#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 229
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Shahidi wa Jamhuri ACP Amin Mahamba.
Mhe. Lissu : Shahidi apatiwe PGO namba 1 aya ya 25 Crimes are Actions defined by law yanayoitwa makosa ni matendo yaliyofafanuliwa na Sheria ya Upelelezi wa Polisi inabidi ufuate masharti ya sheria strictly.
Swali langu kifungu cha 38 (2)d kinataja tendo la kuvuruga uchaguzi ni kosa?
ACP Amin Mahamba : Hapana.
Shahidi kakubaliana na Mhe. Lissu kimtindo kuwa haijataja.
Mhe. Lissu: PGO namba 1 para 3 inasema kila Askari Polisi anawajibu wa kuheshimu Uhuru wa mwananchi kama ulivowekwa kwenye Katiba na Sheria na kwenda kinyume na haya haikubaliki, tafsiri iko sahihi au sio sahi?
ACP Amin Mahamba : Inategemea
Mhe. Lissu anarudia tena swali hilo hilo.
ACP Amin Mahamba anajibu hapa anajiumauma sana ni kweli tunatakiwa kuheshimu haki za raia imetoka kwa mbinde sana mdomoni mwake.
Mhe. Liss : Ibara ya 15 (1 kila mtu ana haki ya kuwa huru na kuishi kama mtu huru kweli au si kweli?
ACP Amin Mahamba : Ni kweli.
Mhe. Lissu; Kuna mahali umezingatia uhuru wangu kwenye maelezo yako polisi?
ACP Amin Mahamba : Hayapo ila aina ya kosa uliloshtakiwa nalo halitakiwi uwe huru, ninachotambua ulikuwa na haki.
Mhe. Lissu : Hao wenzio nilimalizana nao niko na wewe ulitambua haki yangu ya uhuru kwenye maelezo yako?
ACP Amin Mahamba : sikuweka
Mhe: Lissu : Ulizingatia Haki yangu ya uhuru wa kutoa maoni na fikra zangu kwenye maelezo yako uliyotoa polisi?
ACP Amin Mahamba : Ilizingatiwa
Mhe. Lissu anasoma hapa ibara inayoongelea haki ya mtu kutoa mawazo yake hadharan na kujumuika na watu...
Anasema Mwenyekiti wa chama alitoa mawazo yake alipokutana na watu wake hadharani ulizingatia haya?
ACP Amin Mahamba : Ulifanya makosa, uliitisha serikali.
Mhe. Lissu: Hayo maelezo ya kutisha serikali yako wapi? inaweza ikawa una shida ya akili
Shahidi : Kimyaaaa
Mhe. Lissu ; Ulizingatia kuwa nina haki ya kufaidi haki za kikatiba kutokana na ibara ya 29 na ukaweka kwenye maelezo yako?
ACP Amin Mahamba : Hapana sikuweka
Mhe. Lissu: Kama uliangalia video nilishambulia sana Tume ya Uchaguzi kuwa inapendelea CCM miaka yote na watumishi wanaohusika na Serikali, wanapendelea ccm pamoja na wizi wa kura..
ACP Amin Mahamba : Ndio ulisema
Mhe. Lissu : Nilisema kuwa Samia aliamuru wagombea wa upinzani waenguliwe kwenye uchaguzi wa Serikali za mtaa?
ACP Amin Mahamba : Ni kweli, ulisema.
Part 230 itaendelea kwenye post inayofuata.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, amekubali ombi la Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Salum Hapi, la kutaka vyama vya siasa vikaguliwe, huku akitaka ukaguzi huo upanuliwe hadi kwenye mali binafsi na mwenendo wa kifedha wa viongozi wa vyama na Serikali.
Heche amesema CHADEMA haina hofu ya kufanyiwa ukaguzi kwa kuwa fedha za chama hupitia kwenye akaunti rasmi, ikiwemo benki na namba za simu, na kwamba hesabu hizo hukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Amesema chama hicho kimekuwa kikipewa hati safi katika ukaguzi wake.
Akizungumza katika kipindi cha Dakika 45 cha ITV jana Jumatatu, Agosti 10, 2026, Heche amesema amefurahishwa na kauli ya Hapi, lakini amemtaka CAG kutoweka nguvu zake kwenye vyama vya siasa pekee, bali pia kukagua matumizi na vyanzo vya fedha vya CCM, hususan michango iliyokusanywa wakati wa kampeni.
“Huyu Bwana wa CCM mwambieni nimekubali CAG atukague na asiishie tu kwenye Vyama vya siasa, akague mpaka mtindo wa Maisha ya Viongozi na utajiri walionao. Tunataka tukague mpaka fedha wanazomiliki, wanalipa kodi?” alisema Heche.
Heche pia amedai kuwa kuna baadhi ya Mawaziri ambao utajiri wao umeongezeka kwa kiwango kikubwa baada ya kuingia madarakani, akitoa mfano wa Waziri mmoja ambaye alisema aliingia naye Bungeni akiwa na gari moja, lakini kwa sasa anamiliki majengo 20 ya ghorofa jijini Dar es Salaam. Aidha, alidai kuwa baadhi ya viongozi wana nyumba nje ya nchi, ikiwemo Dubai na Ujerumani, pamoja na magari mengi.
Kwa msingi huo, Heche ameitaka taasisi za ukaguzi na mamlaka husika kufanya uchunguzi mpana wa mali za viongozi, vyanzo vya utajiri wao na ulipaji wa kodi, akisisitiza kuwa ukaguzi haupaswi kuishia kwenye vyama vya siasa na Serikali pekee, bali pia kuangalia iwapo mali zinazomilikiwa na viongozi zinaendana na mapato yao halali.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 228
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Shahidi wa Jamhuri ACP Amin Mahamba.
Mhe. Lissu : Hayo maneno ya kuvuruga Uchaguzi yapo kwenye hiko kifungu?
ACP Amin Mahamba : Yapo.
Mhe. Lissu : Tusomee
ACP Amin Mahamba anasoma hapa hiko kifungu
Mhe. Lissu:m : Ulichosoma kimeongelea uchaguzi?
ACP Amin Mahamba : Ndio yapo
Mhe. Lissu : Una akili timamu?
ACP Amin Mahamba : Ndiyo.
Mhe. Lissu anasikitika
Anamuuliza tena ni kweli iko kifungu kinaongelea mtu anaetishia Serikali, Bunge au Mahakama? ni kweli au si kweli?
ACP Amin Mahamba : Ni kweli.
Mhe. Lissu : Na akatishia Bunge au Mahakama na kumalizia kosa lake kwa kuchapisha ndio amefanya uhaini?
ACP Amin Mahamba : Ni kweli.
Mhe. Lissu : Mimi nilitishia Serikali,Bunge na Mahakam?
ACP Amin Mahamba : Ulitishia Serikali
Mhe, Lissu : Nilitishia bunge?
ACP Amin Mahamba: hapana
Mhe. Lissu : Nilitishia Mahakama?
ACP Amin Mahamba : hapana
Mhe. Lissu : Ulisoma shtaka nililoshtakiwa nalo hapa Mahakamani?
ACP Amin Mahamba : Ndio nililisoma.
Mhe, Lissu analisoma tena.
Mhe. Lissu : Hayo ndo maneno uliyoyapeleleza?
ACP Amin Mahamba : kweli ndo hayo niliyopeleleza.
Mhe. Lissu : Unajua maana ya neno serikali?
ACP Amin Mahamba : nafahamu
Mhe. Lissu : Serikali maana yake nini?
ACP Amin Mahamba : Ni mamlaka inayoongoza nchi.
Watu wanacheka kidogo hapa 😂😂😂
Afande anasema Serikali ni Bunge Mahakama na Mihimili Tendaji.
Mhe. Lissu : Hiyo ni kwa mujibu wa nini?
ACP Amin Mahamba : Kwa mujibu wa Katiba yetu
Mhe. Lissu : Naomba asome Art 151 d
ACP Amin Mahamba anasoma
Serikali maana yake ni pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Zanzibar, Halmashauri au mtu anaetekeleza madaraka au mamlaka yoyote kwa niaba ya Serikali...
Mhe. Lissu : Kwenye maelezo yangu nimetaja Halmashauri ya Jiji la Dar, nimetaja jina la Makam wa rais Samia, Nimetaja jina la Waziri mkuu Kassim Majaliwa au Mwenyekiti wa mtaa wa mwakasusa?
Watu wanacheka hapa Mwakasusa sijui ni kule kwetu Mbeya.😂😂😂😂
ACP Amin Mahamba: Haujataja hayo majina
Mhe. Lissu ; Ieleze Mahakama nani anasimamia Uchaguzi
ACP Amin Mahamba : INEC
Mhe. Lissu ; Kwenye maelezo yangu nilitaja Tume na Viongozi wake ama Mwenyekiti au makamishna?
ACP Amin Mahamba : Sina uhakika
Mhe. Lissu : Je katika waliopeleleza yupo ASINSP Andrew Chulu na ndiye aliechukua memory card kutoka kwa P1 na P2 na kuleta Dar ?
ACP Amin Mahamba : sahihi ni yeye
Mhe. Lissu ; Ulisoma maelezo ya Insp Chulu?
ACP Amin Mahamba ; Ndio nilisoma.
Mhe. Lissu: Ni kweli au si kweli kwenye maelezo ya Chulu, kuna maelezo yafuatayo shahidi huyo P alinieleza alikuwa miongoni mwa mashahidi waliokuwepo kwenye Mkutano akitokea Jambo tv na kuirusha mubashara kupitia account ya YouTube ya Jambo tv na instagram ya Jambo tv?
ACP Amin Mahamba : Ni kweli
Mhe. Lissu : Na unasema umesoma maelezo ya P kweli au si kweli?
ACP Amin Mahamba : Kweli
Mhe. Lissu anarudia tena maelezo ya P kuwa Jambo TV walirusha maelezo ya Lissu live na walirusha kwenye mtandao wao wa YouTube hayo maelezo umeyasoma?
ACP Amin Mahamba : kweli nimeyasoma
Watu wanacheka 😂😂😂
Unajua huyu shahidi kule mwanzo alisema Mhe. Lissu ndo aliyechapisha na kupandisha Video kwenye account ya YouTube ya Jambo tv
Anyways tuendelee
Mhe. Lissu : Mnanitesea nini wakati mna ushahidi wa waliofanya makosa na kurusha hivi vitu mtandaoni?
ACP Amin Mahamba : Jukumu langu ni kupeleleza shtaka
Mhe: Lissu : Mnanitesea nini kama watu waliofanya kosa la kuirusha hiyo video mnao?
ACP Amin Mahamba : Hauteswi.
Part 229 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Agosti 11, 2026
Last time tuliishia Part 225 so leo tunaendelea na-;
Part 226
Jana Shahidi wa upande wa Jamhuri ACP Amin Mahamba alianza kutoa ushaidi wake na leo Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia Cross-examination.
Mhe. Lissu : Unaweza kuiambia Mahakama kwamba ulifufuka lini?
ACP Amin Mahamba : Sijaelewa
Mhe. Lissu : Mke wa Amin Mahamba anasema kwamba Amin Mahamba alifariki, sasa iambie Mahakama ulifufuka lini?
ACP Amin Mahamba : Huyo Amin Mahamba anaetajwa sio mimi.
Mhe. Lissu : Kwahiyo ni ushahidi wako kuwa huyu Amini Mahamba ni mwengine sio wewe?
ACP Amin Mahamba : Ndio ni mwingine tena yeye ni mstaafu na wanasema alishariki kweli kama unavosema.
Mhe. Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji kama ulimshirikisha RSO kwenye upelelezi wako?
ACP Amin Mahamba : Sikumshirikisha
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama ulimshirikisha afisa yoyote wa TISS.
ACP Amin Mahamba : Sikumshirikisha
Mhe. Lissu: Unafahamu Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa?na kama uliishirikisha kamati ya ulinzi ya mkoa wa Dar es salaam?
ACP Amin Mahamba :Naifahamu na sikuwaashirikisha
Mhe. Lissu : Ulishirikisha ikulu?ofisi ya VP au Waziri mkuu?
ACP Amin Mahamba : Sikuishirikisha na sikuwaambia lolote.
Mhe. Lissu : Ulishirikisha ofisi ya DPP ndio nilishirikisha kanda maalum NPS.
Mhe. Lissu :Ulimshirikisha nani?
ACP Amin Mahamba: Incharge Mayenga
Mhe. Lissu : Umesema kokote kwenye nyaraka yako?
ACP Amin Mahamba : Sijasema na sijamtaja
Mhe. Lissu : Kwa mujibu wa sheria ya NPS mwenye jukumu la kuratibu upelelezi ni DPP na Mastate Attorney wake.
Waeleze ni DPP yupi au State Attorneys yupi?
ACP Amin Mahamba : Kimya
Mhe. Lissu : Jibu swali wewe Polisi
ACP Amin Mahamba : Sijaelewa swali.
Mhe. Lissu : Swali langu linahusu nani aliecordinate upelelezi?
ACP Amin Mahamba : Ni DPP Mwenyewe, aliteua mtu nilisema jana kuwa sijui jina lake alitoka ofisi ya DPP Dodoma na nilisema ana jina la kibantu nimesahau.
Mhe. Lissu : Tutaenda kwa DPP Mwakitalu atupe hilo jina tuko kwenye serious matters.
😂😂😂 inachekesha sana maana jamaa hajui jina la mpelelezi ambae alishirikiana nae kufanya upepelezi pamoja na kufungua faili la kesi hii.
Mhe. Lissu : Umesema wewe ni mpelelezi wa muda mrefu umewahi peleleza kesi ya kisiasa?
ACP Amin Mahamba : Sijawahi
Mhe. Lissu : Kesi ya uhaini ni kesi kubwa sana ni highest in the land kwahiyo hujawahi kabisa na hii ndo kesi ya kisiasa ya kwanza.??
ACP Amin Mahamba : Sijawahi hii ndio ya kwanza
MheZ Lissu : Umewahi peleleza kesi ya mtu alikuwa mbunge na kiongozi wa Chama kama lissu?
ACP Amin Mahamba :Sijawahi
Mhe. Lissu : Umesema kitengo chako kinashugulika na makosa ya mtandao
ACP Amin Mahamba : Ndio
Mhe. Lissu: Ushapeleleza kesi ya cybercrime?
ACP Amin Mahamba : Ndio nimewahi.
Mhe. Lissu : Kesi gani shahidi?
ACP Amin Mahamba ; Nakumbuka nikiwa RCO Kinondoni
Naona kasita kama dakika 5 hivi then akasema kesi ya Mbowe na Mzee wa karatu Slaa
Mhe. Lissui : Waeleze ilikuwa inahusu nini na iliishaje?
ACP Amin Mahamba ; DPP hakuwa na interest ya kuendelea na kesi ikaisha hewani.
Mhe. Lissu : Una kesi zingine zaidi ya hizi kwenye cybercrime?
ACP Amin Mahamba ;Hapana
Mhe. Lissu: kwahiyo hauna kesi nyingine zaidi ya hiyo iliyofutwa?
ACP Amin Mahamba : Ninazo nyingine nyingi siwezi kuzikumbuka nikiwa RCO na OCCID.
Mhe. Lissu : Kwahiyo jana kweye ushahidi wako unasema mimi ndie niliechapisha video yangu hapa mtandao wa Jambo tv?
ACP Amin Mahamba : Ndiyo nilisema.
Mhe. Lissu ; Unafahamu maana ya neno kuchapisha mtandaoni?
ACP Amin Mahamba : Ndio nafahamu lakini sheria ambayo imetumika kukushitaki sio Cybercrime.
Mhe. Lissu : Waeleze waheshimiwa majaji kama mm ndie nilisambaza video za YouTube kwenye mtandao wa Jambo tv?
ACP Amin Mahamba : Ndio ni wewe ulisambaza hizo video.
Part 227 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
@JamiiForums Hao Polisi wanafanya mangapi gizani?
Ile kesi ya Msaidizi wa Lissu kujaribiwa kutekwa na kufunguliwa pingu polisi mbona uchunguzi haufanyiki?
Hii nchi inaongozwa na wapumbafu.
@Jambotv_ Kama haya mauaji yaliyotekelezwa na Polisi kwa amri ya SSH yalikuwa na uhalali hizi tume zinazoundwa juu ya jambo hili ni za nini? Na haya wanayoyaita maridhiano ni ya kazi gani?
Hili taifa kinaongozwa na wapumbavu wa hali ya juu!
Vitu ambavyo tunataka VICHUNGUZWE na tume ya KIMATAIFA.
1. Nani alizima mtandao kwa zaidi ya siku 5? Kwa maslahi ya nani?
2. Tamko la IGP WAMBURA kufungia watu ndani kwa kazi maalumu. Kazi hiyo maalumu ni ipi waliyofanya?
3. Wale Askari waliokuwa wanapiga RISASI ZA VICHWA WATU MTAANI nani aliwapa ruhusa ya kuuwa watu hovyo hovyo?
4. Watu waliokuwa wanatolewa mahospitali na kuenda KUZIKWA kwenye makaburi ya halaiki wamezikwa WAPI?
5. Kauli za “HAKUTAKUWA NA NYWI NYWI WALA NYWI NYWI” ilitoewa kwa msingi upi na dikteta JIKE?
Kinyume na hapo, ukweli utachelewa tuu ila UTAFAHAMIKA SIKU MOJA.
REPOST 500.
Dikteta Museven ameweka wapinzani wake, Mzee Kizza Besigye, Sam Mugumya & co, jela kwa zaidi ya mwaka. Ameuwa mamia, huku wengi, ikiwemo Bobi Wine, wamekimbilia uhamishoni. Samia amemuomba ampe Jaji amchunguze kwa Majuwaji aliyofanya tangu Oktoba 29. Huu ni ujinga squared!!
@royalmediatz Pumbaf! Yaani mshindwe kuelewana mnapoishi mkaelewane ugenini?
Vyama vya mfukoni vinalazimisha rushwa ya safari.Hakuna vyama humo na huyo SSH na genge la hivyo vyama wanajichoresha tu kwa wananchi.
Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai ya Tanzania inatambua Jeshi la Polisi tu kama chombo pekee cha kufanya UPELELEZI/UCHUNGUZI wa makosa ya jinai & Ofisi ya DPP ndiyo yenye MAMLAKA ya kuanzisha mashtaka.
Hii inayoitwa tume ya uchunguzi wa jinai ya #MO29, italeta MGOGORO na nahisi itatokea hivi; tume itapokea taarifa za UKWELI toka kwa wananchi, mtawala ataikataa, halafu taarifa itafanyiwa MABADILIKO ya UONGO ili mtawala afurahi.
Lakini, kisheria ni kwamba, DPP akifungua mashtaka dhidi ya mtu au kikundi cha watu, basi hao wajumbe wa tume itabidi waje KUTOA USHAHIDI mahakamani kwa sababu wanahusika kwenye ule MNYORORO wa kupatikana kwa ushahidi (chain of custody/evidence).
Ikitokea wajumbe wakasema uongo, hapa ndipo tutaleta wananchi waliotoa taarifa kwa tume hiyo kufanya COUNTER-ATTACK ya kibabe.
Binafsi, naomba Mungu hili suala lifike mahakamani ili ifungue PANDORA BOX ya yaliyomo kwenye ile tume ya Jaji Chande pia. Moto mzito utawaka!!
@420Cousin Ikishakamilika bei itakuwa nafuu kuagiza uarabuni kuliko kununua hapa.
Bwawa la mwalimu Nyerere bei ilipungua?
Vipi gesi ya Mtwara?
Msituchoshe Chawa.
@royalmediatz Huyu jamaa anafanya mambo ya hovyo hovyo ikiwamo mambo ya kumiliki vikundi vya kigaidi kakini hakamatwi wanakamatwa wasiohusika.
Hii inamaanisha Samia uwezo wake wa kufikiri ndio kama huyu jamaa.