"Baraka ulizopimiwa zinakutosha kwa wakati na mazingira uliyopo, ukizidishiwa zaidi ya uwezo wako kuzibeba, utaelemewa, zitakufanya uharibikiwe, ama utaishia kufanya kufuru. Zipokee na uwe na moyo wa shukrani. Mwenyezi Mungu anayetupimia ndiye anayejua stahili na kipimo chetu."
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Dkt.@SuluhuSamia leo Jumatano Agosti 30, 2023 amemteua Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini, Mhe. David Mwakiposa Kihenzile @DavidKihenzile kuwa Naibu Waziri wa Uchukuzi.
Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. @SuluhuSamia amemhamisha aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Mh Dkt Damas Ndumbaro Kwenda kuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. @SuluhuSamia, amemteua Dkt. @DBiteko kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati.
Katika nafasi ya Naibu Waziri Mkuu Mh Dkt Biteko atakuwa anashughulikia masuala ya uratibu wa shughuli za serikali.