EDWIN MTEI: MJENZI WA NCHI, KIONGOZI WA MFANO
Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe na wanafamilia wa marehemu Edwin Mtei,
Viongozi, wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Ndugu wananchi, waombolezaji, mabibi na mabwana;
Nimepokea taarifa za kifo cha Mwenyekiti Mwanzilishi na Mwasisi wa Chama chetu, marehemu Edwin Isaac Mbiliewi Mtei kwa masikitiko makubwa. Katika hili nafikiri sitakosea nikisema kwamba siko peke yangu. Hata hivyo, naombeni mniruhusu niwape pole nyingi watoto, wajukuu, ndugu na wanafamilia wa marehemu Mzee Mtei. Salamu hizi za rambirambi zinawahusu pia viongozi, wanachama na wafuasi wote wa CHADEMA popote walipo katika nchi yetu na nje ya nchi. Aidha, Mzee Mtei alisimama katika mstari wa mbele kabisa katika harakati za ujenzi wa nchi yetu; kwa sababu hiyo, salamu hizi ziwafikie pia wananchi wote wa Tanzania katika ujumla wao.
Maandiko Matakatifu yanatufundisha katika Zaburi 90:10, kwamba “miaka ya kuishi ni sabini, au tukiwa wenye afya, themanini…” Mwenyezi Mungu alimbariki marehemu Mzee Mtei kwa kumpa ziada ya miaka ishirini na nne (24) katika gawio lake la kawaida la miaka ya hapa duniani; na alimzidishia miaka kumi na minne katika nyongeza yake ya miaka kumi kwa wenye afya.
W.E.B Dubois, kiongozi wa harakati za ukombozi wa Waafrika duniani, aliandika katika kusherehekea miaka tisini ya kuzaliwa kwake kwamba “…kama kuishi hakukupi thamani, busara na maana ya maisha, basi hakuna sababu yoyote ile ya kuishi.”
Miaka tisini na nne (94) ya maisha ya marehemu Mzee Mtei yalitupa thamani kubwa, yalijaa busara tele na yalikuwa na maana kubwa. Naomba nikope maneno ya Amiri bin Sudi, au kwa jina lake maarufu ‘Andanenga’, mtenzi na mshairi maarufu wa Kiswahili, pale aliposema: Mzee Mtei …. “alisheheni sifa nyingi sana, njema zisizo idadi, za marefu na mapana, hazipimiki kwa yadi, ilobaki sisi kushindana, dua tumuombe wadudi, ampokee Baba yetu, kwa fukisho la ubani, udi na uvumba.”
Ndugu Waombolezaji,
Marehemu Mzee Mtei alikuwa mmojawapo wa wajenzi wakuu wa misingi mikuu ya kiuchumi ya nchi yetu, hasa katika miongo miwili ya mwanzo ya Uhuru. Alikuwa mmojawapo wa wasomi mahiri wa kwanza katika fani ya uchumi wa mara baada ya Uhuru. Kwa sababu ya umahiri wake, haikuwa ajabu kwamba pale wakuu wa nchi za Afrika Mashariki walipoamua kuvunja iliyokuwa Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki, na kila nchi kuanzisha Benki Kuu yake, Edwin Mtei aliteuliwa kuwa Gavana Mteule, hata kabla Benki Kuu yenyewe haijaanzishwa rasmi. Kwa vyovyote vile itakavyokuwa, jina la Edwin Isaac Mbiliewi Mtei litahusishwa milele na Benki Kuu ya Tanzania; jina na saini yake yalikuwa kwenye noti za kwanza kabisa kutolewa na Benki Kuu ya Tanzania kati ya mwaka 1966 na 1974; na kati ya mwaka 1978 na 1981 alipokuwa Waziri wa Fedha wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa nafasi yake ya Gavana wa Benki Kuu na baadae Waziri wa Fedha, Mzee Mtei alikuwa mmoja wa washiriki wakuu katika kutunga na kutekeleza sera za kiuchumi za serikali ya Mwalimu Nyerere. Historia halisi ya nchi yetu haiwezi kumtenganisha Mzee Mtei na Azimio la Arusha lililopelekea utaifishaji wa mali za makampuni na mashirika binafsi na kuanzishwa kwa mfumo wa serikali kuhodhi njia zote muhimu za uchumi, yote yakifanywa kwa jina la Ujamaa na Kujitegemea. Na wala historia ya kweli ya nchi yetu haiwezi kumtenganisha Mzee Mtei na kushindwa kwa sera hizo kuanzia miaka ya mwisho ya sabini. Alikuwa ‘jikoni’ wakati sera hizo zinaandaliwa; na alikuwa mmoja wa ‘wapishi’!
Heshima yake kuu, na mchango wake kuhusu suala hili ambalo historia ya nchi yetu itauenzi milele ni huu; Mzee Mtei hakunyamaza mara alipogundua kwamba sera za kiuchumi za serikali yake, sera alizoshiriki kuzitunga na kuzisimamia hazitekelezeki tena. Mzee Mtei alimkabili Mwalimu na kumweleza ukweli wake; kwamba sera za kiuchumi za Azimio la Arusha zilikuwa zimeshindikana kutekelezwa; akamshauri Mwalimu kubadili msimamo wake ili kwenda sambamba na mahitaji ya nyakati na hali halisi ya uchumi wa kimataifa
Kwa: Gen Z na watu wote.
Yahusu - Mwendo wa Haki na Ukweli
Machalii na wasee wangu wote,
Natumai mko poa.
Hii message iko straight forward, hakuna kuzunguka,
ACHENI KUMFOLLOW SAA HII , huyu Mwigulu Nchemba.
👉 Unfollow kwa platform ZOTE , IG, X, TikTok, YouTube, kila mahali. Sababu iko wazi, anaongea bila facts, anapotosha watu,
na hajali haki ama ukweli.
Sisi kama Gen Z na wananchi hatuwezi endelea kupea mtu clout wakati anauza uongo.
Hii si chuki, si beef ya kibinafsi , ni simamo ya pamoja.
👉 Unamfollow = unaongeza kelele.
👉 Unam-unfollow = unasimamisha upotoshaji.
Chukueni hii kama direction ya mtaa na ibada takatifu. Mwendo mmoja, lengo moja.
Asanteni kwa kuskia na kuchukua hatua.
Post na sambaza matokeo.
Wenu katika ujenzi wa haki,
God bless Lema
@Elparton112@Simon_Machibya Isitoshe mwamba kafanya investment kubwa ya mavifaa halafu shoo hakuna ... ila alipata mapesa mengi wakati wa kampeni labda kama vegetable hawajamlipa