRO asubuhi unatolewa centro unarudishwa jiji ukikosa iyo hela kazi inakua iyo iyo jiji to centro hawataki kukupeleka mahakamani, af huku mtaani mgambo wanaingia asubuhi wanatoka usiku saa tatu ad saa nne, inamaana hawataki upate hata mia, TUNAKUFA NJAA MWENYEKITI, tunaomba utupazie SAUTI!!!
Banana republic.