MAJIZZO NJOO DARASANI!
Umeleta hoja za Kisiasa alafu unajitoa?! Usijitilishe huruma, SKIA..
MSANII ni KIOO CHA JAMII, hivyo TASWIRA au KAZI yake, inatakiwa KUAKISI (Reflect) JAMII YAKE, kwa wakati muafaka. Kama Jamii ina NJAA, Msanii nae inabidi awe hajala au Kazi yake ijae MAUDHUI ya Njaa.
SANAA ni Burudani, Elimu, Utambulisho na Biashara. Upande wa ELIMU ni kwa Kui habarisha, kanya, rekebisha, shawishi pamoja na KUISEMEA Jamii. Sio lazima ufanye vyote, maana ITIKADI, DINI, MITAZAMO, JINSIA, TAMADUNI huweza kukuzuia kufanya yote, ila kwenye masuala ya Kijamii yanayokuathiri pia, NI WAJIBU WA KILA MSANII KUSIMAMA NA JAMII YAKE.
Jamii ikipata Madhila, kimbilio lake ni WASANII. Msanii anafikisha UJUMBE kwa Watawala, Watesi au Wakombozi. MAUDHUI YA SANAA hugeuka Faraja, Tiba, Tumaini; and ART becomes THERAPY & MOUTHPIECE. WANANCHI wakajiona hawapo wapweke au peke yao (Feel Seen). Mfano KATUNI ZA KIPANYA. Au NYIMBO ZA ROMA MKATOLIKI na NAY WA MITEGO.. Jamii ikiona na kusikia, inapata hauweni na tumaini na Watesi wanapata Jumbe.
MAJIZZO, Watu wametekwa, wameuwawa, wapo Rumande, wamebambikiwa Kesi, wamepigwa, wamepotea, wamelawitiwa, SERIKALI KIMYA!
Wasanii wanaimba MAPENZI na KUISIFIA SERIKALI iliyo waangusha WANANCHI. Wananchi ndio wanaipa Madaraka Serikali, ila inayatumia vibaya (Jeshi, Polisi, Usalama) kutisha na kuminya UHURU. Na inatumia WASANII kuwashawishi na Kuwapumbaza Watu ili wao Wabaki MADARAKANI.
Pengine mimi binafsi sijafanya hivyo, ila ni kweli kuwa Wasanii tumeshindwa kutekeleza wajibu wetu kama Kioo Cha Jamii, na Sauti za Wasio nazo.
Umeongelea SIASA, sisi hatupo huko, na umeongelea Mashambulizi PERSONAL, well post inayofata nitakuonyesha what personal is… usijitie Huruma, wala kuleta kiherehere cha uGodfather, ingawa najua umetumwa.
The Leader