Kwa Nini Wakristo ni Wachache Israel?
Kitu cha kwanza kuelewa ni kwamba Yesu mwenyewe alikuwa Myahudi. Mitume wote kumi na wawili walikuwa Wayahudi, na hata waumini wa kwanza wa Kanisa walikuwa Wayahudi. Mwanzoni, Ukristo haukuonekana kama dini mpya, bali ulionekana kuwa kundi la Wayahudi waliodai kwamba Yesu ndiye Masihi aliyekuwa ameahidiwa katika Maandiko.
Tatizo lilianza pale viongozi wengi wa dini ya Kiyahudi walipokataa kumkubali Yesu. Walikuwa wakimtarajia Masihi ambaye angeikomboa Israel kisiasa kutoka chini ya Warumi na kuifanya kuwa ufalme wenye nguvu zaidi hata Zaidi ya Warumi. Badala yake, Yesu alihubiri toba, upendo, msamaha na Ufalme wa Mungu. Kwa wengi, huyo hakuwa Masihi waliyetarajia, kiufupi waliona kama ni utapeli na uongo.
Ndiyo maana Yesu alipingwa, akasalitiwa na hatimaye akasulubiwa. Hata baada ya kufufuka kwake, mitume waliendelea kupigwa, kufungwa gerezani na kuuawa kwa sababu ya kuhubiri kwamba Yesu ndiye Kristo.
Mwaka 70 BK, Warumi walipolivamia Yerusalemu, waliangamiza Hekalu la pili. Hekalu hilo lilikuwa kitovu cha maisha ya Wayahudi. Kuanzia hapo, Wayahudi wengi walitawanyika katika mataifa mbalimbali duniani. Tukio hili linajulikana kama Diaspora ya Wayahudi. Wakristo nao walikuwa tayari wameanza kuenea katika Siria, Asia Ndogo, Ugiriki, Roma na maeneo mengine kutokana na mateso.
Hapo ndipo jambo la kushangaza lilipotokea. Wakati idadi ya Wakristo ilianza kupungua katika nchi ya Israel, ilianza kuongezeka kwa kasi katika mataifa ya nje. Paulo aliihubiri Injili kwa watu wa mataifa (Wasio Wayahudi), na makanisa yakaanzishwa katika miji kama Antiokia, Efeso, Filipi, Korintho na Roma. Ndani ya karne chache tu, Ukristo ulikuwa umeenea sehemu kubwa ya Dola la Kirumi.
Karne ya nne BK ilileta mabadiliko makubwa. Mfalme Konstantino alikubali Ukristo, na baadaye Ukristo ukawa dini yenye nguvu katika Dola la Kirumi. Makanisa makubwa yakajengwa Yerusalemu na sehemu mbalimbali . Hata hivyo, hali hiyo haikudumu milele.maana
Mnamo mwaka 638 BK, majeshi ya Kiislamu yaliteka Yerusalemu. Tangu wakati huo, eneo hilo lilitawaliwa na falme mbalimbali za Kiislamu kwa karne nyingi. Wakristo waliendelea kuishi huko, lakini walikuwa wachache kuliko Waislamu na Wayahudi.
Karne ya ishirini ilipoanza, Wayahudi wengi kutoka Ulaya, Urusi, Afrika Kaskazini na Mashariki ya Kati walianza kurejea katika nchi yao ya kihistoria. Baada ya kuanzishwa kwa taifa la Israel mwaka 1948, uhamiaji huo uliongezeka sana. Ndiyo maana leo Wayahudi ndio Wenye idadi kubwa ya wakazi nchini Israel.
Cha kushangaza zaidi ni kwamba, ingawa Israel ina Wakristo wachache, nchi hiyo hupokea mamilioni ya Wakristo kila mwaka kutoka karibu kila kona ya dunia. Watu huenda kuona Bethlehemu, Nazareti, Mlima wa Mizeituni, Bustani ya Gethsemane na Yerusalemu, lakini wengi wao hurudi katika nchi zao baada ya kutembea.
Historia hii inafundisha kuwa mpango wa Mungu haukuwa kuifanya Injili ibaki Israel pekee. Mbegu ilipandwa Yerusalemu, lakini mavuno yalikuwa ya dunia nzima.
Yesu alisema:
"Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe." (Marko 16:15)
Leo, mataifa yaliyokuwa hayamjui Mungu katika Agano la Kale ndiyo yenye mamilioni ya Wakristo. Hii inaonyesha kwamba Mungu hana upendeleo wa taifa; anayemwamini Kristo kwa imani ndiye anayekuwa sehemu ya familia ya Mungu.
Huenda unaishi mbali na Israel na hujawahi kufika Yerusalemu. Lakini ukimpokea Kristo kwa moyo wako, unakuwa karibu na Mungu kuliko mtu anayekaa Yerusalemu bila kumwamini Yesu. Wokovu hautegemei jiografia, bali unategemea Imani. Asanteni
✍️✍️
Today 🤖🐐
✔️1. Bodo Glimt vs Lillestrom Sk - Over 1.5
✔️2. Rangers - Over 0.5
✔️3. Cork city - Win (1uP)
✔️4. Club Brugge - Win or lose
✔️5. Dinamo Zagreb - Win (1uP)
✔️6. Hammarby W- Win
✔️7. Nomme Utd vs Trans Narva - Over 1.5
✔️8. Czarni Sosnowiec W - Win (1uP)
✔️9. CSKA Moscow u19 - Win
✔️10. Kairaty Almaty - Win
Good luck
Jana niliona post ya mtu anasema kuhusu izi kebo kwamba hamna kitu, leo asubuhi naenda kutupa taka nakuta Kuna jirani katupa hapa. Binafsi naogopaga sana kitu cha umeme kinachouzwa bei ndogo.😀
Inaonekana wale Neema Gospel Choir wameinvest pesa nyingi sana kwenye kazi zao.
Maana gharama za vifaa vyao wanapofanya zile live concert ni mamilioni ya pesa
Still kwaya ina watu wengi sana ambao wanapaswa kuvaa sare mpya kila mara + make up na matumizi mengine.
I hope ndio uwekezaji mkubwa kwenye gospel upande wa matamasha ya live na wanaachia nyimbo kila mara🙌
Today Top 15 ⚽️🤖
✔️1. Gyori ETO FC - Win
✔️2. Ajax - Win
✔️3. FC Koper vs NSI Runavik - Over 1.5
✔️4. Benfica - Win
✔️5. HJK Helsinki - Over 0.5
✔️6. FC Vaduz - Over 0.5
✔️7. Partizan - Over 0.5
✔️8. Rigas Futbola Skola - Win
✔️9. Ludogorets - Win or lose
✔️10. Maccabi Tel Aviv - Win
✔️11. Ferencvaros vs Twente - Over 1.5
✔️12. PAOK vs Dynamo Kyiv - Over 1.5
✔️13. Dinamo Minsk - Over 0.5
✔️14. Nomme Kalju vs Shelbourne FC - Over 1.5
✔️15. FK Jablonec vs NK varazdin - Over 1.5
Good luck 🤌🏾