Sam Mugumya huyo picha ni mwanaharakati na mwanasiasa wa Uganda, alikuwa msaidizi wa karibu wa Dkt. Kizza Besigye. Aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa Youth League ya FDC na alikuwa miongoni mwa wahusika wa harakati za Walk to Work
Alizaliwa mwaka 1979 Rukungiri, Uganda na alisoma Political Science katika Chuo cha Makerere akahitimu mwaka 2006
Mwaka 2014 alikamatwa nchini DRC na kuwekwa kwenye gereza la kijeshi la Ndolo kwa takribani miaka 8 kabla ya kuachiwa Oktoba 21, 2022
Mwaka 2025, Mugumya alitoweka tena Mbarara kwa kutekwa na watu wasiojulikana. Mamlaka za Uganda zilikanusha kumshikilia, huku Mahakama ikiagiza Serikali kumleta au kueleza alipo na kama anakosa ashitakiwe na awajibishwe kwa mjibu wa sheria
Agosti 2026, picha na video zilisambaa mitandaoni zikimuonyesha akiwa hai lakini katika hali ya kudhoofika sana na amepitia mateso makubwa hawezi hata kusimama. Leo pia zimevuja video zikumuonyesha alivyoteswa na kukonda vibaya mno hawezi hata kutembea
Wakati huo huo, aliyekuwa boss wake Dkt. Kizza Besigye ambae ni mpinzani mkuuu wa Museveni yuko gerezani kwa siku 683 tangu kukamatwa kwake Nairobi tarehe 16 Novemba 2024, akikabiliwa na mashtaka ya uhaini
#BREAKING: AFISA WA UJASUSI WA JESHI LA UGANDA ATHIBITISHA MUGUMYA KUTESWA HADI KUWA MLEMAVU
Afisa wa ujasusi wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda (UPDF) ametangaza kujitenga na jeshi na kuthibitisha kuwa mwanaharakati wa upinzani Sam Mugumya aliteswa hadi kuwa mlemavu akiwa katika kizuizi cha siri cha kijeshi.
Katika taarifa ya video ya dakika 30 iliyotolewa Septemba 30, 2026, Luteni Herbert Mabonga Matanda, aliyewahi kuhudumu katika Makao Makuu ya Ujasusi wa Kijeshi Mbuya, alisema dhamira yake haiwezi tena kustahimili “kukamatwa kiholela, kupotezwa, kutekwa nyara na kuteswa.”
Mabonga alifichua kuwa Mugumya, 47, aliyewahi kuwa msaidizi wa Dr. Kizza Besigye, ni “mtu mlemavu… aliteswa hadi kuwa mlemavu” katika nyumba ya siri chini ya ulinzi wa Special Forces Command (SFC) huko Entebbe.
Ushuhuda wake unathibitisha video iliyosambazwa na rais wa NUP Robert Kyagulanyi mnamo Julai 31, 2026, ikimuonyesha Mugumya akiwa dhaifu, amekonda na akihangaika kusimama kwa msaada wa kifaa cha kutembea, baada ya zaidi ya mwaka mmoja kizuizini bila mashtaka.
Kuna zile #Chenja za jeshini nilikuwa nikizisikia na nikiwaona wanaziimba napata vibe sana na hamasa mno!!
Aaf nawakubali sana wajeda!!
But since last year oct 29, kuna mzuka umekata kabisa, hata nikisikia chenja kali vipi siipati ile hamasa!!
Kuna namna wanetu wamejipunguzia trust na love kubwa sana kutoka kwa raia!!
One of the great speeches delivered by an African president.
I think kama AU ingekuwa coordinated, kila Rais anayezungumza kwenye jukwaa hili angepaswa kuifanya hoja hii kuwa sehemu ya agenda ya hotuba yake. A powerful message becomes even more powerful when an entire continent speaks with one voice.
Hii video imemeba ujumbe mkubwa.
1. Matumizi ya magari yenye namba bandia (Huku usajili halisi wa gari ukiwa ni STM 5806, wakati wa tukio gari lilikuwa na namba za kiraia za T 881 ENZ)
2. Matumizi ya Land Cruiser mkonga, zenye tinted
3. Dereva wa Land Cruiser bila kujitambulisha anageuka kuwa arresting officer kwenye kesi inayomuhusu, akitumia bastola kutaka kuondoka na dereva wa basi kusikojulikana.
4. Muitikio wa wananchi waliokuwa karibu na tukio
The above three scenarios tally exactly with the domains of many reported incidents of forced disappearance.
Inawezekana dereva wa Land Cruiser hii akawa very innocent asiyehusika na matukio ya utekaji na upoteaji wa watu.
Lakini gari anayomiliki na mazoea ya kiholela ya vyombo vya dola kutumia namba za bandia wanapoenda kukamata watu, kukampa kujiamini dereva huyu kufanya alichofanya akiamini wananchi wameshaanza kuchukulia kawaida aina hii ya ukamataji usiofata sheria yoyote
Matukio mengi ya aina hii yameishia kuwaacha wananchi wakilalamika kutowaona tena ndugu zao waliokamatwa na watu wasiojulikana kama ilivyokuwa kwa dereva huyu.
Wananchi hawa wakifikisha taarifa polisi hakuna matokeo yoyote chanya wanayoyapata bali zaidi ya taarifa zao kupotezewa under the pretext ya “Uchunguzi unaendelea”
“Mtu sio nyau”, wananchi sasa wanaona imetosha. Sasa hawaogopi bastola, hawaogopi tena Land Cruisers, hawaogopi tena tyre covers za jeshi, na hawaogopi wasiojulikana.
Wananchi kwa umoja wameamua kujihami na kumuhami dereva aliye hatarini kupotezwa. Wanatoka kumkabili mtekaji mtarajiwa.
Nini kitajili endapo wananchi kote nchini wakianza kuwa disobedient kwa wakamataji na labda wakavuka hadi mpaka wa kuwapiga wakamataji wao wasiofata sheria na hata kuchoma magari yao?
Jambo hili japo siombei litokee, linaweza kuzaa a very critical second wave of massacres hasa tukizingatia wakamataji hawa wanamiliki vyombo vya moto na kuna nyakati waliwahi kuvitumia kuua mamia na hakuna aliyewajibishwa wala kuwajibika bado.
Machafuko yoyote yatakayotokea kutokana na tabia hizi, hayatakuwa yamesababishwa na uchochezi wa kisiasa, bali yatakuwa yametungwa, yakazaliwa na kulelewa na watu tuliowapa dhamana ya usalama wetu.
It’s high time, wakuu wa vyombo vya dola watoke hadharani ya ukamataji holela usiofata sheria. Waziri Simbachawene alishawahi kutoka hadharani na kukemea hili.
Kuna ugumu gani mtu akikamatwa kwa RB kwa mujibu wa PGO?
Kuna ugumu gani mkamataji akijitambulisha, akamtajia kosa mkamatwaji na kueleza anapotaka kumpeleka?
Zaidi, kuna sifa gani unapomkamata mtu kama kuku na kumuweka mafichoni bila ndugu zake au mawakili wake kujulishwa?
Ukamataji wa aina hii una manufaa kwa Jamuhuri au una interest binafsi kwa wakamataji. Nauliza hivi nikiamini Jamuhuri haiathiriki na chochote endapo mtu atakamatwa kwa kufata sheria. Ni kwa sababu nia ya Jamuhuri ni kumfikisha mtu huyu mahakamani hivyo hakuna maana yoyote ya kumficha mtu unayetarajia kumfikisha mahakamani.
Ukamataji wa kujificha ni must be in line with “nia ovu”
End of morning rant dear hoofmen
DAR: Mkurugenzi mstaafu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (#LHRC) Dkt. Hellen Kijo-Bisimba, amesema hayo Septemba 15, 2026, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani.
Mjadala unaendelea https://t.co/LmBsht2yzV
#JamiiForums#Demokrasia #InternationalDayOfDemocracy
HII NI TANZANIA.
Imagine mtu anatoa dukuduku lake kwamba Kijijini kwake hakuna maji, Anakamatwa na Polisi, Je huyu anaenda kuandikiwa Kosa gani?
Achana na huyu muerevu mmoja, Chakushangaza Wanakijiji ambao ni wenzake wenye changamoto moja, Mwenzao anakamatwa yametulia kama mazezeta.
Hii nchi safari bado ndefu sana
Wanangu hii movement ni yetu sote,na kila mtu ana namna yake yakuipambania, kikubwa ukiambiwa hii njia sio nzuri sikiliza usikaze kichwa kwasababu utaumia kweli, upande wa pili wamejipanga kisawasawa kutuumiza so tujitahidi kuwakwepa, 2030 we need everyone fit.
Raia aliyempiga Askari ni Daktari bingwa wa magonjwa ya ndani, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Kampasi ya Mloganzila.
Wanaomfahamu Dr. Conrad wanajua ni mtu mpole sana. Ni jambo la kushitua kumuona kwenye matukio haya. Haijulikani yule askari alimfaya nini. Kwa bahati mbaya matukio yanayowahusisha polisi na raia, huwa tunasikia upande mmoja tu wa polisi wenyewe, raia wasio polisi hatuwasikilizi upande wao wanasema nini.
Kwa mfano kwenye tukio hili, tunaambiwa raia alimpiga polisi wakati huyo polisi akitekeleza majukumu yake, lakini huyo raia hapewi nafasi ya kusikilizwa ilikuwaje hadi akafanya hivyo.
Mbaya zaidi, kwenye tukio la namna hii polisi kwa akili zao wanaweza kuwa wamempiga sana huyo raia. Kuna taarifa (zisizo rasmi) kwamba huyu Daktari yupo ICU.
Rai yangu kwa polisi, kupitia kwa Afande Murilo, polisi wamfikishe mbele ya vyombo vya sheria huyu Daktari, akiwa salama salmini. Hukumu yake kwa kosa alilofanya inatakiwa itolewe na vyombo rasmi. Sio kazi ya polisi kutoa hukumu. Huko kwenye vyombo vya sheria tutajua ni kitu gani kilitokea mpaka kupelekea ugomvi huo.
Nitumie nafasi hii pia kuwashauri viongozi wa Jumuiya ya Madaktari Medical Association of Tanzania kutoa wito wa kutaka Daktari Conrad awe salama huko wanapomshikilia.
Nafuatilia kujua kama ni kweli amepigwa sana hadi kulazwa ICU.
Nawasilisha!
Dr. Chris Cyrilo.
Leo, Godlisten Malisa alikuwa akiingia nchini kupitia mpaka wa Namanga. Alishikiliwa na Uhamiaji kwa saa kadhaa, na kisha baadaye akachukuliwa na Polisi. Mpaka sasa, hata Wakili wake, Dickson Matata, hajui alikopelekwa. Akiwa Namanga, Godlisten alinipigia simu mara kadhaa na kunieleza mambo aliyokuwa akikabiliana nayo. Baada ya kuchukuliwa na Polisi, mawasiliano yakakatika.
Hili si jambo la kawaida, wala si jambo la kuchukuliwa kirahisi. Serikali haiwezi kumkamata mtu, ikamchukua mahali pasipojulikana, halafu ikanyamaza kuhusu alipo. Hata kama kuna tuhuma au uchunguzi wowote unaomhusu, sheria inamtaka mtu huyo ashughulikiwe kwa taratibu zinazotambulika na haki zake zilindwe. Godlisten Malisa yuko wapi? Amepelekwa kituo gani cha Polisi? Kwa kosa gani? Na kwa nini wakili wake hajui alipo?
Haki za msingi za mtu haziwezi kusimamishwa kwa sababu tu ameshikwa na vyombo vya dola. Mamlaka si ruhusa ya kutowesha watu. Serikali iwajibike na itoe majibu sasa.