@DenyTheDr Katavi atasoma kwa vitendo zaidi, Chuo kipo halmashaur ya Mpimbwe wilaya ya Mlele, inaongoza kwa ulimaji wa nyuki kwa ukanda ule.
Kama nia yake kupata elimu, huko panamfaa zaid, atajifunza maisha mengine mapya na atakuwa tayar kuishi sehemu yoyote ndani ya Tanzania hii.
Aende tu.
@kasulukwetu@HilmiHilal88 Ukifanikiwa kuweka standard kwenye familia yako, hadi vitukuu vyako vitakuja kujilinganisha na wewe, haijalishi ni vizazi vingap vimepita katikati yao.
Nyerere ni MTOSA wa taifa hili, na ni Mtosa wa Africa by Nkwame Nkurumah
@jaliluzaid@tonyalfredk Nimeamini kuswali na kuhifadh Quran hakuna Uhusiano na "Utu"... Unaweza ukawa mtu wa swala 5 lkn ukawa huna "Utu".
Ndio maana naamini Pepo itakuwa ngumu sana.
Iko hivi,
Kukakola moja yenye mls 350 ina takriban gramu 39 za sukari, sawa na vijiko 10 vidogo vya chai vya sukari.
Funta Chungwa yenye mls 350 ina takriban gramu 44 za sukari, sawa na vijiko 11 vidogo vya chai vya sukari.
Pipsi yenye mls 350 ina takriban gramu 41 za sukari, sawa na vijiko 10–11 vidogo vya chai vya sukari.
Upande mwingine, chai unayoweka vijiko vidogo, kawaida vijiko vidogo 1 mpaka 3, vina takriban gramu 8–9 za sukari tu.
Mpaka hapa utaona chai ni bora zaidi kuliko soda, kwa sababu ina sukari kidogo sana na haina madhara makubwa ikiwa inakunywa kwa kiasi.
Sasa utamu upo hapa, hizi sukari zinatofautiana, hapa ndipo madhara ya soda yanaonekana.
Sukari iliyopo kwenye soda inaitwa high-fructose corn syrup (HFCS) au sucrose, hii inatengenezwa kutoka kwenye mahindi, ni mchakato mrefu, mahindi yanachemshwa, unga wake unachakatwa na kemikali na ule wanga unabadilishwa kuwa glucose kisha sehemu yake inabadilishwa kuwa fructose, huu utamu wake balaa, ndio sukari ya soda, kifupi soda ule utamu ni kemikali zimechanganywa.
Sasa mwilini hii sukari ya soda huchakatwa na ini, na ukinywa nyingi, yaani zaidi ya unavyohitaji (nguvu unazotunia au mazoezi) ndipo ini hubadilisha kuwa mafuta ili itunze kenye stoo za mwili (nyuma matakoni na tumboni), mtu ananenepa, mafuta yanaongezeka mwilini + sukari na hapo ndipo anasogelewa na magonjwa ya kisukari na moyo.
Sukari ya chai hii tunakoroga yenyewe ni sucrose ya kawaida, yaani table sugar, kwanza tofauti na ile ya soda inayotokana na mahindi hii inatokana na miwa au beetroot, pili hii unakunywa gramu chache tu (8-9) na tatu mwili huitumia sukari hii moja kwa moja kama nishati na hatari ya kubadilishwa mafuta ni ndogo kama unatumia kiasi hiki kidogo.