‼️AMKENI!! WAUAJI WAMEKWAMA JUMUIYA YA MADOLA (COMMONWEALTH)
Serikali haramu iliwakilishwa na Kombo mzanzibari huko mkutano wa dharura wa Mawaziri wa Commonwealth na alijieleza wee na mauongo yake! Ila si mnajua British style wakikushushua au kukunamga wanatumia lugha fulani unaweza kudhani wanakusifia 😅! Nadhani Kombo alijua ametoboa hadi maamuzi yalipofanyika na kutoka rasmi kwani Tanzania itaendelea kujadiliwa maana serikali IMESHINDWA kushughulika na yale maeneo manne waliyowekewa kama masharti na Commonwealth ikiwemo demokrasia, media nk
Wamewakumbusha maharamia hawa kuwa Katibu Mkuu anataka kufika nchini - yaani kimama kila saa anatafuta sababu! Kapewa pole ya msiba naona ndo Kombo atakuja kutangaza ka mafanikio 🙄
#JusticeForMO29 #Tanzania #SamiaMustGo
Tafsiri:
CMAG ilikumbushia masharti manne yaliyoainishwa katika Mkutano wake wa Sabini na Moja wa Desemba 2025 na matarajio ya muda yaliyowekwa katika Mkutano wake wa Sabini na Tatu wa Julai 2026. Ikitambua maendeleo katika maeneo fulani, CMAG ilisisitiza hitaji la kuongeza juhudi zaidi ili kuendeleza mchakato jumuishi na unaowezeshwa kwa uaminifu kati ya vyama; ulinzi wa uhuru wa kiraia, kisiasa na vyombo vya habari; mipango ya haki, ya wakati na ya uwazi katika kesi zilizosalia; na michakato inayoaminika ya uwajibikaji, na fidia inayofaa kwa wale walioathiriwa.
Watu wanaendelea kuchangia #ToneTone mpaka tufikie lengo.
TUENDELEE KUCHANGIA
M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ
NMB Bank
Namba ya Akaunti: 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Hii ni kama Movie sasa kuhusu wakina Angela Kizigha na familia yake nzima ya Mzee Charles Kizigha,mkongwe wa tasnia ya habari ya Bongo pale Daily Mews.SIKILIZA
1. _Bongolanderz_ wasiomjua Bi Angela Kizigha, huyu ni binti ya Mzee-Mzima Charles Kizigha, aliyekuwa Kigogo _Daily News_ enzi za Mwalimu.
2. Huenda Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, angekuwa amedanjishwa 1983 kama si Charles Kizigha!
3. Wahaini, akina Zacharia Hanspope na wenzie 19, walipanga kumdanjisha Bwana Julius Januari 9, 1983 kwenye kanisa la St Peter's, Oysterbay.
4. Mkiambiwa Pombe ina madhara kuliko faida, mkaage kwa kutulia. Miongoni mwa wahaini hao wakawa wanakodi taxi ambayo mara nyingi Charles Kizigha ndio alikuwa akiikodi pia.
5. Siku moja, taxi driver akamwambia Charles Kizigha "Kuna Mijamaa ina mbumba za kufa mtu nimeanza kuipeleka maeneo mbalimbali na huwa haibishi nikiitajia bei. Kila yakilewa yanamkosoa sana Rais Nyerere na kusema siku zake zimefika, sijui wana mpango gani".
6. Charles Kizigha akawezesha wahaini hao kunyakwa kama kuku wa mdondo! Walienda kukutania nyumba moja pale Kinondoni, mamwera wakawaingilia! Komandoo Tamimu akaruka ukuta akawa anakimbia kuelekea Kawawa rd. Akadandia pick up iliyokuwa na bia, akaanza kurushiana na mamwera ambao walimdanjisha!
Kwahiyo familia ya Angela Kizigha ni familia konki sana katika siasa za Tanzania,pamoja na hilo moja ambalo Mzee wa Atikali katukumbusha, lakini pia familia hii ina damu ya kiukombozi kwani waliweza kupambania Nchi ya Tanzania na Viongozi wake na ndio maana Maadam Angela Charles Kizigha amekuwa akiaminika "nyakati" zote kwa kuipambania Tanzania kama ilivyokuwa kwa wazazi wake,kwa wanaojua historia ya Tanzania yetu nadhani wanatikisa vichwa.
Sina shaka kuwa Makala hii fupi inaenda kuziba pengo la taarifa kwa wale wanaodhani kuwa Maadam Angela Kizigha ni mtu wa kuja tu ndani ya Taifa hili.
Msipende kuwachukulia poa poa watu msiwajua.