Wakija kwa sura kirafiki wakati ni maadui wakaribishe tu kwa furaha, wakija kama Marafiki na wakaishi kirafiki wakaribishe tu
Kitu kimoja ambacho wanapaswa kujua, kwasasa huhitaji Marafiki wala Maadui, unahitaji watu wa fursa na michongo
Rafiki au Adui kama una mchongo? KARIBU
Maisha yetu ni mafupi sana. Tusali. Huwezi kupendwa na wote lakini tuwapende wanaotupenda. Tupunguze maadui. Tuipiganie nchi yetu iwe sehemu salama kuishi kesho. Tujitahidi kuwa na familia. Tupate watoto. Tuwape elimu. Tuwatafutie mali. Tusitelekeze watoto wetu, ndiyo urithi.
Raia waliojitokeza hapa mahakamani wamempokea Freeman Mbowe wakimuita โRais, Rais, Raisโ na ulinzi wa askari Polisi na askari magereza ni mikubwa sana, raia pia ni wengi sana katika viwanja vya mahakama. #MboweSioGaidi
Maisha ni mazuri ukiwa na furaha. Lakini yatakuwa mazuri zaidi watu wengine wakiwa na furaha kwa sababu yako. Tuishi tukiwatendea wengine mazuri bila kuhesabu. Tunaweza kuifanya Dunia kuwa sehemu salama kuishi. Tuache alama kwenye uso wa Dunia. Tufanye yetu, tusingoje, tusepe.
Mtoto wa Waziri mkuu Mstaafu aliyesoma Weruweru na Kilakala kisha akasoma UDSM na baadaye akasoma zaidi huko UK. Akafanya kazi NIMR na baadaye akapata nafasi ya juu huko UN Shirika la Afya. 2015 akachukua fomu CCM ya Kuwania Urais, Dr.Mwele Malecela amefariki akiwa na miaka 58.
Kazi ya MAHAKAMA ni KUSIKILIZA pande zote kwa ukamilifu chini ya Ibara ya 13(6)(a) ya Katiba na kisha kutoa UAMUZI. Ni kosa kubwa Sana HAKIMU kumzuia WAKILI wa utetezi ASIONGEE. Kazi ya HAKIMU siyo KUENDESHA MASHITAKA.