Nimeona matusi na sintofahamu nyingi mtandaoni baada ya kuchapisha ujumbe wa kutoa pole kwa Mama Samia, hasa niliponukuu salamu za pole za Mwenyekiti Lissu kutoka gerezani.
Kwa sisi jamii tunaodai kupigania uhuru wa maoni na demokrasia, hili linapaswa kutufikirisha. Kutofautiana kwa hoja hakuhitaji matusi, dhihaka wala chuki.
Lissu amekaa gerezani takribani mwaka mmoja na miezi sita, akikabiliwa na kesi ambayo sisi tunaamini ni ya kisiasa na isiyo na haki. Anafahamu yaliyompata na serikali iliyomweka mahabusu. Lakini alipofahamishwa kuhusu msiba wa mume wa Mama Samia, akiwa mbele ya mahakama, alitoa salamu zake za pole kwa wafiwa mara mbili.
Huu si unyonge. Hii ni hekima, utu na ukomavu wa kiwango cha juu.
Na si mara ya kwanza. Aliwahi pia kumtetea Sabaya katika kesi yake Moshi. Wengi tulishangaa, nami nilishangaa. Lakini nilipomuuliza baadaye, nilielewa kwamba kwake haki haichagui upande.
Hilo ndilo fundisho kubwa tunalopaswa kulibeba. Tunaweza kupinga serikali, kudai haki na kupigania demokrasia bila kujenga harakati zetu juu ya chuki na kisasi.
Lakini kama tunasema tunampenda Lissu, basi pale anaposema ana pumzi ya kuvumilia mateso na kukaa gerezani, sisi tunapaswa kuchukua kauli hiyo kama mwito wa ujasiri, si ruhusa ya kukaa kimya.
Kama tunaamini kesi hii si ya haki, basi viongozi tunanapaswa kuwaongoza wananchi katika hatua za amani, kisheria na kidemokrasia za kudai haki, pengine kwa njia ya maandamano. Sio kwenye keyboard tu na microphone.
Demokrasia inahitaji wananchi wanaothubutu kusimama kwa kile wanachoamini. Na kama siku moja tutapata nafasi ya kuongoza nchi hii, tusije tukarudia makosa tunayoyapinga leo. Lazima tutawala kwa haki, utu na dhamira njema.
Mimi nitasimama kwenye upendo, utu na haki siku zote ktk kazi hii. Anyway , hekima ya Lissu kutoa pole kwa Mama Samia was a top-class thinking. Inaonyesha kwamba hata unapoteseka, unaweza kuchagua utu, hata unapopinga, unaweza kukataa kisasi.
Wakati mwingine Mungu hataki umshinde adui yako kwa chuki, bali kwa upendo, hekima na maisha yenye ushuhuda kwamba uovu wake haukukushinda.
Mimi niko tayari kusimama kwa amani na kwa ujasiri. Katika hatua ya kupigania uhuru wa Lissu kuwa nje ya kuta za gereza na sio kusema ana pumzi ya kukaa jela hata maisha. Tuna watu wengi sana Chama hiki , pumzi yetu itoke mtandaoni , fikeni tu hata mahakamani kwa sasa na huku viongozi wakuu watusaidie kutafakari jambo muhimu la haki , sheria na amani.
โYou donโt have to hate those who hurt you. Sometimes the greatest revenge is to rise above them with peace, dignity, and success.โ
Thank you !!
Ukiniuliza mimi, nitakwambia game ya chadema vs wanaharakati iko so tricky and kindโf complicated.
Kuna mmoja hapo anakuwa driven na hisia kuliko uhalisia wa siasa.
Chadema ni chama cha siasa, lengo lake kuu ni kushika dola, agenda yake kuu ni kupinga,kukosoa na kushauri serikali (chama tawala)
Kwenye hizo agenda kuu sasa ndo kuna tricky hapo, chadema inampasa kujiuza kwa wapiga kura kwa kuwaambia kuwa sisi hatuko hivo kama wao watawala na tukishika dola hatutayafanya haya na yale wanayofanya hawa watawala!!
Hatutaua, kwaio inabidi wasiue hata sasa.
Hatutaiba, inabidi wasiibe hata sasa.
Hatutafurahia tukiona binadamu amekufa au ameuliwa hata akiwa ni adui!! Na inabidi waanze kuonyesha hayo sasa.
Adui akifa au akifiwa tutaenda kuzika na tutaenda kuhani msibani!!
Yote haya ni ili chadema asionekane yeye naye ni roho mbaya tu kama alioko kwenye kiti!!
Kwahiyo chadema unakuta ana jukumu la kumpenda hadi adui ili kuonyesha watu kuwa sisi hatuko hivyo.
Otherwise mpiga kura ataona aaah mtawala wa sasa ni mkatili, lakini mbona hata huyu chadema nayeye anaonekana ni mkatili kabla hata hajashika dola!!๐ค Huyu akishika dola si ndio atakuwa katili zaidi ya wa sasa!!
Finally mtu anaamua bora shetani wa zamani niliemzoea kuliko shetani mpya!!
But kwa wanaharakati sasa ni tofautiโฆ. hisia zinawapush wawe na mentality ya ngadu kwa ngadu,
๐ฆท kwa ๐ฆท, mwaga bapa namwaga kichanganyio!!
Anayekuua na kukuteka na kukutesa, siku nayeye akifa angusha party kihomeboy shangilia!!
Its very complicated hii game!!
Ndo yale yale nasemaga, kama unamkosoa kiongozi wa chadema kwenye comment then akakublock means huyo siku akiwa tu DC ukakosoa anakutia ndichi masaa 72!!
Ni lazima anayempinga mtawala asiwe na characters za mtawala!!
Sijui kama niko sahihi au nimeamka na wenge!!