@ayubu_madenge Madenge hamna kiongozi wa Africa hasa Maraisi anakuwaga na hotuba mbaya. Kama kweli alikuwa na dhamira hiyo tungeanza kuona juhudi zake kwa jirani zake.
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam DAWASA imetoa taarifa kwa wakazi wa Dar es Salaam na Pwani kuhusu upungufu wa huduma ya maji katika baadhi ya maeneo unaotokana na kushuka kwa uzalishaji wa maji katika mtambo wa Ruvu Chini.
Taarifa hiyo iliyotolewa Desemba 6 mwaka 2025 imeeleza kuwa maeneo yanayohudumiwa na mtambo wa Ruvu Chini yakiwemo Bagamoyo Tegeta Boko Mbezi Beach Mwenge Kinondoni Mwananyamala Masaki hadi Ilala yameathirika kutokana na kushuka kwa kina cha Mto Ruvu hali iliyosababishwa na kuchelewa kwa mvua.
Hata hivyo kwa upande wa mtambo wa Ruvu Juu unaohudumia maeneo ya Kibaha Kibamba Kimara Tabata Kinyerezi Pugu hadi Kisarawe hali ya uzalishaji inaendelea vizuri na huduma ya maji inapatikana kwa wananchi kama kawaida.
DAWASA imesema kuwa kwa kushirikiana na Wizara ya Maji jitihada mbalimbali zinaendelea kufanyika ikiwemo kusitisha matumizi ya maji ya Mto Ruvu kwa shughuli za kilimo na kuyaelekeza kwa matumizi ya binadamu pamoja na kuongeza matumizi ya visima ili kupunguza changamoto ya huduma.
Mamlaka hiyo imetoa wito kwa wananchi kuendelea kuhifadhi maji yanayopatikana kwa matumizi muhimu huku ikiomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na kusisitiza kuwa itaendelea kutoa taarifa za hali ya upatikanaji wa maji mara kwa mara ili kuwawezesha wananchi kupanga shughuli zao za kiuchumi kwa ufanisi.
@ze_mandevu Na wewe hujui kwanini panzi ana miguu mingapi au buibui, unajuwa maana ya classification, hadi leo hufahamu faida ya classification kwenye tafiti? Wake up jamani.
@fumbokhanJr Elimu yako ikusaidie na isaidie ndugu zako. Kwa miaka kumi wamefanikisha mradi mmoja wa kunufaisha watu 6k, sasa tuambie Kibaha ina wakazi wangapi, wangapi wanashida ya maji kwa pace hiyo ya watu wako unao shabikia itawachukua miaka mingapi kumaliza shida ya maji?
@fumbokhanJr Hospital ya kanda kwa karne hii mnajisifia X-ray na CT-scan unachekesha. Unajuwa bei zake ukalinganisha na yale ma V8? Kuna vitu nyamazeni, sio watanzania wote ni ng'ombe mzee.
Ndugu watanzania.
Jana kuna wenzetu waliumizwa na Polisi Mahakamani walipokuja kufuatilia kesi ya UHAINIya Mhe Lissu. Mmoja alivunjika mkono na wengine wana majeraha mwili mzima.
Wengi wenu mliomba utaratibu wa namna ya kuwasaidia wenzetu matibabu ikiwa ni pamoja na kuwatia Moyo.
Tafadhali, tunaomba mchangie kwa namba hii.
PAMOJA TUNAWEZA.