Mwaka 2025 nikipokea gawio na michango kutoka taasisi na mashirika ya umma nilitoa maelekezo ya uboreshaji zaidi. Nina furaha kuona maelekezo hayo yamefanyiwa kazi, na gawio la serikali mwaka 2026 limeongezeka kwa asilimia 30, kufikia shilingi trilioni 1.32. Siku ya Gawio si siku ya kusherehekea mafanikio ya kifedha pekee, bali ni fursa ya kutathmini maeneo yanayohitaji uboreshaji zaidi ili mafanikio tuliyoyapata yaendelee.
Mafanikio hayo ni uthibitisho kuwa, taasisi na mashirika ya umma yanaweza kutoa huduma na kuwa sehemu ya ujenzi wa uchumi wa taifa letu. Tunapoelekea kuanza utekelezaji Dira ya Taifa 2050, ni muhimu tufahamu kuwa hatutaweza kujenga uchumi shindani kwa taasisi zinazofanya kazi kwa mazoea, ni lazima tujipime kwa matokeo, na si takwimu. Haya ndiyo maono na mwelekeo wa taifa letu.
Pamoja na hayo, ninazipongeza taasisi na mashirika yote yaliyotoa gawio kwani hii ni sehemu ya lengo letu la kuongeza mapato ya ndani katika kugharamia shughuli za maendeleo. Hata hivyo, pongezi hizi zisiwe sababu ya kuridhika na kubweteka, kwani hatutasita kuchukua hatua tunapobaini uzembe na matumizi mabaya ya rasilimali za umma.
Ninaipongeza Klabu ya Yanga kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa mara ya tano mfululizo. Mafanikio haya ni ushahidi wa juhudi, nidhamu na kujituma kwa wachezaji, benchi la ufundi, uongozi pamoja na mashabiki.
Aidha, ninazipongeza klabu zote zilizoshiriki Ligi Kuu msimu huu kwa ushindani mzuri uliofanya mchezo wa mpira wa miguu nchini Tanzania kuendelea kukua, kuvutia na kuongeza hamasa kwa mashabiki pamoja na wadau wa mchezo huu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akutana na kufanya mazungumzo na Mfanyabiashara kutoka nchini Nigeria ambaye pia ni Mwanzilishi na Mmiliki wa Dangote Group, Alhaji Aliko Dangote pamoja na Ujumbe wake, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 28 Juni, 2026.
Leo nimepata heshima ya kufunga Mafunzo ya Uongozi Ngazi ya Juu Kozi Namba 28 na Uongozi Daraja la Pili Kozi Namba 48 kwa Mwaka 2025/26 katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania (TCT) cha Jeshi la Magereza jijini Dar es Salaam, ambapo wanafunzi 657 wamehitimu.
Jeshi la Magereza lina nafasi muhimu katika mfumo wa haki jinai nchini. Hivyo, pamoja na kuwapongeza wahitimu, nimewasihi kuwa maarifa waliyoyapata yawe nyenzo ya mabadiliko ya kiutendaji, mathalan katika urekebishaji tabia za wafungwa, na uboreshaji taswira ya jeshi hilo, sawa sawa na mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai na maelekezo ya Dira 2050.
Ili kuhakikisha wafungwa wanaoachiwa hawarudi magerezani, serikali itaweka utaratibu wa kuwapatia mitaji ili watumie ujuzi wanaoupata magerezani kujiendeleza. Aidha, nimelielekeza Jeshi la Magereza kuwa na mfumo wa TEHAMA utakaowezesha kuwafuatilia na kuwafanyia tathmini wafungwa walioachiwa, kujua walipo na shughuli wanazofanya.
Nawatakia Watanzania wote Heri ya Miaka 62 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Tuendelee kuuenzi na kuudumisha Muungano wetu ili kujenga Tanzania moja, imara na yenye ustawi kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Novemba 14, 2025 nikifungua Bunge la 13 niliahidi tutaimarisha uvuvi wa Bahari Kuu na kukuza uchumi wa buluu. Leo ninafuraha kuwa tumetekeleza hilo kwa kupata meli ya kwanza ya uvuvi wa Bahari Kuu ambayo nimeizindua mkoani Dar es Salaam. Meli hii itaongeza uzalishaji wa samaki wa Bahari Kuu, itatoa ajira, itakuza sekta ya uvuvi na mchango wake katika Pato la Taifa (GDP).
Uwepo wa meli hii utatuwezesha kunufaika na uvuvi wa Bahari Kuu ambao kwa miaka mingi umefanywa na meli na kampuni kutoka nje ya nchi. Kwa kutambua kuwa takribani wananchi milioni 6 wanategemea sekta hii, tumeboresha mazingira ya uvuvi kwenye maziwa kwa kuwezesha upatikanaji wa mitaji, utaalamu, vifaa na miundombinu. Aidha, tumejipanga kujenga bandari ya uvuvi Bagamoyo, baada ya ile ya Kilwa, kununua meli nne za uvuvi na moja ya mafunzo na boti za doria.
Ili tufanikishe malengo yetu nimesisitiza:
1. Tuendelee kudumisha amani na usalama
2. Nimeielekeza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kutunza mitambo tunayoinunua, na iwawezeshe wavuvi wadogo kwa masoko, vifaa, mitaji na elimu ya ujasiriamali na utunzaji fedha. Pia idhibiti uvuvi haramu na iimarishe ushiriki wa sekta binafsi kwenye uvuvi.
Ikulu, Dar es Salaam, Aprili 23, 2026
Hotuba yangu leo nilipopokea ripoti ya Tume niliyoiunda kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025.
Tupoendelea kushughulikia na kuyapatia majawabu yaliyotokea, ninawasihi tuongozwe na maneno haya kutoka katika vitabu vitakatifu:
2 Mambo ya Nyakati 7:14
“Ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekeza, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi zao, na kuiponya nchi yao.”
Surah Al-A'raf (7), Aya ya 23
"Mola wetu Mlezi! Tumejidhulumu nafsi zetu, na usipotusamehe na kuturehemu, hakika tutakuwa miongoni mwa waliopata hasara.”
Mungu Ibariki Tanzania.
Nchi yetu imepata heshima ya kuwa mwenyeji wa kwanza barani Afrika wa Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Shirikisho la Jumuiya ya Madaktari wa Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu (WFNS) ambao leo nimeufungua jijini Dar es Salaam. Uamuzi huu unadhihirisha imani kubwa katika maendeleo yetu na utayari wetu katika kuimarisha zaidi huduma za afya, hususan huduma za kibingwa na ubingwa bobezi.
Matokeo ya kazi kubwa tuliyofanya katika miaka mitano iliyopita katika huduma za afya za kibingwa na ubingwa bobezi yanaonekana ambapo;-
1. Hospitali zinazofanya upasuaji wa kibingwa wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu zimeongezeka kutoka 2 hadi 7.
2. Madaktari bingwa wa upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu wameongezeka kutoka 12 hadi 37.
3. Tumeongeza kwa kiasi kikubwa vifaa muhimu kama MRI, CT-Scan na X-ray.
Uwekezaji huu umeifanya Tanzania kuwa moja ya nchi chache Afrika zenye uwezo mkubwa wa kufanya upasuaji huo, na sasa inahudumia wagonjwa kutoka nje ya nchi.
Ninashukuru Chama cha Madaktari wa Upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya Fahamu Tanzania kwa tuzo mliyonipa, hakika, hii ni heshima yetu sote. Serikali yetu itaendelea kushirikiana na taasisi za kikanda na kimataifa kuimarisha huduma za afya kwa kuzifanya kuwa bora, nafuu na za uhakika ili kuokoa maisha ya wananchi na kurejesha tumaini kwa jamii.
Baada ya miaka 35, tumelazimika kufanya tena tathmini ya mfumo wa kodi nchini ambapo leo nimepokea ripoti ya Tume ya Rais ya Kutathmini Maboresho ya Mfumo wa Kodi Nchini niliyoiunda Julai 2024. Tume imewasilisha mapendekezo 284 yanayolenga kuboresha mfumo wa kodi ili uendane na mabadiliko ya kiuchumi, kiuwekezaji na kibiashara duniani.
Maboresho ndiyo maendeleo. Kwa muktadha huo, tumechukua hatua hii kwa malengo makuu mawili; kwanza, kupanua wigo wa walipakodi, ili kila mwananchi ashiriki kujenga uchumi wa nchi yetu, na pili, kutambua kuwa mfumo bora wa kodi ni muhimu katika kujenga uchumi imara, jumuishi na shindani, sawa na malengo ya Dira 2050.
Ninawashukuru wananchi wote kwa kutoa maoni kwani mmeshiriki kuamua hatma ya leo na kesho yetu na Taifa letu. Aidha, katika utekelezaji wa mapendekezo hayo, tutashirikiana kikamilifu na sekta binafsi, wananchi na wadau wengine ili tufanikishe lengo la ukusanyaji rasilimali zinazohitajika kwa ustawi wa watu na maendeleo ya nchi yetu.
Ninawapongeza na kuwatakia kheri wanawake wote katika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake. Siku hii inatupa fursa ya kipekee ya kutambua, kujivunia na kusherehekea mafanikio tuliyopata, hasa katika elimu, afya, uchumi na uongozi.
Siku hii inatukumbusha pia wajibu wetu wa msingi kwa waasisi wetu na kwa vizazi vya sasa na vijavyo; wa kuendelea kupanga na kutekeleza mipango ya kumwezesha mwanamke, ikiwa ni sehemu muhimu ya kazi ya kukomboa familia, jamii na Taifa kwa ujumla.
Karibu Tanzania Mheshimiwa Rais.
Ikulu, Dar es Salaam leo nimempokea Kaka yangu, Rais wa Jamhuri ya Uganda, Mheshimiwa Yoweri Kaguta Museveni. Ziara yake hii nchini ikiwa ni siku chache tu baada ya Uchaguzi Mkuu wa Uganda inaonesha namna Uganda inavyothamini ushirikiano wake na nchi yetu, ambao umejengwa katika misingi ya udugu, ujirani na kuheshimiana.
Tumejadili maendeleo ya Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP). Mradi huu ambao ni moja ya vielelezo vya uhusiano wetu, unatarajiwa kuanza kufanya kazi Julai mwaka huu. Vilevile, tumejadili mpango wa kuunganisha reli (SGR), ujenzi wa mabomba ya kusafirisha gesi asilia na mafuta, kukuza matumizi ya bandari za Tanzania, ulinzi na usalama, pamoja na namna bora ya kukuza biashara baina ya nchi zetu kwa kuondoa vikwazo visivyo vya kikodi.
.
PRAY ...… Like Nehemiah
BUILD ..... Like Noah
LEAD ....... Like Moses
FAITH …… Like Abraham
OBEY ....…. Like Daniel
FIGHT ....... Like David
SERVE ....… Like Martha
BELIEVE ..... Like Mary
EDUCATE … Like Paul
LOVE ..……….. Like JESUS
Can I get an “AMEN” ???
.
Asubuhi ya Oct 29, 2025, mitaani kulikuwa kweupe kabisa bila waandamanaji. Amani ikiwa imetawala.
Ghafla from nowhere, kila sehemu ikalipuka!
Hali hiyo ikawapa hamasa wananchi waliotamani maandamano nao kuingia mitaani wakijua kumbe kweli inawezekana
Kikanuka kweli kweli
Hawa watu wa kwanza kuingia mitaani ni kina nani?
𝐀 𝐏𝐑𝐄𝐋𝐔𝐃𝐄
Tarehe 26 February , 2021, katikati ya dhoruba la kufiwa viongozi wake waandamizi, rais Magufuli anamteua Bashiru Ally kuwa Katibu mkuu kiongozi, kufuatia kifo cha John Kijazi
Rais wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Dkt. Mwigulu Nchemba kuwa Waziri Mkuu. Jina la Mbunge huyo wa Iramba Magharibi limewasilishwa Bungeni na Mpambe wa Rais (ADC) Brigedia Jenerali Nyamburi Mashauri kwa ajili ya Bunge kumthibitisha kuwa Waziri Mkuu.
Watumishi wa Umma na Watanzania lazima tuwe tayari, lazima twende kwa gia ya kupandia Mlima-Waziri Mkuu Mteule Dkt. @mwigulunchemba1
📍Dodoma-Tanzania
🗓️Novemba 13, 2025