Nendeni jela wanangu. Kuna maisha. Kuna wanetu wameishi kule miaka tele. Sio mwisho wa dunia. Kesi za mchongo zina mwisho. Lakini majitoleo yenu yatakumbukwa milele. Jamhuri inawashitaki. Jamhuri ni sisi. Na sisi hatuwadai. Mungu awalinde. Tutashinda. Ninyi & wenzetu wote.
Hawa wanaotukanwa kila siku kwasababu wanaPush Hashtag zisizo rafiki kwa Watanzania wengi wanaona ni sawa kwasababu ndio tunaocheka nao, tunaoMeet, tunakula na kunywa nao, tuko kwenye biashara zao.
Na wanajua kabisa watatukanwa na watavumilia kutukanwa na siku wakiona inatosha wataacha na watarudi kwetu wakisema โNisameheni, yale mambo siendelei nayo tena, najua niliwakera ila nimeachaโ. Na sisi kama kawaida tutawapokea vizuri tukisemaโAngalau umejitambua, hayo ndio maneno, safi umefanya jambo zuriโ na maneno mengine mengi. Pasipo kutambua waliyoyafanya tayari yalishasababisha damage/madhara mengi.
Ninachojaribu kusema chochote kibaya kwa sasa kinapaswa kukataliwa sio kwa maneno tuu bali hadi vitendo vihusike, kama utakataa hashtag kwa maneno ila mtu huyohuyo ni mshirika wako kwenye mambo mengine ina maana ataona ni sahihi yeye kuendelea kufanya yale yasiyo sahihi. (Mfano, ukikemea uuaji alafu marafiki zako ni wauaji ina maana na wewe unachangia wauaji wale wawe comfortable kufanya yale mauaji kwasababu hakuna repercussions, (wanaona hutowafanya chochote mwisho wa siku).
Tunapokataa hashtag zao alafu haohao ndio tunawaita marafiki, wapenzi, washkaji, dada/kaka, shangazi, Mwana, shoga yangu, Shemeji, ni kama tunawapa urahisi wa wao kufanya yale wanayoyafanya.
Tukikataa Hashtag tukatae na wanaozisambaza, na hata siku wakiona wameshajikusanyia mitonyo ya kutosha hivyo wanataka kuacha na kujirudi kundini pia muendelee kuwakataa, itakuwa ni funzo kwao na funzo kwa wale wanaofikiria kufanya yale yanayoumiza Wananchi.
Kama tutapuuzia na kuona ni ujinga au hatuwezi basi pia tusilalamikie habari za Hashtag Kandamizi. Maana malalamiko ya bure bila vitendo ni sawa na kumpigia mbuzi gitaa. Mabadiliko huanza na wewe, Kesho Bora umeibeba wewe.
#TajiriLaKihaya
Hakuna maendeleo yoyote yanayozidi Damu ya Raia mmoja kumwagika!
Uhai wa mtu mmoja ni mkubwa kuzidi mradi wowote ule haijalishi umetumia gharama gani na una ukubwa gani!
Maana miradi yote inaletwa Kawa ajili ya Raiaโฆ
Raia wasipokuwepo miradi Haina maaana๐ฏ
No amount of development will make us forget our brothers and sisters who died๐๐๐
Kitu nimejifunza in hard way ni; hakuna kitu juu ya utu, uhai na haki
Despite all differences, status, social classes, levels na treatments ila Uhai, utu na haki vinasimama no matter what
Kwa hili kama binadamu wa kawaida nimepaswa kua na common sense na kubadili mienendo yangu
Hongera Dr. Samia kwa ushindi wa kishindo
Hongera ,kwa watu milioni 31 kutoathiriwa na hali ya maandamano iliyojitokeza siku ya uchaguzi wakakupigia kura kukuchagua
Uongozi wako wa usikivu uliwahamasisha watu milioni 31 kufurika na kuvijaza vituo vya kupigia kura kukuchagua na kupuuzia wote walioshawishi kususiwa kwa uchaguzi
Kwa kukemea kwako na kukomesha matendo ya utekaji na ukamataji holela wa wapinzani wako, kuliwapa motisha watu milioni 31 kusimama kwenye misururu mirefu kwenye vituo vya kupigia kura. Ilibidi vituo hivi viongeze muda wa kupiga kura ili kumpa kila raia haki ya kukuchagua.
Hongera Dk. Samia. Ushindi wako wa kishindo unaonesha ni asilimia mbili tu ya vizabizabina, ndio walisusia kwenda vituoni kukuchagua.
Naam!
Ni asilimia mbili tu ya wananchi, ndio walivamia vituo vya kupigia kura, kuchoma kura na kukimbia na msanduku ya kura. Hata hivyo nawapongeza maafisa wa tume kwani waliweza kukusanya kura zilizoungua na kuchanwa bila athari yoyote.
Sasa umeapishwa kuwa rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania. Nakuombea moyoni ubaki na ukweli wa kilichotokea.
As a president, I know you are the most informed citizen in our country. You know the truth. You know what really happened. You know how you won.
Please madam President, take your time, have a deep breath and reconstruct the situation.
Anticipate where we failed as a nation. The real causes and consequences. Who were real perpetrators of the situation. The failure in intelligence gathering to rescue the situation.
Utakachokipata, kifanyie kazi haraka.
Rudisha Tanzania ilipotoka.
Biashara Asubuhi, Mahesabu Jioni.
Leo, Jumamosi ya tarehe 28 Juni 2025, saa mbili kamili asubuhi, nimekuwa mtia nia wa kwanza kufika katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Siha, Mkoa wa Kilimanjaro, kuchukua rasmi fomu ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Siha.
Hatua hii ni ya heshima, lakini pia ni ya dhamira. Nimefika mapema si kwa bahati, bali kama ishara ya namna ninavyochukulia jukumu hili kwa uzito, umakini, na heshima kwa wananchi wa Siha.
Ninakuja si kwa maneno tu, bali na rekodi ya kazi, uwezo wa kushirikisha watu, na maono ya kujenga Siha yenye maendeleo jumuishi, fursa kwa vijana, na huduma bora kwa wananchi wote.
Nimelelewa Siha. Nimepitia changamoto zake, nimeiona thamani yake, na naamini sasa ni wakati wa kizazi kipya kutoa mchango wake.
Leo ni mwanzo wa safari rasmi. Safari ya kusikiliza, kujifunza, na kutumikia kwa moyo wote.
Siha ni nyumbani. Na sasa, ni wakati wa kuijenga pamoja.
@jaliluzaid Kila la kheri kaka Jalilu. Sema sikuwepo humu Kwa muda ndio maana sikufahamu jambo hili la kheri. Yote na yote Mwenyezi Mungu awape moyo wenye kusamehana na kuonea huruma๐