KINACHOENDELEA MAHAKAMA KUU YA DAR ES SALAAM MUDA HUU.
Muda huu saa sita mchana, Jengo zima la Mahakama umeme umezimwa, kuna giza nene kama tupo kuzimu halafu njee kuna mvua inaendelea kunyesha.
Msajili wa Mahakama hii, Lyakinana anawaogopa sana Magereza na hawa Mapolisi wa Kingai utadhani wao ndo wanamlipa mshahara, kwasababu Mapolisi ndio wanaamua nani akutane na Mwenyekiti Lissu na nani asikutane nae na yeye ndo aliyepewa order na Kingai kwamba azuie Mawakili wetu wasionane na Mhe. Lissu.
Sasa hivi wanapanga kupunguza viti ndani ya ukumbi Mahakamani ambao huwa tunautumia siku zote lengo likiwa ni kupunguza idadi ya watu watakao ingia ndani ili wasingizie kwamba ukumbi umejaa, kumbe wameondoa viti.
Mazingira hayo yanaonekana toka asubuhi muda ambao Mawakili walitakiwa kuingia kumuandaa shahidi wakishirikiana na Mh. Tundu Lissu.
Tunasubiri hiyo saa nane mchana tujue nini kimeendelea.
Taarifa kutoka vyanzo vyetu hapa Mahakamani vinasema Mwenyekiti Lissu amekutana kwa muda dakika 10 na Ramadhani Kingai na inaonekana kuna jambo halijaenda vizuri japo tunahisi huenda Mhe. Lissu atakuwa amemwambia hatuwezi kuendelea bila uwepo wa Mawakili wake, ambao wangesaidia kumchukua maelezo ya maandishi ya shahidi wake kabla hajaenda kutoa huo ushahidi Mahakamani.
Ukweli wa yote tutaujua baada ya masaa mawili kutoka sasa so tuwe na subira.
TUNDU LISSU: Siwezi kumuweka shahidi kizimbani kabla sijamuanda kwahiyo lazima nikutane nao na niwaelekeze cha kufanya ili wakija kugeuka hapo kizimbani basi niwashughulikie sawasawa. Siwezi kwenda ofisini kwao wala gerezani so nilazima tuonane na kupanga hapa hapa Mahakamani.🤣
Hapa ni Dar Tegeta Kibaoni wafanyabiashara wanatakiwa kutoka kwenye Maeneo yao haraka iwezekanavyo.
Kila mtu atafikiwa kwa wakati wake usijione upo salama, tuungane kupigania haki.
VIDEO:
Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Dkt. Charles Kitima, amebainisha kuwa demokrasia halisi katika nchi yoyote inasimikwa kwenye utawala wa sheria, uhuru wa mahakama, uhuru wa kitaaluma wa wasomi, na uhuru wa vyombo vya habari
Akizungumza leo, Septemba 15, 2026, mkoani Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya Siku ya Demokrasia Duniani yaliyoratibiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Padre Kitima ameeleza kusikitishwa kwake na kupungua kwa uhuru wa kitaaluma nchini, akibainisha kuwa tofauti na zamani ambapo jamii ilikuwa ikisikiliza na kupata miongozo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, siku hizi maprofesa na wasomi wamekuwa wakiwekwa ndani.
Akitahadharisha kuhusu athari za maisha ya hofu kwa ukuaji wa uchumi na ubunifu, Padre Kitima ameongeza kuwa nchi haiwezi kufikia uchumi unaotegemea maarifa iwapo wananchi na wasomi wanaishi kwa hofu, huku akisisitiza kuwa uhuru wa vyombo vya habari vya kijamii na vya kawaida ni nguzo nyingine kuu.
Haya ndio maumivu yetu, Ahsanteni mnayoyawakilisha kama yalivyo………
Ndio maana tunakuwa bongo tukiona waliolishwa asali wanatuambia tuwe na huruma na tuwe soft kwa waliotuua….
Tunataka accountability sio ku move on……..
HATUTAKI MARIDHIANO KABLA YA ACCOUNTABILITY, NA YOYOTE ATAKAETUPELEKA KWENYE MARIDHIANO KABLA YA DAMU ZA NDUGU ZETU KUPATA HAKI HUYO NI ADUI WA WATANGANYIKAA!!!!!!!!
HAKUNAAAAAAA!!!!!
"Akitokea mtu awe Mwanachadema au mpenda Demokrasia na Haki, akasaliti mapambano ya kutafuta Katiba Mpya ni sawa sawa na kusaliti damu za watu waliouawa kwa sababu ya kupigania #KatibaMpya na Demokrasia."-; Mhe. @jjmnyika
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo September 15, 2026
Last time tuliishia part 417 so leo tunaendelea na -;
Part 418
Majaji wameingia muda huu hapa Mahakamani na sauti ya high Courtttttttttt kali imepigwa na leo imepigwa tena na Mwanadada.
Anasimama Karani wa Mahakama kusoma namba ya kesi.
Anasimama wakili wa Serikali Ajuaye Zengeli akiwa na wenzake Katuga, Mrema, Ignas Mwinuka, Thawabu Issa, Mbiringe na Winniwa anasema wapo tayari kuendelea.
Mhe. Lissu nae anasema yupo tayari.
Shahidi namba 5 tayari yuko kizimbani
Jaji Ndunguru anamkumbusha Shahidi kwamba yupo chini ya kiapo.
Anasimama Katuga kwa ajili ya kuendelea na cross examination
Katuga: Shahidi habari ya asubuhi
Heche: Salama
Katuga: Ni ushahidi wako kwamba Mshtakiwa alisema na kuweka msimamo kwamba hatuko tayari kushiriki kwenye chaguzi za namna hii ambayo matokeo yake ni mauaji
Heche: Huo msimamo uliwekwa na Kamati Kuu ya Chama
Katuga: Ni sahihi kuwa msimamo ulikuwa kutokushiriki uchaguzi wa namna hiyo mpaka mabadiliko yafanyike?
Heche: Sahihi
Katuga: Uliiambia Mahakama hii kuwa Lissu alipokuwa akipita kwa wadau hakusema neno kuhamasisha uasi
Heche: Sahihi
Katuga: Kama kutakuwa na shahidi akasema kuwa Lissu alitumia neno uasi wakati anapita kwa wadau
Heche: Niulize ushahidi wangu nitakujibu usiniulize ushahidi wa mtu mwingine ila majibu yangu niliyotoa ndo sahihi.
Katuga: Ni ushahidi wako kwamba maneno tutahamasisha uasi na wewe kusema kuwa hakutumia neno tutahamasisha uasi
Heche: Inategemeana na context, Lissu alitumia maneno hayohayo inawezekana asitumie neno hilohilo ila context
Katuga: Katika ushahidi wako ulisema vyombo vya habari havitoi nafasi sawa
Heche: Sahihi
Katuga: Ulisema hii inatokana na mapungufu ya mfumo wa uchaguzi
Heche: Sahihi
Katuga: Katika ushahidi wako uliiambia Mahakama ni sheria ipi au mapungufu gani ya mfumo wa uchaguzi yanayopelekea upendeleo?
Heche: Nilieleza
Katuga: Ulieleza ni Sheria gani inayozuia waandishi au kuelekeza waandishi watoe habari za huyo na kuacha za yule?
Heche: Vyombo vya habari huwa vinafungiwa wakati wa uchaguzi, nchii hii imejaa impunity sheria hazifuatwi.
Katuga: Shahidi jibu swali au unataka nikubembeleze?
Heche: Kabembeleze mke wako
Katuga: Ni ushahidi wako kuwa mawakala wamekuwa wakipata usumbufu, procees inakuwa inacheleweshwa na kuzuiwa au kucheleweshewa viapo
Heche: Ni sahihi
Katuga: Ulitaja kuwa ni kituo fulani na kituo fulani?
Heche: Nilisema ni nchi nzima
Katuga: Unajua au hujui kuwa uliposhinda uchaguzi ulituhumiwa kuingiza kura feki mpaka ukashinda uchaguzi?
Heche: Hilo unaniambia wewe mimi sijui
Katuga: Unajua au hujui kuwa mwanasiasa akishindwa huwa hakubali kirahisi?
Heche: Sisi ni chama cha demokrasia ukishindwa unaenda nyumbani.
Katuga: Waambie majaji kama kweli wewe uliposhindwa ulienda nyumbani?
Heche: Uchaguzi haukuwa huru na haki
Katuga: Kwahiyo unaiambia mahakama hii kuwa ukishindwa ukaenda nyumbani inategemea na aina ya Uchaguzi?
Heche: Uchaguzi ni aina moja tu na Mahakama ilishasema uchaguzi usiokuwa huru na haki sio uchaguzi
Katuga: Uchaguzi wa 2015 ulioshinda uliukubali au uliukataa?
Heche: Niliukubali japo ulikuwa na makosa mengi.
Katuga: Jimboni kwako uchaguzi ulikuwa huru na haki?
Heche: Haukuwa huru na wa haki wagombea wa udiwani walienguliwa.
Katuga: Unajua mahakamani hatuwi kama makasuku?
Heche: Wewe ndio kasuku
Katuga: Ni sahihi kama uchaguzi wa jimboni kwako haukuwa na haki, ulikuwa na uhuru wa kutokukubali kutangazwa au kukubali kutangazwa?
Heche: Nililazimisha kutangazwa na uchaguzi haukuwa huru na haki na nchi hii haijawahi kuwa na uchaguzi huru na wa haki.
Katuga: Kama wewe ni mtu wa haki na sio pepepe ulikuwa na uwezo wa kukataa au kukubali kutangazwa??
Heche: Fafanua maana ya pepepe
Katuga: pepepe ni maneno ya mdomoni
Heche: Ok, sikuwa na uwezo wa kukataa kutangazwa maana wananchi walikuwa wananiunga mkono sana
Part 419 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
Kwa mnaouliza jina la hiyo Bank ambayo imetoa taarifa za Makam Mhe. @HecheJohn ni CRDB Bank yani hiyo ndo Bank pekee ambayo mtu yeyote anaweza kwenda kuomba taarifa za Bank account yako na wakamuuzia bila kujiuliza mara mbili sasa nyie endeleeni kuweka pesa zenu.
Mimi nilidhan CRDB inalalamikiwa tu kwenye swala la kuiba pesa za wateja wao, kumbe hadi taarifa za Wateja wanauza.🙌
‼️MAMBO KWA USHAHIDI‼️
Juzi @godbless_lema alisema Mhe. @HecheJohn alirudishiwa passport yake na Mkurungenzi wa Usalama wa Taifa.
Sasa huu ndo ushahidi wa namna ambavyo Heche alipata passport yake barua ya Kwanza ni ambayo Mwanasheria Mkuu wa Chama Dr Rugemeleza Nshala aliwaandikia Uhamiaji, barua ya pili ni majibu ya Uhamiaji.
Swali la kujiulizani ni kwanini Lema aliamua kumsingizia Kiongozi mwenzake jambo la uongo kubwa kiasi hiki halafu aliliweka public ili kila mtu asome lengo lake lilikuwa nini????
Tanzania inawazarendo kweli kweli huyu TESHA aliisha sema na sote tunaona kinachoendelea,
🫳utekaji 🫳udini 🫳matumizi mabaya ya ofisi
🫳mauaji🫳uzanzibar🫳matamko yasiyo ya staha
🫳ufisadi🫳 ubambikiaji kesi,
Miezi mitano iliyopita Dudubaya alituambia Wanachadema tuwe makini na Ishengoma ni kibaraka wa Abdul.
Sasa baada ya Abdul kuona kwamba ushahidi waliotoa Mahakamani kwenye kesi ya Uhaini dhidi ya Mhe. Lissu hautoshi kumtia hatiani Mhe. Lissu ndo kampa kazi huyu Ishengoma ili aje kusema Mhe. Lissu ndo aliwatuma kufanya uhaini.
Abdul ni zero brain ndo maana hata watu ambao anawatumia kwenye mambo yake ya kiwaki na wao hawana akili kama yeye.🚮🚮
Uzuri wa Lissu ndo huu,, ni msafi kuanzia sirini hadi hadharani...
Hapa Agenda kuu ni Katiba mpya, kumfuata gerezani usiku utadhani mnaenda kuwanga ameshawaambia mumkome😃...