Tupiganie Katiba Mpya kivipi Wakati Lissu alipigania Katiba Mpya mkamfungulia kesi ya Uhaini?
Tukomae na Katiba Mpya kivipi wakati Vijana walipokomaa na Katiba Mpya mwaka jana mliwapiga risasi za moto na kuwaua?
Tupiganie Katiba Mpya gani ambayo vijana wa CHASO Mbeya, Mwanza, Iringa na mikoa mingine wakifanya hivyo wanafunguliwa kesi za Ugaidi na Uhaini?
Tupiganiaje Katiba Mpya wakati Dr. Melkisedeki Kaijage wa UDOM amewaambia wanafunzi wake Darasani kuwa kuandamana ni Haki ya Kikatiba leo amefunguliwa kesi ya Ugaidi?
Unasemaje kama unataka Amani lazima Utende Haki na usione aibu kutamka haki katika mazingira ya nchi ambayo Vijana wanatekwa, wanapotezwa, wanafunguliwa kesi za uongo za ugaidi na uhaini ? Wanaoruhusu haya yafanyike ni akina nani Bwana Nchimbi atueleze tumuelewe.
BAVICHA tumesema huu ni wakati tunaohitaji VITENDO dhidi ya MANENO. Hatuhitaji kauli tamu za kutufurahisha.
Wanaokula kodi zetu watanzania tunahitaji watuambie:
Katiba Mpya itapatikanaje kabla ya 2029 na 2030 wakati hadi sasa hakuna Bajeti ya Mchakato huo?
Hakuna Calendar ya matukio ya namna mchakato huo utakavyofanyika na kukamilika. Tutaaminije?
Msimamo wa BAVICHA na Chama chetu ni No Reforms: No Election kwa Uchaguzi wa 2029 na ule wa 2030. Ni muhimu wanaotumia kodi za Watanzania wakawekeza kwenye kuhakikisha mazingira ya kupatikana Katiba Mpya ya Wananchi inapatikana kweli na sio mbwembwe na propaganda.
Deogratias Mahinyila @AdvMahinyila
Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa.
24/07/2026.
MaCCM wamefilisika kisiasa; wamebaki kutegemea nguvu za dola na Mahakama, ambako bado tunawashinda kwa hoja. Sasa wanajaribu kuzuia CHADEMA kuzungumza na waandishi wa habari nje ya viunga vya Mahakama. Hii ni baada ya kesi ya kikatiba inayohusu haki za Tundu A.M Lissu gerezani ikiwa ni pamoja na haki ya faragha kwa mawakili wake. Polisi wanadai hii ni amri kutoka kwa Msajili wa Mahakama. Nafikiri, tutaihoji amri hii Mahakamani na kuhakikisha sheria inatunzwa, inalindwa na kuheshimiwa!
#FreeTunduLissu #TunduLissuSioMhaini
#FreeTunduLissu #TunduLissuSioMhaini
Kwenye post za hili tamko la leo kuhusu wa 🇹🇿 pambanieni katiba.
Comments nyingi zinasema
-Huyu anatufaa anaongea lugha yetu.
-Anavyoongea kwa upole hadi raha
-Huyu anaonekana ana huruma na wananchi
-Mzee kanyooka sana anatufaa!!
Kiukweli mitanzania ni mibumunda sana, rahisi kweli kuichota akili 🚮
aaaf inasahau haraka!!
Inasahau kuwa kila aliyekuja kuwa miyeyusho alianza kwa lugha tamu hizo hizo!!
Mimi nitakuwa wa mwisho kumuamini whoever anayetoka upande ule wa vegetables.
Ni kweli VICEnt seems like a good man, tatizo anaongelea akiwa wapi!!
Mimi moyo wangu umekuwa mzito sana kuwaamini hawa……
Wamiliki wa project ya kumchafua Heche na tone tone leo wametoka fronti. AIBUUUUU..
KUCHANGIA TUMA PESA:
M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ
NMB Bank
Namba ya Akaunti: 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche leo Julai 22, 2026 akizungumza na Waandishi wa Habari katika ofisi ya chama hicho Kanda ya Pwani amesema hawako tayari kufanya maridhiano ya maigizo na wamepewa maagizo na Mwenyekiti wao wa Taifa, Tundu Lissu kufanya kazi.
Kama ishara ya kuridhishwa na kile kinachofanyika, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu amemtaka Makamu Mwenyekiti wake Bw. John Heche kutia bidii zaidi kwenye kile anachokifanya kama Kiongozi wa Chama hicho cha Upinzani Nchini Tanzania.
Hayo yamejiri leo Jumatano Julai 22, 2026 wakati Heche akimpa salamu Tundu Lissu, wakati wa usikilizaji wa shauri la Lissu kwenye Mahakama kuu Jijini Dar Es Salaam, akisema "ukiona wanalialia ujue kazi zimewafikia".
"Peleka moto, peleka moto, ukiona wanalialia ongeza moto zaidi. All the best, wasalimie familia na waambie wana baraka zangu zote." Amesikika Lissu akimueleza Joh Heche.
✊🏽 #FreeTunduLissu
Today Lissu exhibited his legal expertise in court and proved why he is one of the best human right lawyers in the history of #Tanzania
Yataisha tu! Hawana namna na wanajua!
Mwandishi mkongwe wa habari na mchambuzi wa masuala ya kijamii na kisiasa, Jenerali Ulimwengu, ameibua hoja kuhusu mchakato wa maridhiano ya kisiasa nchini Tanzania, akihoji wahusika wakuu wa mazungumzo hayo ni akina nani.
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X, Jenerali Ulimwengu ameandika akisema, “Maridhiano mnayojadili ni kati ya nani na nani? CCM na CHADEMA? CCM iko Polisi, CHADEMA iko Ukonga. Sasa tufanyeje? Tuwafungulie CCM kutoka Polisi na CHADEMA toka Ukonga, ndipo tutapata fursa ya maridhiano ya aina yoyote."
Kauli hiyo imekuja wakati mjadala wa maridhiano ya kisiasa ukiendelea nchini, huku baadhi ya wadau wakitaka hatua za kujenga mazingira ya mazungumzo ya wazi baina ya vyama vya siasa. ([Chama Cha Mapinduzi][1])
Katika ujumbe wake, Ulimwengu anaonekana kuhoji uwepo wa hali anayodai kuwa inazuia mazungumzo ya kweli, akitaja kuwepo kwa viongozi au wanachama wa pande za kisiasa katika mazingira ya kizuizi cha kisheria.
Mchakato wa maridhiano umekuwa sehemu ya mjadala mpana wa kisiasa baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na matukio yaliyofuata, huku vyama mbalimbali vikiwa na mitazamo tofauti kuhusu namna ya kushughulikia changamoto za kisiasa zilizopo.
Ujumbe wa Jenerali Ulimwengu umeibua mjadala miongoni mwa wananchi na wanasiasa kuhusu maana ya maridhiano, wahusika wake, pamoja na hatua zinazohitajika ili kujenga mazingira ya mazungumzo ya kisiasa yenye ufanisi.
"Kuna jambo linafurahisha sana kama Taifa kwamba kila mtu kwa nafasi yake anazungumzia maridhiano ya Kitaifa hasa kuanzia kwenye Chama chetu, Mwenyekiti Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu wake Mzee Wassira, kila mtu anazungumzia maridhiano hilo kwa busara linaonesha kuwa ipo sehemu tumekwama, tumekosea na ninaamini hata upinzani pia unaamini katika maridhiano ila tuwe wakweli wapinzani nchi hii ni Chadema tu, vyama vingine hata mtoto anajua tu kuwa hawa wengine ni mitego tu."
"Shida inakuja tunafanyaje maridhiano wakati Mwenyekiti wao yupo ndani? Sasa maridhiano yatakuwa ya aina gani? Maridhiano yanahitaji watu wenye nguvu kuridhiana, kwahiyo mimi ninaamini Mhe. Rais kwa nia njema kabisa bila kushinikizwa na mabeberu naamini Bw. Lissu atakuwa nje ili turidhiane, twendeni kwenye uhalisia."- Seleman Msindi maarufu kama Afande Sele leo Jumamosi Julai 18, 2026.
Agenda ya kufunika wizi mkubwa kwenye sketa ya mafuta.. Watanzania msikubali.
Tunataka kujua kwanini Vitol ametuuzia mafuta kwa usd 260 sawa sh 689,000.
Wakati huo huo anawauzia Uganda mafuta hayo hayo kwa USD 83 sawa na sh 212,000
Msumbiji usd 90 sawa na 238,500.
Hawa watu wanaoitwa NAMARO na TPDC wamehusikaje kwenye huu ufisadi wa kufilisi Nchi.
Huu ni uhujumu uchumi mkubwa kuwahi kutokea katika Nchi hii.
Kuna zaidi ya 1.2 trilioni imeibiwa katika mafuta.
Katibu mkuu wa Nishati bwana Mataragio alisema tuna mafuta ya kutumia miezi mitatu.
Watanzania tusikubali huu wizi.
Vitol yuko na nani?
Nani wamempa tenda ambayo Watanzania wanauziwa mafuta kwa usd 200-260 wakati Uganda anauziwa usd 83 na Msumbiji anauziwa usd 90.
Hawa Namaro waliosajiliwa Dubai mwaka 2023 ni kina nani? Wana uhusiano gani na wizi huu mkubwa unaoumiza Watanzania.
Vyombo vya habari Tanzania kwanini hamfuatilii na kuandika huu ujambazi unaongamiza Nchi kwenye wizi wa mafuta..
TPDC kwanini hawakutoa tenda shindanishi katika suala kubwa kama hili la mafuta.