Katika kumbu kumbu ya siku ya mfanano wa kuzaliwa kwangu ,Ujumbe wangu kwako ni Ujitahidi kuwa mtu bora na kutenda kwa haki kwa kadiri utakavyo jaliwa na Mungu.
Simama na wanao onewa siku zote Paza sauti kwa niaba ya wasio na sauti, kemea dhuluma,onya kwa haki shauri au adhibu kwa haki.
Namna pekee ya kukufanya wewe kuwa salama ni kwa kuhakikisha Usalama wa Jirani aliye karibu nawe.
KATIBA ndiyo Msingi wa Sheria Bora.
Katika kumbu kumbu ya siku ya mfanano wa kuzaliwa kwangu ,Ujumbe wangu kwako ni Ujitahidi kuwa mtu bora na kutenda kwa haki kwa kadiri utakavyo jaliwa na Mungu.
Simama na wanao onewa siku zote Paza sauti kwa niaba ya wasio na sauti, kemea dhuluma,onya kwa haki shauri au adhibu kwa haki.
Namna pekee ya kukufanya wewe kuwa salama ni kwa kuhakikisha Usalama wa Jirani aliye karibu nawe.
KATIBA ndiyo Msingi wa Sheria Bora.
SASA KWANINI TUNAKATAA URAIA PACHÀ KAMA URAIA UNAWEZA KUGAWIWA KWA WAGENI KWA URAHISI NAMNA HII ?
Kimsingi sheria ya Uraia imeweka bayana kwamba kigezo cha Msingi cha Mtu anayeomba Uraia lazima awe ameishi Tanzania kwa Kipindi kisicho pungua Miaka 10
Aidha yapo mazingira maalum ambapo mgeni ambaye hajatimiza miaka 10 ya kuishi Tanzania anaweza kupewa uraia.
Hii ni kwa mujibu wa Sheria ya Uraia ya Tanzania, Sura ya 357. Haya ni mazingira maalum yanajumuisha
1. Uraia wa Heshima (Honorary Citizenship) Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi anaweza kumpa mtu uraia wa Tanzania kwa njia ya heshima ikiwa mtu huyo:
a. Amechangia kwa kiwango kikubwa katika maendeleo ya nchi ya Tanzania, mfano katika uchumi, kijamii, au kisayansi.
b. Anajulikana kimataifa kwa sifa nzuri au kwa mchango wa kipekee katika jamii.
Katika mazingira ya namna hii Mh.Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi anayo mamlaka kisheria kumpa mtu URAIA bila kuhitàjika kukaa miaka 10 hapa nchini.
2. Uraia kwa Ndoa
Mtu anayeolewa au kuoa raia wa Tanzania anaweza kuomba uraia baada ya kuwa kwenye ndoa kwa kipindi kisichopungua miaka 2 na kuishi Tanzania kwa muda huo. Hata hivyo, lazima aoneshe dhamira ya kuendelea kuishi Tanzania.
3. Watoto wa Mgeni Aliye Raia wa Tanzania
Mtoto wa chini ya miaka 18 wa mgeni ambaye amekuwa raia wa Tanzania anaweza kupewa uraia wa Tanzania, hata kama hajaishi miaka 10. Mtoto huyo lazima awe anaishi chini ya uangalizi wa mzazi wake.
4. Uraia kwa Upendeleo Maalum
Sheria inampa Waziri wa Mambo ya Ndani mamlaka ya kumfikiria mgeni kwa upendeleo maalum hata kama hajaishi miaka 10, ikiwa ni kwa maslahi ya kitaifa au hali nyingine maalum.
5. Wakimbizi Waliopo Tanzania
Kwa mujibu wa sheria za kimataifa na makubaliano ya kikanda, wakimbizi wanaweza kupewa uraia wa Tanzania kwa upendeleo maalum, hata kama hawajatimiza miaka 10, baada ya taratibu za kuandikishwa kama wakimbizi kukamilika na kukidhi vigezo vingine.
Muhimu;
Ingawa sheria inataka muda wa miaka 10, kuna mazingira maalum kama yaliyoainishwa hapo juu ambapo mgeni anaweza kupewa uraia kabla ya kutimiza muda huo kupitia Mamlaka ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Hata hivyo, maamuzi yote ni kwa mamlaka ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye ana mamlaka ya mwisho juu ya maombi yote ya uraia hapa Tanzania.
Haya ni maoni yangu kwa Ujumla lakini kila nikijaribu kuangalia hao wachezaji 3 wa Singida United ambao ndiyo chanzo cha kuibuka kwa hoja za wananchi kwa maoni yangu sioni ni yupi kati yao anaye angukia katika exception hizo hapo Juu.
Waziri mwenye dhamana atoke na kutueleza kwa kutoa ufafanuzi wa kina unao eleweka.Hatupingi watu kupewa uraia lakini Uraia haupewi kama Karanga za kuonjeshwa.
Lazima Kuzingatia sheria na Taratibu.
BAK Mwabukusi
Shambani Busokelo