⛓️💥 The situation between Vinícius Jr and Real Madrid has taken a major turn. According to reliable reports, the Brazilian winger is no longer interested in renewing his contract, bringing all extension negotiations to a complete halt.
Arsenal are keeping a very close eye on this developing situation and have internally decided to push with everything they have to secure the blockbuster signing of the Brazilian superstar. 🌟
Kwa wale mnaopenda kusoma na kusali kwa kutumia vifungu vya Biblia:
Anza na Isaya 41:10 kuomba nguvu, ujasiri na msaada wa Mungu wakati wa changamoto. Endelea na Yeremia 29:11 kuomba tumaini, mwelekeo na mipango mema ya Mungu katika maisha yako. Kisha soma Wafilipi 4:6–7 kuomba amani ya Mungu na kuondoa hofu na mawazo mengi. Malizia na Methali 3:5–6 kumwomba Mungu akuongoze katika kila hatua na maamuzi yako. 🙏
Siku moja, matokeo yako yataeleza kile ambacho maneno yako hayakuweza kueleza.
1. Linda vision yako.
2. Kubali gharama yake.
3. Usikate tamaa.
4. Mwisho wa safari ndiyo ushahidi wa thamani ya uvumilivu wako.
@mangekimambi@Liberatus80 Wewe dada nilijuaga km wale wadangaji tu na wapenda mambo ya umbeo kumbe ni mtu mwenye AKILI sana na unawaza haraka sana hongera sana Hapo umeongea point sana
Wakati Dharau Inapokuwa Ndiyo Menyu, Ondoka Mezani
Na Rev Peter Simon Msigwa
Kuna wakati katika maisha unapaswa kujifunza moja ya masomo magumu zaidi, lakini yenye nguvu ya kukuweka huru: ondoka mezani pale ambapo dharau imekuwa ndiyo menyu.
Tangu utotoni, wengi wetu tulifundishwa kwamba kuvumilia kila kitu ni ishara ya nguvu. Lakini sikiliza vizuri: nguvu si kukaa kwa muda mrefu mahali panapokuvunja. Nguvu ni kuwa na ujasiri wa kusimama, kusukuma kiti chako nyuma na kuondoka.
Dharau haiji kila wakati kwa matusi makubwa au kelele. Mara nyingi huja kimya kimya, ikijificha kwenye tabia ndogo ndogo zinazokufanya uanze kujiuliza kama kweli unathaminiwa.
Dharau ni pale mtu anapopuuzia hisia zako kila mara. Ni pale anapodharau mafanikio yako, anapofanya mzaha juu ya maumivu yako, au anapokutumia kihisia, kifedha au kiakili. Ni pale anakukumbuka tu anapokuwa na jambo analokuhitaji.
Hatari ya kuendelea kuvumilia dharau ni kwamba, ukikaa kwa muda mrefu, unaanza kuiona kama jambo la kawaida. Polepole unaanza kujiona huna thamani. Unaanza kujitilia shaka. Mwishowe unaweza kuamini kwamba hiyo ndiyo aina ya upendo unaostahili, au ndiyo namna bora zaidi ya kutendewa.
Hiyo ndiyo hatari ya kukaa muda mrefu kwenye meza ambayo inakudharau.
Mara tu unapoitambua dharau, unawajibika kuamua utabaki hapo kwa muda gani.
Kumbuka hili: Unawafundisha watu jinsi ya kukutendea kupitia yale unayokubali kuyavumilia.
Ikiwa menyu ni dharau… ikiwa kila unachopewa ni kukosolewa, kudhalilishwa, kudhibitiwa au kunyanyaswa… ikiwa kila mazungumzo yanakuacha ukiwa umevunjika moyo kuliko ulivyoingia… basi umefika wakati wa kusimama, kusukuma kiti chako nyuma na kuondoka.
Kuondoka si kiburi.
Kuondoka si hasira.
Kuondoka si kulipiza kisasi.
Kuondoka ni kujiheshimu.
Huenda si kila mtu ataelewa mipaka yako, wala si kila mtu ataiheshimu. Lakini unapochagua kuondoka mahali penye dharau, unakuwa unasema:
“Sina njaa ya kupendwa kwa gharama ya heshima yangu. Sihitaji kuomba kuthaminiwa. Ninajua thamani yangu. Meza hii ni ndogo mno kwa kusudi na ukuu ambao Mungu ameweka ndani yangu.”
Na hili ndilo tumaini kubwa:
Mungu kamwe hakuondoi mahali pabaya bila kukuandalia mahali pazuri zaidi.
Atakuongoza kwenye meza ambayo utathaminiwa, ambapo sauti yako itasikilizwa, ambapo uwepo wako utaheshimiwa badala ya kuvumiliwa.
Meza ambayo menyu yake ni amani, upendo, heshima na uwazi.
Hapo ndipo mahali pako.
Leo, jiulize:
Umeketi kwenye meza ya nani?
Wanakulisha nini?
Je, unalishwa ili ukue, au unalishwa sumu inayokumaliza polepole?
Ikiwa menyu ni dharau, simama. Sukuma kiti chako nyuma. Ondoka kwa heshima na kwa utulivu.
Na kamwe usiombe msamaha kwa kuchagua kujiheshimu.
Maamuzi Yatakayo Badilisha Maisha Yako:
1. Kuamka mapema
2. Kujifunza kila siku
3. Kuheshimu muda
4. Kufuatilia mambo yako
5. Kutoogopa kufeli na kuanza upya
6. Kuchagua marafiki mnaofanana maono
7. Kuweka akiba na kuwekeza kwa nidhamu
8. Kulinda afya yako ya akili na mwili
Amka saa nane za usiku kwa siku saba mfululizo, kisha usali sala hii kwa imani. Mwombe Mungu avunje kila kikwazo, afungue milango iliyofungwa, aondoe kila kinachozuia maendeleo yako, na akupe kibali mbele zake na mbele za watu katika kila jambo unalolifanya:
Ee Mungu Mwenyezi, ninakuja mbele zako kwa jina la Yesu Kristo. Naomba uvunje kila kifungo, uondoe kila kikwazo, na ufungue kila mlango uliofungwa katika maisha yangu. Niongoze katika njia zako, unipe hekima, nguvu, na neema ya kushinda kila changamoto. Nibariki kazi za mikono yangu, unipe kibali katika kazi, biashara, masomo na mahali popote nitakapokwenda. Uniongoze kwenye mapenzi yako, na mapenzi yako yatimizwe katika maisha yangu. Naamini hakuna lisilowezekana kwako. Amina.
Isaya 45:2
"Nami nitakutangulia, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja milango ya shaba, na kuzikata-kata mapingo ya chuma."
20 Stoic Lessons in 60 Seconds
That Will Make You Stronger
1. Anger is punishment you give yourself.
2. Discipline is the highest form of self-love.
3. Ego is the enemy — stay humble.
4. Do the right thing, not the easy thing.
5. You become unstoppable when you stop seeking approval.
6. You don’t need to respond to everything.
7. The world owes you nothing — earn your life.
8. Most fears are illusions — face them.
9. Let go of what you can’t change — or it will own you.
10. The strongest person is the one in control of themselves.
11. Emotion kills logic — breathe, don’t react.
12. You suffer twice when you worry about tomorrow.
13. Not everything deserves a reaction — silence wins battles.
14. If it doesn’t matter in five years, let it go today.
15. Become the person your past self prayed for.
16. Focus on effort, not outcome — outcome belongs to fate.
17. A wise mind listens twice before speaking once.
18. Suffering becomes strength when you accept it.
19. Routine builds warriors — chaos builds victims.
20. Your time is your life — guard both.
Mwanaume ana njia chache za kujitoa kwenye msongo wa mawazo.
- Kutafuta pesa.
- Kufanya mazoezi ya mwili.
- Kumwamini Mungu.
- Kufuatilia kusudi lake.
Hii ni cheat code nimekupa kwa sababu nataka ufurahie maisha yako.
Hakuna miaka mingi mbele kutoka leo. Pombe inatengeneza janga ambalo wengi hawalioni. Ikiwa mwenendo wa sasa utaendelea, itaua watu wengi zaidi, kuvunja familia nyingi zaidi, na kuchochea kuporomoka kwa maadili ya jamii kwa kiwango ambacho kitakuwa tishio kubwa kwa mustakabali wa taifa letu. Inatisha sana.
@MariaSTsehai@AbroadTanzania Hon.Lema alilisema hili kwamba Msigwa kilicho mkimbiza CDM ni MWAMBA so asamehewe tu kwani MWAMBA baada ya kupiwa kata funua kazila Chama na hata move ya akina Jasusi pori ma kesi ya akina Said Issa na wenzie ni yeye na Salum Mwalimu ndo wasukaji!
Tangu udogo wangu nimekua shabiki mkubwa wa Arsenal. Ilipofika mwaka 2015 vipigo vilizidi nikamua ili nisipate "pressure" niliapa kutokuangalia mechi yoyote ya Arsenal mpaka siku itakapochukua ubingwa tena.
Hatimaye leo ile siku imefika. Hakika hii ilikuwa ni "the long wait"
We are the champion 🏆