Hatujaamka kwa bahati, na hatupaswi kuishi bila malengo. Leo ni nafasi nyingine ya kurekebisha jana, kujenga kesho na kusogea karibu na ndoto zetu. Mapambano yanaendelea, bila kuchoka wala kurudi nyuma. Mungu atutangulie katika kila jambo.
Good Morning Family
Mungu Nakushukuru Kwa Kuniamsha Salama.Asante Kwa Zawadi Ya Pumzi Ya Uzima,Afya Njema,Na Nafasi Nyingine Ya Kuiona Siku Mpya Ambayo Wewe Umeifanya.Naomba Nifungulie Milango Ya Baraka,Kibali,Na Mafanikio Katika Kila Eneo La Maisha Yangu.🙏🏼
Good Morning🌄Ladies And Gentlemen🫂
HABARI:
Aliyekuwa Mgombea Urais kupitia Act Wazalendo 2025 na Mbunge wa zamani wa Jimbo la Kisesa, Luhaga Mpina akizungumza na wanahabari leo Oktoba 15, 2026.
VIDEO:
Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu akiingia mahakamani kwa ajili ya kusikiliza hukumu ya kesi ya kikatiba juu ya haki za Mawakili wake kumuona na kuzungumza nae kwa usiri akiwa Gerezani.
Hukumu hiyo itatoelewa katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam na Jopo la Majaji watatu wakiongozwa Jaji Amir Mruma.
Siku nyingine, nafasi nyingine, na mwanzo mwingine wa kupambana na maisha. Tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa zawadi ya uhai, tusali kwa imani, tufanye kazi kwa bidii na tuishi kwa nidhamu.
Good Morning Family
Kusema mtu hana hatia hadi athibitishwe kuwa nayo ni kanuni iliyopo kwenye Ibara ya 13. Lakini mtu anayekaa mahabusu miaka mitano bila hukumu tayari ameadhibiwa. Katiba mpya iweke haki ya kusikilizwa kesi ndani ya muda unaofaa, na fidia kamili kwa wanaocheleweshwa. #KatibaMpya
Mtu anapopata baraka, jizoeshe kuwa mwitikio wako wa kwanza uwe ni dua badala ya kujilinganisha naye.
Riziki yao haipunguzi riziki yako, na furaha yao haipaswi kuwa chanzo cha huzuni kwako.
Muombe Mwenyezi Mungu awabariki na kuisafisha moyo wako.
Mwenyezi Mungu anasema:
Sitakuacha kamwe uingie katika hali yoyote peke yako.
Ninatangulia mbele yako, Ninasimama kando yako, ninatembea nyuma yako.
Hali yoyote unayokabiliana nayo, uwe na uhakika kwamba niko pamoja nawe.🤍
Mwenyezi Mungu atujaalie mwisho mzuri kwa vipindi vigumu vya Maisha yetu, Heri zisizotarajiwa katika mambo yetu, na Nyoyo zinazodumu kwa Shukrani katika kila hatua ya Maisha yetu, walinde tunaowapenda, na utufanye kuwa chanzo cha Heri popote tunapokwenda.
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, amelitaka Jeshi la Polisi kutoa majibu ya wazi kuhusu hatima ya watu wanaoripotiwa kutekwa na kupotea, akiwataja Mdude Mpaluka Nyagali, Soka na Humphrey Polepole, akisisitiza kuwa familia zao na Watanzania wana haki ya kufahamu ukweli kuhusu walipo.
Mwabukusi amesema kuna haja ya Jeshi la Polisi kuweka wazi taarifa za uchunguzi kuhusu Mdude Mpaluka Nyagali, huku akihoji hatua zilizochukuliwa kubaini hatima ya Soka na Humphrey Polepole. Amesisitiza kuwa masuala hayo yanahitaji majibu rasmi ili kuondoa sintofahamu inayozikabili familia zao na wananchi kwa ujumla.
Katika ujumbe aliouchapisha leo, Oktoba 9, 2026, Mwabukusi pia amelitaka Jeshi la Polisi kueleza ukweli kuhusu matukio ya Oktoba 29, 2025 na siku zilizofuata, akitaka kufahamika waliohusika na vifo vya wananchi, madai ya matumizi ya amri ya “shoot to kill” na mazingira ya kuondolewa kwa majeruhi hospitalini pamoja na madai ya baadhi yao kupotea.
Amehoji pia silaha zilizotumika katika matukio hayo zilitoka wapi, nani alizitoa na nani alitoa amri ya kuzitumia, huku akitaka uchunguzi wa kuaminika kuhusu madai ya wananchi kunyimwa huduma za matibabu na familia za marehemu kupewa taarifa zisizo za kweli wakati wa kukabidhiwa miili ya wapendwa wao.
Kwa mujibu wa Mwabukusi, maswali hayo yanahitaji majibu rasmi, uchunguzi huru na uwajibikaji kwa wote watakaobainika kuhusika. Amesema familia za watu waliopotea zina haki ya kujua hatima ya wapendwa wao, huku waathirika wa matukio ya Oktoba 29 na wananchi kwa ujumla wakistahili kufahamu kilichotokea.
Aidha, amelitaka Jeshi la Polisi kueleza hatua zinazochukuliwa dhidi ya watu wanaotoa vitisho vya wazi kwa wananchi, wakosoaji wa Serikali na wanaharakati, akisisitiza kuwa sheria inapaswa kutumika kwa usawa bila upendeleo.
Mwabukusi amesema amani ya kudumu haiwezi kujengwa kwa kufunika majeraha ya wananchi, akitaka ukweli, haki na uwajibikaji vipewe kipaumbele badala ya kauli na maonyesho ya kujenga taswira nzuri mbele ya umma.
Kama maisha yanaweza kumuondoa mtu ambaye hukuamini kabisa kuwa unaweza kumpoteza, yanaweza pia kukuletea mtu ambaye hukuwahi kabisa kuota kuwa naye..!! 📌
Mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (BAVICHA) Mkoa wa Mbeya, Elisha Chonya, amesema kesi inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, ni kesi ya uhaini ambayo kwa mujibu wa maelezo yake inaweza kupelekea adhabu ya kunyongwa hadi kufa.
Akizungumza katika kikao cha ndani cha BAVICHA kilichofanyika Oktoba 7, 2026, Chonya amesema Serikali na vyombo vyake vimeendelea katika mchakato wa mahakamani unaolenga kuthibitisha madai kwamba Lissu alitenda kosa la uhaini na kwamba anastahili adhabu hiyo.
Chonya amehusisha kesi hiyo na historia ya kushambuliwa kwa risasi kwa Lissu, akidai kuwa watu waliokuwa wakihusishwa na tukio hilo kama wasiojulikana sasa wanaonekana katika mazingira tofauti kutokana na mchakato wa kesi unaoendelea dhidi yake.
Amesema endapo kutakuwa na hatua za kumwadhibu Lissu kwa sababu ya msimamo wake wa kisiasa na wa chama, wanachama wengine wa CHADEMA wanaendelea kuwa tayari kusimamia msimamo wa chama hicho.
Aidha, Chonya amesema msimamo wa Lissu kuhusu kupinga sheria anazoziona kuwa kandamizi, za uovu na za uonevu si msimamo wake binafsi, bali ni msimamo unaoelezwa na CHADEMA kama chama.
Katika hatua nyingine, Chonya amesema CHADEMA inaamini katika utawala unaozingatia uwazi na uwajibikaji, pamoja na kuwashirikisha wananchi katika kutoa maoni na kushiriki katika mchakato wa kutunga sheria.
Wateja wa Yas na Mixx wataweza kupata msaada wa huduma moja kwa moja masokoni kote Nchini, huku wakijishindia zawadi katika maduka ya kampuni hizo, kupitia Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyozinduliwa leo Jijini Mwanza na itakayoendelea hadi Oktoba 9.
Uzinduzi huo umefanyika Rock City Mall ambapo Viongozi mbalimbali wa chapa hizo wamesema kaulimbiu ya mwaka huu, 'The Extra Mile', inasisitiza wajibu wa kwenda hatua ya ziada katika kumhudumia Mteja, ikiwemo kumsikiliza, kumpa msaada kwa wakati na kutimiza ahadi anazopewa.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja wa Yas, Mwangaza Matotola, amesema timu za Yas na Mixx zitafika katika masoko makubwa Nchini kukutana na Wateja, kusikiliza maoni yao na kutatua changamoto zao papo hapo, Jijini Mwanza, timu hizo zitakuwa katika soko kuu la Mwanza.
Matotola ameahidi kuwa maoni na mrejesho wote wa Wateja utafanyiwa kazi, na Wateja watapewa taarifa za hatua zilizochukuliwa kupitia njia mbalimbali za mawasiliano za kampuni, changamoto zinazohitaji uchunguzi zaidi zitafuatiliwa hadi zipatiwe ufumbuzi.
"Tunapomsaidia mteja kupata suluhisho kwa wakati, maana yake tunawezesha mambo yake biashara yake, urahisi wa mawasiliano na familia yake au kukamilisha jambo lililokuwa limekwama," amesema Matotola. #MillardAyoUPDATES
Aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa LHRC, Dk Hellen Kijo-Bisimba, amefunguka kwa kina kuhusu hofu, utekaji, maumivu, uhuru wa kujieleza, vifo vya baada ya uchaguzi na Katiba mpya