@kasesco_tz Kama simu yako ni original copy hii nyumba na paste bila kubadilika chochote..๐
โฑโฅโโโโโโโฃ
โโฉโ๐โคโโคโคโ
โโโโโโฉโ
UNATAKA KUANZISHA BIASHARA YA KUUZA DAWA ZA BINADAMU NA HUJUI UANZIE WAPI?
TARATIBU ZA KISHERIA ZIKOJE?
JIFUNZE KISHERIA NAMNA YA KUFUNGUA BIASHARA YA PHARMACY NA UKA RUN BILA MASHAKA.
_MAOMBI
_ GHARAMA
_FINES/KIFUNGO๐
Umepata Ajali Au Umefiwa? Jua Haki Zako Katika Bima na Usipate Kudanganywa na kutojua sheria sio utetezi.
ukiwa umekata Bima na ukapata ajali, kabla ya kwenda kwenye kampuni husika ya Bima kuna vitu lazima uende navyo ili upate stahiki yako bila kufanya hivyo mkuu utalaumu watu bure.
shuka na uzi kutojua sheri sio utetezi bali utaona msumbufu tu.
Anaandika Baba Askofu Rev.Dr.Benson Bagonza (PhD), Mkuu wa KKKT Dayosisi ya Karagwe.
_________
1. KKKT ina Mkuu wa Kanisa mmoja tu. Madereva wawili hawawezi kuendesha gari moja kwa wakati mmoja.
2. Hakuna cheo kinaitwa โMkuu wa Kanisa Mstaafuโ bali kuna "aliyewahi kuwa Mkuu wa Kanisa." Malasusa amewahi kuwa Mkuu wa Kanisa na sasa amechaguliwa tena. Kama angekuwa "mstaafu" asingechaguliwa tena. Ukistaafu unapumzika.
3. Ukipenda, usipende kwa niaba. Ukichukia, usichukie kwa niaba. Kila ulimi una uwezo wa kuonja wenyewe.
4. KKKT ni shirikisho la Dayosisi 28 za Kilutheri. Ukitaka kusema kwa niaba ya shirikisho, unashawishi wenzio sio kuwaburuza.
5. Naweza kumpenda Rais Samia na kukikosoa chama chake. Naweza kukipenda chama chake nikamkosoa yeye. Lakini yote hayo nitayasemea Karagwe sio ugenini. Wanyambo haturuhusu mgeni kupiga mluzi katika nyumba ya mwenyeji.
6. Kanisa lina wanachama wa vyama vyote na pia lina waumini wasio na vyama. Chadema msitutolee macho na CCM msishangilie. Shoka lipo shinani, mti usiozaa matunda utakatwa.
7. Rais Samia ana uwezo wa kujiharibia mwenyewe, tusimharibie. Hajaomba msaada. Lipo kundi linalodhani linamsaidia kumbe linamharibia. Na Lipo kundi linalodhani linamharibia kumbe linamjenga.
8. Kuna watu wanatumia dini kueneza siasa. Na kuna watu wanatumia siasa kueneza dini. Mimi si mmoja wa hao wawili. Mimi natumia ujinga kueneza dini na siasa. Wajinga wenzangu ndio wananisikiliza na kunifuata. Wewe mjuaji kaa pembeni tuendelee na safari.
9. Nikisema jambo mkashingilia mnanipa kiburi cha kusema bila kufikiri. Nidhamu ya washangiliaji huja kwa kutafakari, si mihemko. Anayesema kweli hahitaji kukumbuka alisema nini jana, bali muongo anapaswa kuwa na kumbukumbu nzuri.
10. Mungu analipenda Taifa hili kuliko mtu yeyote au chama chochote. Tusiombe Mungu atuonyeshe anavyolipenda taifa letu. Ina gharama nzito.
NB: Hata anayerudi nyuma ana mbele anakoelekea. Ukisifiwa kuwa na mbio, jihadhari usipitilize nyumbani kwenu. KKKT ina Mkuu wa Kanisa mmoja tu.!