#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 1
Mh. Lissu ameingia tayari akiwa na vibe kubwa sana.
Majaji pia wameingia.
Kesi hii itasikilizwa na majaji watatu wa Mahakama Kuu na wao pia wameshaingia.
Nitawapa majina ya hawa majaji watatu.
Wakatikati yuko bize kuandika hawa wawili wengine tunaangaliana nao uso kwa macho.
Kesi haijaitwa bado.
Jaji anateta kidogo na mwenzake. Anawasha kipauza sauti.
Anasimama kalani anasema Criminal case No. 19605/2025 Jamhuri dhidi ya Tundu Lissu.
Anasimama Nassoro Katuga wakili wa serikali tupo pamoja na
Job Mrema, Thawabu Issa, Mossie Kahima, Harrison Lukosi, Cathbert Mbiringi na Winiwa Kasala.
Hao ndio Mawakili saba wanaoiwakilisha Jamhuri mbele ya mahakama hii.
Mshitakiwa yupo naomba upande wa utetezi waweze kujitambulisha.
Anasimama mwanadada.
Anasema naitwa Neema Saruni ni Wakili. Mdada mrefu ananywele nyinginyingi.
Namuwakilisha mtuhumiwa aliyepo mbele ya mahakama hii tukufu.
Na kwa uwakilishi huo kwa mujibu wa PROBONO na nilipata wasaaa wa kuonana mteja wangu nikakutana nae.
Naomba mahakama impatie nafasi aweze kuelezea.
Watu wameshangaa ngoja tuone sasa.
Jaji anaandika kidogo.
Naambiwa kiutaratibu kesi kubwa watuhumiwa hupewa mawakili na mahakama.
Ngoja tuone.
Jaji anasema ngoja kwanza upande wa mshitaka waseme kesi imekuja kwa hatua gani.
Katuga anasema kesi ilikuja kwa ajili ya Preliminary hearing na sisi tuko tayari.
Kabla ya kuendelea na shauri hili Katuga anasema upande wa Jamhuri ulikuwa na Concern kadhaa kama tutapewa nafasi kuelezea.
Tuko tayari na plea taking na preliminary hearing.
Jaji anamwambia subiri kwanza.
Anaandika kidogo.
Amesimama Neema Saruni anasema tumemsikia Wakili wa Serikali Katuga lakini lipo suala la Uwakilishi wangu ikipendeza mteja apewe nafasi.
Jaji amesema sema wewe kwanza, niliwasiliana na mteja akasema atajiwakilisha mwenyewe, hayuko tayari nimuwakilishe.
Tulianza kushangaaa mbona anasimama wakili ambae hatumfahamu wakati Akina Mzee Mpoki wapo.
Anaanza Mh. Lissu kusema anasema nawashukuru Majaji kwa kunipatia Mawakili.
Pamoja na kwamba mimi sikumuomba na simfahamu wakili Neema Saruni alikuja mwenyewe kuniona kwenye gereza la Ukonga alijitambulisha na kuniambia yeye ndio amepewa hilo jukumu.
Nilifurahi kwa yeye kufanya hivyo. Walifanya vizuri sana.
Sasa Mh. Jaji alivyokuja na kunieleza nilimjulisha kuwa kwenye kesi kubwa kama hii ambayo ni kosa kubwa kuliko yote kwa mujibu wa ibara ya 28.
Kwenye kosa linaloshitakiwa kwa kusema maneno.
Kosa la aina hii nitajitetea Mwenyewe.
Kwasababu inabidi tuambiwe na nchi hii ukisema maneno yasiyowapendeza watu fulani fulani unaweza kuhukumiwa kifo.
Kwasababu hiyo nikasema nitajitetea mwenyewe.
Part 2 itaendele kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako kwenye tweet hii.
@iJimmy38@udsm_icon Kuna namna ya ku block ads,unaingia kokote bila premium subscription na ads hazichungulii,iwe boom play,audiomark, na website zote unazozjua wewe
@ZagyGirl Wazilaum billion zao bn,kila siku vikamera site,uwanja uko shwari na porojo nyingiiiiiii,ifike muda tuache siasa,pia haiwez kuwa quality ndan ya week 3,personally I expected this