Fr. Dr. Charles Hugo Kitima (BSc, MSc, PhD), Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) alivamia katika makazi ya Maaskofu Katoliki, Msimbazi Centre na akajeruhiwa katika jaribio la kumuua. Waliofanya hivyo hadi leo hawajamatwa. Unatarajia TEC wasitoe TAMKO?
Tamko la TEC limefanya mambo matatu tu.
1. Limelaani MAUAJI ya kikatili yaliyifanywa kwa raia.
2. Limechambua mzizi wa tatizo: USALAMA, DEMOKRASIA, na UBUTU WA MIHIMILI.
3. Limeonesha tiba: UWAJIBIKAJI, UADILIFU, SAUTI YA RAIA, na KATIBA MPYA.
Period.
Mambo 5 Mungu Anatamani Ujue :
1. Kila kitu kina wakati wake.
2. Hakuna kilicho kigumu kwake.
3. Anajua mwanzo na mwisho wako.
4.Fanya unachoweza, acha Yeye atimize.
5.Usiache kumwamini.
🔥✊🏽
“Siwaombi majaji chochote!Mtakachoamua, msiamue kwa huruma. Muamue yote kwa haki na kwa mujibu wa viapo vyenu. Msinihurumie na sihitaji huruma yenu nahitaji muamue kwa haki.”
Tundu Antipas Lissu
11 Septemba 2025
Mahakama Kuu D’Salaam
“Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga anasema kwa busara tu ndiyo maana tuliletwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa sababu kosa lilifanyika huku (Dar es Salaam). Sasa mimi nasema tafsiri ya masuala ya kisheria haipaswi kuwa tafsiri ya busara. Hii sio Mahakama ya busara ni Mahakama ya sheria. Ingekuwa Mahakama ya busara msingekuwepo hapa Mahakamani leo. Pengine huko mtaani wapo watu wengi wangekuwa majaji na ninyi mngekosa kazi hii mliyonayo. Lakini sisemi kwamba mmekosa busara lakini ninachosema ni kwamba ninyi ni majaji kwa sababu ya sheria siyo busara”. – Tundu A.M Lissu
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 5
Anasimama Mhe. Lissu kuanza na suala la jurisdiction kwanza.
Ameleta pingamizi kuwa mahakama hii haina mamlaka kivipi kusikiliza kesi hii.
Mh. Lissu anaanza kwa kusema taarifa hii niliyoitoa nilishaitoa mapema huko nyuma hasahasa mahakama ya Kisutu.
Naomba niibadilishe hiyo hoja kidogo sana.
Hoja yangu isomeke mahakama hii haina mamlaka ya kusikiliza kesi hii kwasababu ya makosa mengi na makubwa yanayoonekana kwenye uso wa rekodi ya mahakama ya ukabidhi (committal Court) yaani ile mahakama ya kisutu.
Makosa hayo yameuharamisha utaratibu wote wa committal Court.
Anasema kingereza chake cha haya niliyoyasema ni hiki. Anatema ung'eng'e kwamba under section 184 of CPA on the face of record the committal proceedings includes irregularities.
Jaji anauliza tunaachana nayo kivipi? Anamjibu kuwa nilichokwambia kwa sasa ndio iwe record yako na nitazungumzia kwa namna nilivyoliweka hili pingamizi kwa sasa. Tuendelee kwa utaratibu huo tafadhali. Wanakubaliana hapa.
Mh. Lissu anaendelea anasema naomba nianze kuweka msingi wa kisheria.
What is the law on committal proceedings? Hii sheria inasemaje na ikoje?
Kif. cha 261cha CPA kinasema pale ambapo shitaka limepelekwa mahakamani dhidi ya mtu yeyote kwa kosa ambalo haliwezi kusikilizwa na mahakama ya chini basi mashauri ya ukabidhi (committal case) itafanyika katika mahakama ya huko chini.
Anasoma hapa hicho kifungu cha sheria kilivyoandikwa.
Kwahiyo committal proceedings ilipaswa kufanyika kwenye hiyo mahakama ya chini.
Kifungu cha 184 of CPA kilipaswa kusomwa pamoja na kifungu cha 261 nilichosema awali.
Ambapo kinasema hakuna kesi ya namna hii itaendelea hapa bila ya mtuhumiwa kuwa committed kwenye mahakama hii ili iweze kusikilizwa.
Sasa sheria inasema utaratibu wa Committal lazima ufuatwe ili tuendeleee vizuri hapa leo.
Mahakama ya rufani ya Tz ineweka msimamo wake kwneye nasuala haya kesi ya Jamhuri vs Dodoli Kapufi na wenzake. Criminal Rev. CAT At Mbeya.
Ninayo nakala moja niko gerezani, ukurasa wa 25 sect. 178 of the CPA creates a bar against a taking of cognizance unless the same has been investigated and the accused have been committed duly committed for trial.
Kwanza lazima iwe properly investigated na pia iwe duly yaani properly ina accordance of the law.
Hayo masharti kwa namna ya kuifanya hiyo kesi ifike hapa jwenye mahakama hii. Je masharti hayo ni yapi? Masharti gani hayo?
Kif. Cha 262(1) cha CPA kinaweka sharti la kwanza la committal processes.
Kinasema kwamba pamoja na mambo mengine sharti la kwanza unapelekewa kwenye mahakama ya eneo ulilokamatiwa.
Mimi nilikamatiwa Mbinga, mkoa wa Ruvuma. Committal proceedings zimefanyikia Kisutu Dar es salaam. KM nyingi kutoka Mbinga. Sheria ilisema nipelekwe nilipokamatiwa.
Sharti la Pili ni la kusomewa shtaka kif. 262(2) cha CPA na hatatakiwa asijibu.
Sharti la tatu, liko kwneye kifungu cha 262(3) of CPA baada ya charges kusomwa mtuhumiwa aambiwe kuwa hatapaswa kujibu na atapelekwa gerezani.
Sharti la nne ni kwamba liko 262(6) of CPA baada ya upelelezi kukamilika ataandaa information (mashtaka) kwa mujibu wa sheria na kuyafungua mahakama kuu.
Sasa waheshimiwa ma jaji sharti muhimu kwa ajili ya hoja yangu ya leo lipo kwneye section 265(1) ya CPA.
Kifungu hicho kinasema kuahirishwa kwa kesi wakati wa committal. Nitakielezea pia.
Part 6 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
Nimesoma vizuri mfululizo wa maandiko ya dada Hilda @HildaNewton21... itoshe kusema tunapigana vita kali sana. Hii si vita ya kawaida
Naomba tusome Waefeso 6:12
KANISA Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, limewaagiza Madekano, Maparoko, Watawa na Waamini wote Walei, kutekeleza agizo lililotolewa na Askofu Mkuu Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa'ichi, kufunga Novena ya kuliombea taifa.
Taarifa ya Jimbo Katoliki Dar es Salaam, iliyosainiwa na Pd. Vincent Mpwaji, imesisitiza kuwa “Mhashamu Askofu Mkuu ameagiza kwamba katika Parokia zote na Asasi zote katika Jimbo Kuu la Dar es Salaam, ifanyike Novena ya siku tisa (9) kuomba Haki na Amani kuanzia tarehe 15 hadi 23 Agosti 2025.”
Amesema, Askofu Mkuu ameelekeza kwamba Novena hiyo iambatane na kuabudu Ekaristi Takatifu, Kusali Rozari Takatifu na kusali sala ya Kuiombea Tanzania kama iliyotolewa na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).
Ameongeza, “Katika siku ya kilele cha Novena, yaani Jumamosi ya 23 Agosti, ambayo ni kuomba Haki na Amani, sote tunaalikwa kufuata ratiba iliyotolewa na Idara ya Kichungaji ya TEC.
“Ratiba hiyo inaelezea namna ya kufanya sala na mfungo huo ambao utaanza siku hiyo tarehe 23 Agosti kwa adhimisho la Ekaristi Takatifu, ikifuatiwa na kuabudu Ekaristi Takatifu ikiambatana na vipindi mbalimbali vya sala, mafundisho, na ukimya, na kuhitimishwa Dominika tarehe 24 Agosti kwa adhimisho la Misa Takatifu kama inavyoelekezwa katika maelekezo yaliyotoka TEC.”
Maelekezo ya Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, yameambatanishwa na kinachoitwa, “barua ya TEC na mwongozo wa sala.”
Anasema, uongozi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, unapendekeza kwa Parokia zote, kwamba Misa hii ya hitimisho la mkesha iwe Misa ya kwanza.
“Sala mbalimbali ambazo zimeelekezwa/ zimependekezwa katika ratiba hii iliyotolewa na TEC, tunaweza pia kuzitumia katika kusali Novena iliyoelekezwa hapo juu,” imeeleza taarifa ya kanisa.
TEC limeagiza kufanyika sala maalum ya kitaifa kwa makanisa yake na mafungo, ili kuliombea taifa haki na amani, kuelekea uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani wa 2025.
Maaskofu walitoa wito huo kupitia barua yao rasmi ya tarehe 20 Juni 2025. Ilisainiwa na mwenyekiti wa idara yake ya Liturujia, Simon Chibuga Masondole, Askofu wa Jimbo Katoliki la Bunda.
Uamuzi wa maaskofu wa TEC ulifikiwa mara baada ya kumalizika mkutano wao mkuu wa 109 uliofanyika Kurasini, jijini Dar es Salaam, kuanzia tarehe 16-19 Juni 2025.
Mkutano wa TEC ulihitimishwa kwa kauli mbiu ya “Taifa linapoendelea na safari katika Tumaini lisiloisha katika mwaka huu Mtakatifu wa Jubilei Kuu 2025.”