TANZIA
Mchoraji wa katuni mashuhuri, King Kinya, amefariki dunia leo, na mwili wake unatarajiwa kuzikwa Septemba 18, 2026 katika Makaburi ya Mwananyamala.
King Kinya alijulikana kwa katuni zake zilizotumia ucheshi na vijembe kuzungumzia masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.
The Citizen editorial cartoonist King Kinya, has died.
He was renowned for his bold, thought-provoking cartoons, which used humour & satire to examine political, economic & social issues.
His work often challenged those in authority and stimulated public debate.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan atakuwa Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma siku ya Jumanne tarehe 8 Septemba, 2026.
Mheshimiwa Prof. Palamagamba Kabudi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu akizungumza na Waandishi wa Habari kutoa taarifa ya tukio hili kubwa na la kihistoria kwa Tanzania.
Pro. Chachage alikerwa vyuo vikuu kushushwa hadhi kuwa kama shule za sekondari, anasema Dkt. Kamata
Ameyasema haya kwenye mhadhara uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Agosti 14, 2026 katika kumbukizi ya miaka 20 tangu kifo cha mwanazuoni nguli wa Tanzania Prof, Chachage S. Chachage.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa pamoja na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Dkt. Sidi Ould Tah kuashiria ufunguzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka, Awamu ya Pili (BRT II) unaohusisha Barabara ya Kilwa, Chang’ombe, Sokoine na Kawawa, Jijini Dar es Salaam, tarehe 07 Agosti, 2026.
𝐇𝐎𝐍𝐆𝐄𝐑𝐀 𝐊𝐖𝐀 𝐕𝐈𝐎𝐍𝐆𝐎𝐙𝐈 𝐖𝐀𝐋𝐈𝐎𝐏𝐀𝐓𝐀 𝐔𝐓𝐄𝐔𝐙𝐈!
Tunawapongeza viongozi wote waliopata uteuzi wa kuendelea kukitumikia Chama na Taifa. Tunawatakia kila la kheri mnapoendelea kutekeleza majukumu yenu kwa uadilifu, uzalendo na kujituma kwa maslahi ya wananchi.
Tembelea: https://t.co/XFsl2Qg9M9
_______
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#CCMIpoKazini
#CCM
📸 𝐏𝐈𝐂𝐇𝐀: Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao Maalum cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kilichofanyika Zanzibar,Leo Jumatano tarehe 29 Julai, 2026.
Kikao hicho kilijadili masuala muhimu ya Chama na Taifa, pamoja na kuimarisha utekelezaji wa maamuzi na Ilani ya CCM kwa maendeleo ya wananchi.
Tembelea: https://t.co/XFsl2Qg9M9
_________
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#CCMIpoKazini
Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoani Arusha, Saipulan Ramsey amesema uchawa ni jambo ambalo linaharibu taifa, hivyo viongozi wajifunze kuwa na watu wanaojitambua.
A traditional technique used by young shepherds of Ethiopia's Banna tribe. They use stilts to watch over their livestock and avoid snakes and predators like lions and leopards.
Sekta ya Kilimo pale Uholanzi, nchi yenye raia 19,000,000 waliojazana kwenye eneo sawa na mkoa wa Dodoma huku ardhi yake ikiwa imeathiriwa kwa kiasi kikubwa na chumvi ya bahari, inagenerate mapato ya dola Bilion $200+ kwa mwaka, sawa na bajeti ya Tanzania kwa miaka 15. Wanawezaje halafu sisi tunashindwa?
Mapato ya Uholanzi yaliyotokana uuzwaji wa bidhaa za maziwa, mayai, na nyama mwaka 2022 ni dola billion $23, sawa na bajeti ya Tanzania ya mwaka 2026/27. Wanawezaje halafu sisi tunashindwa?
Mapato yote haya ya matrilioni ya fedha yanazalishwa na raia laki mbili tu ambao wanajishughulisha na kilimo, sawa na 2% ya labor force ya Uholanzi.
Waholanzi laki mbili tu wanatumia kilimo kutengeneza zaidi ya shilingi trillion 525 za kitanzania kwa mwaka mmoja tu.
Wakati huo huo, WATANZANIA zaidi ya milioni 20, sawa na asilimia 63% ya labor force, wanaojihusisha na kilimo mwaka jana 2025 waliingiza mapato ya dola billion 3.8 tu kwa shughuli zao zote, sawa na robo ya pesa waliozalisha Waholanzi kwa kuuza mayai tu mwaka 2022. Why??????
Kwa nini watanzania wenye ardhi yenye rutuba zaidi ya hekta millioni 44 tushindwe kuzalisha hata kijifraction tu cha mapato ya kijinchi chenye hekta milioni moja zilizojaa chumvi ya bahari????
Ukitafakari vizuri utagundua “TATIZO NI WANAHARAKATI waliokosa uzalendo.”
MWENYEKITI MPYA WA KAMATI YA OLIMPIKI TANZANIA (TOC)
SOMO KUTOKA IOC: UHALALI WA UCHAGUZI HAUPASWI KUVURUGWA
Sehemu ya 1 kati ya 3
Pongezi za dhati kwa Mhe. Anthony Mtaka kwa kutambuliwa rasmi na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) kuwa Rais halali wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC). Pongezi pia zimwendee Makamu wa Rais na wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji kwa kusimama imara kutetea uamuzi wa Mkutano Mkuu. Tukio hili limetufundisha somo muhimu: demokrasia haiishii kwenye kupiga kura; hukamilika kwa kuheshimu matokeo ya kura.
Na kwa wale wote waliohusika katika mchakato huu, ushauri wangu ni mmoja tu: tuheshimu uamuzi wa IOC bila mabishano. Uamuzi huo haukutolewa kwa bahati mbaya. Ulifanywa baada ya mwangalizi huru wa IOC na ANOCA kushuhudia uchaguzi, na baada ya IOC kupokea taarifa kutoka vyanzo mbalimbali. Tukio hili ni onyo kwamba tabia ya kuamini matokeo yanaweza "kurekebishwa" baada ya kura kupigwa inaweza kuiweka Tanzania katika hatari ya kupoteza heshima yake mbele ya jumuiya ya kimataifa.
Hatari hiyo si ya viongozi pekee. Waathirika wakubwa wangekuwa vijana wetu wanaojitahidi usiku na mchana kuipeperusha bendera ya Tanzania katika Michezo ya Olimpiki ya Los Angeles 2028 na mashindano mengine ya kimataifa.
IOC si taasisi inayoyumba katika masuala ya utawala bora. Katika historia yake imewahi kusimamisha Kamati za Olimpiki za Mataifa mbalimbali pale ambapo uhuru wa Kamati hizo ulipoingiliwa au taratibu za uchaguzi kuvurugwa. India ilisimamishwa baada ya sheria za serikali kukinzana na Hati ya Olimpiki. Kuwait ilisimamishwa kutokana na kuingiliwa kwa uhuru wa utawala wa michezo. Guatemala ilisimamishwa kufuatia kuingiliwa na serikali na mahakama. Hivi karibuni Iraq ilisimamishwa baada ya serikali kuivunja Kamati halali ya Olimpiki na kuunda nyingine chini ya Waziri wa Michezo.
Methali ya Kiswahili inasema: "Ukiona mwenzako ananyolewa, zako tia maji." Tusifike huko.
Kusimamishwa kwa Kamati ya Olimpiki ya Taifa si adhabu kwa viongozi pekee; ni pigo kwa taifa zima.
Madhara yake ni makubwa:
Wanamichezo wanaweza kushindwa kushiriki Olimpiki chini ya bendera ya Tanzania au wakaruhusiwa kushiriki kama wanamichezo wasio na taifa (neutral athletes).
Fedha za Olympic Solidarity zinazofadhili mafunzo ya wanamichezo, makocha, vifaa, tiba ya michezo na ufadhili wa masomo husimamishwa.
Vijana hupoteza fursa za mafunzo na mashindano ya kimataifa.
Programu za kukuza vipaji hudhoofika.
Wadhamini wa sekta binafsi hupunguza uwekezaji kutokana na kupungua kwa hadhi ya nchi.
Taswira ya Tanzania katika jumuiya ya kimataifa hudhoofika.
Kwa kifupi, viongozi wanaweza kubadilishwa; lakini ndoto za wanamichezo zikivunjika huchukua miaka mingi kujengwa upya.
Leo hii kuna mwanariadha anayefanya mazoezi kila alfajiri akitumaini kufuzu Los Angeles 2028. Kuna mwogeleaji anayesaka ufadhili kupitia Olympic Solidarity. Kuna bondia anayehitaji mashindano ya kimataifa kujenga kiwango chake. Kuna mwanafunzi wa sekondari anayeota siku moja kuivaa jezi ya Timu ya Olimpiki ya Tanzania.
Ndoto zao hazipaswi kuvurugwa na makosa ya kiutawala ambayo hayawahusu.
Katika barua yake ya tarehe 9 Julai 2026, IOC ilitambua rasmi viongozi waliochaguliwa na Mkutano Mkuu wa TOC. Wakati huohuo ilieleza wasiwasi wake kuhusu kile ilichokiita jaribio la dakika za mwisho la kubadilisha matokeo ya uchaguzi wa Rais kwa kutangaza mgombea ambaye hakuchaguliwa. IOC ilieleza kuwa kitendo hicho kilikiuka Hati ya Olimpiki, Katiba ya TOC na misingi ya maadili ya Harakati za Olimpiki, na ikaagiza uchunguzi pamoja na hatua stahiki dhidi ya waliohusika.
�
TAN - NOC Elective General Assembly held on 5 July 2026 - IOC-ANOCA letter to NOC - 9 July 2026.pdf
Itaendelea...