بعض البشر لو أعطيته في كفيك عسلًا، يأكل العسل وبعدها يعض اليد التي أكرمته
Baadhi ya watu, hata ukiwapa asali mikononi mwako, wataila hiyo asali, kisha baadae wataung'ata mkono uliowatendea wema.
✍️ Kuna watu hawana shukrani, hata uwafanyie wema kiasi gani. Badala ya kukushukuru wanaweza kukudhuru.
السهر جميل حين تختاره، لكنه مؤلم حين يختارك
Unapochagua kukesha basi mkesha unakuwa mzuri. Lakini mkesha unapokuchagua wewe, hapo ndipo maumivu ya kukesha yanapoanza.
Kama unarafiki yako ana familia, au kwao yeye ndio mtegemewa. ....akakupigia simu jioni nakukwambia mambo yake sio mazuri anaomba elfu kumi au tano. ......
Tafadhali mpatie hata kama huna kwenye simu nenda kaweke mtumie😢😓
Mojawapo ya vitu vinavyopunguza machungu ya maisha ni matumaini kuwa mambo yatakuwa poa siku moja. Bila matumaini maisha yangekuwa magumu zaidi.
Usiache kumtumainia Mungu wako. Tumaini ndio faraja pekee unaweza kuwa nayo ndani yako bila hata kuambiwa na mtu.
Urafiki unakuwa na maana pale kila mmoja wenu anapojua kuwa tumeshakua watu wazima na kila mmoja ana majukumu yake na kuheshimu hilo , kwa hiyo sio kila wakati tutaonana, ila siku tukionana ni kama tunaendelea tulipoishia juzi.
بعض الناس مجرد أن تختلف معهم تتحول أسرارك إلى إعلانات تجارية
Baadhi ya watu ukitofautiana nao tu, siri zako zote hubadilika na kuwa kama matangazo ya biashara.
Big up kwa WADADA wote wanaopambania ugali kwa jasho lao,big up kwa mabinti wote wanaotafuta kipato chao cha halali,Big up kwa madada wote waliobeba nafasi ya baba.
Wanaopambania kipato sababu ya wadogo zao,Mama zao na familia zao kwakuwa tu kwa familia hakuna wa kuchukua jukumu
Kwenye simu yako una washikaji wengi wenye pesa lakini ukipata Shida, amini utasaidiwa na washikaji zako wasiokuwa na pesa Ishi nao kwa akili, thamini anaekuthamini.
MUNGU naomba hela, zisiwe nyingi sana zitoshe tu kuiondolea fedheha familia yangu.
Zikidhi mahitaji yote,yanayohusiana na furaha za wanaonitegemea.
Zi solve na Matatizo ya marafiki zangu na ziwainue wanao tazama.
Nizitumie hadi nisiojuana nao, nitawapa sadaka ya kushukuru kwangu.