Kundi kubwa la watu wenye maambukizi ya UKIMWI ni vijana wa miaka 14-25 na maambukizi yameongezeka kwa asilimia 33.3.
Kwenye hilo kundi jipya wanawake ndo wanaongoza.
Umri huo bado ni wanafunzi wa shule, tuweni makini uko nje kwa moto.
Source: Itv News
Wasichana umri wa miaka 15- 24 wanaambukizwa sana UKIMWI, hali ni mbaya sana.
Kibaya zaidi wanaogopa Mimba kuliko UKIMWI, Wanasema ni kama Ugonjwa wa malaria tu
Wamezaliwa kipindi ambacho dawa za kufubaza Zipo wanauchukulia poa sana hivi Wangewaona wale waathirika wa zamani 🤔
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Prof. Palamagamba Kabudi, amesema Wasichana na Wanawake Vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24 ni miongoni mwa makundi yanayokabiliwa na changamoto ya maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI (VVU) nchini Tanzania.
Akizungumza leo, Novemba 19, 2026, na Waandishi wa Habari kuelekea maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani, Prof. Kabudi ametaja takwimu zinazoonesha kuwa kundi hilo linachangia asilimia 33.3 ya maambukizi mapya ya VVU nchini, huku akitaja pia asilimia 77.7 inayohusishwa na maambukizi mapya miongoni mwa Vijana wa Kike.
Takwimu hizo zinaonesha umuhimu wa kuendelea kuimarisha elimu ya kujikinga na VVU, huduma za upimaji na upatikanaji wa njia za kinga, hususan kwa Wasichana na Wanawake vijana, ili kupunguza maambukizi mapya nchini.
Kauli hiyo imetolewa wakati Tanzania ikijiandaa kuadhimisha Siku ya UKIMWI Duniani, inayofanyika kila mwaka Desemba Mosi, kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu VVU na UKIMWI na kuimarisha mapambano dhidi ya maambukizi mapya.
#MillardAyoUPDATES
Hatari ya ujinga si kutokujua, bali ni kuamini kwamba unajua kila kitu. Mtu anayefahamu mipaka ya maarifa yake bado ana nafasi ya kujifunza. Mtu anayejiona ameshafika mwisho wa maarifa amejifungia milango ya hekima. Falsafa huanza kwa swali, si kwa kujifanya kuwa na majibu yote.
Jenga mali kwa ajili ya maisha, lakini jenga watu kwa ajili ya vizazi. Kwa sababu siku moja nyumba utakayoijenga inaweza kubomoka, lakini mtu uliyemfundisha, uliyempenda, uliyemsaidia na kumuinua anaweza kuendeleza mema uliyoyaacha duniani.
Hakuna Mtu mwenye Wajibu wa kukusaidia, usimchukulie Poa
anayetoa kilicho chake kwaAjili yako.
Jifunze Kuthamini Hata Vitu vidogo unavyofanyiwa. Shukuru kwa Maneno, Heshimu kwa Vitendo na unapopata Nafasi, kuwa Msaada kwa wengine pia.
Thamini Watu kabla hujachelewa.
Watu tayari wana maumivu ya kutosha. Usiongeze mengine kwa maneno, dharau au matendo yako. Kuwa mtu ambaye uwepo wake unaleta faraja kwa wengine badala ya majeraha.