UKWELI na UWAJIBIKAJI pekee ndiyo utawapa uhalali.
INTERAHAMWE waliokaa kimya wakati wananchi wanapigwa risasi na kuuwawa, sasa wamepewa kandarasi ya kuifanyia kampeni kitu kinachoitwa ‘tume ya kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani’.
MAHARAMIA waliokaa kimya au kushindwa kulaani kabisa matukio hayo wanayoita ‘uvunjifu wa amani’ sasa wanatumika katika kuhalalisha au kupigia debe chombo kinachopaswa kuchunguza matukio hayo.
WASHENZI hawaogopi kutapakaza damu mbichi katika mikono yao. Hawaoni tatizo kufanya biashara haramu katika dimbwi la damu. Hawa ni viumbe hatari ambao hawana roho ya huruma na utu ndani yao.
Katika sayansi ya siasa na sosholojia (sociology), hali hii huitwa utekaji wa wasomi (elite capture) vikundi vyenye maslahi vinatumia mifumo ya kisheria kuhalalisha vitendo vyao vilivyopita badala ya kuwajibika.
Tume yoyote inayoundwa kuchunguza uvunjifu wa amani inahitaji kitu kimoja kikubwa: Imani ya Umma. Hawa wahuni ambao mnawatumia kufanya kampeni tume yenu, hawawezi kuwasaidia kuaminika na umma.
Ikiwa wananchi wanaona watu au makundi yenye rekodi zenye utata katika jamii wanahusishwa na kuikuza au kuilinda tume hiyo, basi mashaka yanaongezeka hata kabla uchunguzi haujaanza. Wananchi siyo wajinga.
Kitaalamu, tume huru ya uchunguzi (Independent Commission of Inquiry) haipaswi kupigiwa kampeni. Badala yake, tume inapaswa kujidhihirisha kupitia: (i) Muundo wake (ii) Mamlaka yake (iii) Uwazi
Ikiwa nguvu nyingi inatumika kuishawishi jamii kuikubali tume kupitia makundi yenye sifa tata, hiyo inajenga picha ya jitihada za kusafisha taswira (PR exercise) badala ya nia ya dhati kupata ukweli na uwajibikaji.
Tume huru ya uchunguzi inapigiwa kampeni?