Rais wa Simba SC, Mohammed Dewji (@moodewji) leo amekutana na kuzungumza na wachezaji na benchi la ufundi pamoja na kuwapa hamasa kuelekea michezo ya mwisho wa msimu. #NguvuMoja
Moja ya malalamiko makubwa ambayo tumekutana nayo katika ziara ya Operesheni Maji Maji ni USHURU WA MAZAO ya Wakulima. Halmashauri za Wilaya zinazoongozwa na CCM zinawakamua wakulima ushuru mkubwa kiasi cha kuzidi kiwango kilichowekwa na sheria. Kwa mujibu wa sheria ya fedha ya Serikali za Mitaa Ushuru haupaswi kuzidi 3% ya thamani ghafi ya zao husika.
WADIAKONIA DUNIANI WAKUTANA TANZANIA
Askofu Dkt. Frederick Shoo amesema Mkutano wa Kmataifa wa Udiakonia ni fursa kwa wadiakonia kujifunza pamoja na kubadilishana mbinu mbalimbali za kidiakonia katika kuihudumia jamii kwenye maeneo mbalimbali duniani...
https://t.co/zHcz4zPZ2w
Alhamisi kama Leo mwaka mmoja nyuma ilikuwa 27.3.2024 ndio siku ambayo sitaisahau daima kwenye maisha yangu maana ndio siku niliyozaliwa UPYA kwenye MBUGA YA KATAVI.
Baada ya kipigo sana pale porini jana yake (Jumatano) WATEKAJI wakaniambia wanaenda kunirudisha DAR na nikatulie nifunge MDOMO. Nikakubali sawa, moyoni nikiwa na furaha kuwa nimeponea kwenye SHIMO LA SIMBA.
Safari ikaanza nikiamini narudishwa Dar. Gari ilikuwa speed sana kama kawaida speed ile ile ya 120-140, wakati wote huu nilikaa siti ya nyuma kati kati, pembeni kulia na kushoto kuna watu-mikononi nimefungwa PINGU na usoni kama kawaida nimevalishwa kinyago nisione naenda wapi na nipo na wakina nani.
Tayari jioni ilikuwa imeingia. Wakati huo nilikuwa nikilia njia nzima maana kulikuwa na baridi sana na ndani ya gari kulikuwa kumewashwa A/C ambayo ilikuwa kama inaingia kwenye mifupa ya kwenye viungio vya unyayo, magoti, enka na mabega. Mwili mzima ulikuwa kwenye maumivu makali.
Kila waliposikia kelele walikuwa wakinipiga na Chupa za bia kwenye magoti na kuniambia nikae kimya huku wakinitukana. Kama kawaida ndani ya gari wakati wote walikuwa wakivuta BANGI na kunywa pombe wakati wote.
NIKAPATA MSHTUKO BAADA YA KUTEMBEA MUDA MREFU NA KUONA KAMA MBONA HATUFUKI? Na kwa ile speed ya gari niliamini dar tungefika ndani ya masaa 8 lakini kwa ule muda tuliotembea niliona kabisa masaa yamezidi na tulikuwa tukitembea USIKU KUCHA.
Basi pale ndio nikakata tamaa kwamba sipelekwi dar huenda nahamishwa sehemu myingine. Kilichobaki nikawa mtu wa kulia tuu na nikiomba jambo baya zaidi lisinikute.
Basi baada ya kutembea kwa muda nikasikia gari imesimama. Na nikaambiwa “SHUKA UKAKOJOE”. Sikuwaomba nikakojoe, ila wao ndio wakaniamrisha nishuke nikakojoe. Kumbuka hapo nimeshaumizwa miguu siwezi kutembea.
Basi wakanivuta nikadondoka nje ya gari, maumivu yakaanza upya, wakaanza kunipiga upya na MABAPA YA UPANGA MGONGONI kuniforce nitembee niende nikakojoe. Nilishindwa kabisa kutembea.
Wakaanza kuniburuza na kunikokota kuelekea ndani ya MSITU. Nilikuwa napelekwa na watu wawili, wawili walibaki pale lilipo paki gari. Baada ya kufika na mimi walipopataka nikasikia SAUTI KUTOKA kwa wale ambao tumewaacha kwenye gari mmoja wao akasema kwa sauti “PIGA CHUMAAA”
Hiyo ndio ilikuwa sauti ya mwisho kuisikia. Nikajikuta nasikia kelele kichwani mwangu zikilia “Tiiiiiiiiiiiiinnnnnnnnnnnggggggg” kisha DAMU zikaanza kumwagika kutoka MASIKIONI, MDOMONI,PUANI.
Gafla nikaona wale watekaji wananivua boshori iliyokuwa KICHWANI, na kufungua pingu zilizokuwa mikononi. Baada ya hapo wakaanza kuondoka huku wakikimbia wakiamini wameshamaliza kazi “WAMEUA”.
Nikiwa pale chini nikaona kabisa roho inaacha mwili. Nikaanza kupush kutafuta PUMZI , nikapush kama sekunde 30 kisha nikapata Flow mzuri ya kupumua. Baada ya hapo nikaanza kusmhukuru MUNGU.
Ilikuwa ni pembezoni mwa MTO ambao sikuona kitu zaidi ya maji ya mto. Kisha nikasikia mlio wa ile gari ya watekaji kwa mbali inaondoka. Pale pale nikajua hapa SIFI TENA.
Ilikuwa ni ALFAJIRI mida kama ya saa 12 asubuhi kuelekea saa 1. Kisha nikaanza kuscrow na mikono maana miguu haikuweza kabisa kutembea.
Nikajivuta ndani ya ule MSITU nikiwagika damu za kutosha kitoka kichwani. Mdomoni meno yalikuwa SHAGALABAGALA. Ile risasi ilivunja TAYA YOTE YA CHINI NA kutokea kwenye kidevu.
Baada ya muda nikiwa natafuta upenyo nikasikia mlio wa gari likipita. Nikajua upande huu kuna barabara. Nikajivuta mpaka ilipo barabara. Wakati wote nikiwa porini tembea yangu ilikuwa ni kuscrow (kutembelea tumbo) na mikono kama nyoka na kuburunguka kwenye vibonde.
Mpaka nikafika ilipo barabara. Ilikuwa barabara ya VUMBI. Ndio pale NIKAPATA MSAADA WA KIBINADAMU ambapo nikarekodiwa ile video ambayo ilisambaa siku kama ya leo mwaka jana. Hiyo ndio safari yangu ya KUTEKWA.
Nimesimulia siku zote nne kila siku kilichojiri mwaka mmoja nyuma.
Nawashukru WATANZANIA KWA KUNIPAMBANIA. Kwasasa nitajilinda SANA KWA WIVU MKUBWA SANA KWAAJILI YENU.
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
CONSISTENCY AND RESILIENCE
Angalia video hizi mbili kwa makini.
Hii ni Korogwe,Tanga leo Asubuhi saa 5 :00 viwanja vya shule ya Msingi Mazoezi,mkutano ulipoanza ilishuka mvua kubwa sana.
Viongozi wa CHADEMA tukakubaliana hakuna kuahirisha mkutano wala kukimbia mvua,tumehutubia katika mvua kubwa.
Makamu Mwenyekiti J.W.Heche amehutubia saa nzima katika mvua kubwa huku Wananchi wachache wakiwa wamejificha mvua katika vibanda lakini wengine walibakia uwanjanj bila kujali mvua.
Video ya pili ni mvua baada ya Kukatika watu wakiwa wameongezeka zaidi na kutoka katika Vibanda.
Kocha msaidizi wa Simba SC Seleman Matola akizungumza kuelekea mchezo wa nusu fainali CRDB Bank Federation Cup dhidi ya Singida Black Stars utakaochezwa uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Manyara
@CRDBBankPlc@azamtvtz@PrecisionAirTz