Tatizo ni nini?
Ni huyu SamiaSuluhu! Uwezo wake mdogo na ubaguzi wake wa kizanzibari anaona sifa kutimua watanganyika hovyo na kutofuata sheria, katiba!
Shida watanganyika wasiojielewa na kutekeleza huu upumbavu!
Acha twende hivihivi hadi #TutaelewanaTu
Kwa kuwa, maamuzi ya maombi ya marejeo (Revision) yaliyofunguliwa na DPP dhidi ya Tundu A.M Lissu, katika mahakama ya rufaa Tanzania yamesoma na Tundu A.M Lissu AMESHINDA.
Upande wa Jamhuri una machaguo mawili; turudi mahakama kuu kuendelea na tulipoishia katika kesi ya uhaini wa mchongo, au waifute hiyo kesi (nolle prosequi) na kumuachia huru Tundu A.M Lissu.
Huko Mahakama Kuu ndiyo kuna wale mashahidi wao wa siri kwenye kichumba cha joto, na wamewamaliza na walitaka kuingiza mashahidi wengine wapya. Ushahidi wao wa msingi ulikataliwa mapema.
Kama upande Jamhuri wakiamua kuendelea na kesi hiyo, tunakwenda kwenye hatua ya ‘No Case To Answer’ na Tundu A.M Lissu akikutwa na kesi ya kujibu anatakiwa kuanza kujitetea mara moja.
Mashahidi wa TAL unawakumbuka? TUONDOKEEE….
Baraza Kuu la Maaskofu Katoliki Afrika Mashariki na Kati (AMECEA) limemchagua Askofu Gervas Nyaisonga wa Jimbo Kuu Katoliki Mbeya kuwa Rais Mpya wa baraza hilo kwa kipindi cha miaka minne. Askofu Nyaisonga anachukua nafasi ya Askofu Charles Sampa Kasonde wa Jimbo Katoliki Solwezi, Zambia ambaye amemaliza muda wake wa kipindi kilichoanzia mwaka 2018.
AMECEA ilianzishwa mwaka 1961 na inaundwa na nchi 10 wanachama ambazo ni Eritrea, Ethiopia, Kenya, Malawi, Sudan Kusini, Sudan, Tanzania, Uganda, Zambia na Djibouti. Makao makuu yakiwa Nairobi nchini Kenya. Hii ni mara ya pili kwa Askofu kutoka Tanzania kuwa Rais wa baraza hilo kubwa la kiroho, wa kwanza akiwa Askofu Mkuu mstaafu Josephat Lebulu (Arusha) aliyeongoza kuanzia 1995 hadi 2002.
Askofu Gervas John Mwasikwabhila Nyaisonga, alizaliwa tarehe 3 Novemba, 1966, Wilayani Bunda, Mkoani Mara. Alisoma shule ya msingi Mwenga iliyopo Vwawa mkoani Songwe na kuhitimu mwaka 1982. Mwaka 1983 alijiunga na St. Joseph Seminary iliyopo Sumbawanga kwa elimu ya sekondari na kuhitimu mwaka 1986. Mwaka 1987 alijiunga na shule ya sekondari Sangu, Mbeya kwa masomo ya A-level na kuhitimu mwaka 1989.
Alipata wito wa Upadre na mwaka huohuo alijiunga na Seminari Kuu ya Kibosho kwa shahada ya kwanza ya Falsafa (Bachelor Degree in Philosophy) na kuhitimu mwaka 1992. Kisha akaendelea na masomo ya Theolojia Seminari Kuu ya Charles Lwanga (Segerea) na kuhitimu shahada ya kwanza ya Theolojia (Bachelor Degree in Theology) mwaka 1995.
Alipokea daraja takatifu la Ushemasi na kutumwa kwa huduma kichungaji katika Parokia ya Itaka, Jimbo Katoliki Mbeya kwa muda wa mwaka mmoja. Tarehe 11 Julai 1996 alipewa daraja takatifu la Upadre na Hayati Askofu Yakobo Dominic Sangu. Baada ya Upadrisho alifanya utume wake kama Paroko Msaidizi, Parokia ya Itumba Mbeya, na Mwalimu wa Bible Knowledge Seminari Ndogo ya Mbalizi.
Mwaka 1998 alitumwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kwa shahada ya kwanza ya Elimu (Bachelor of Arts with Education) akijikita katika somo la Jiografia ambapo alihitimu mwaka 2001. Alirudi jimboni na akateuliwa kuwa Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Pandahill.
Alifundisha Pandahill hadi mwaka 2006 alipotumwa tena masomoni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), kwa shahada ya umahiri ya Jiografia (Master of Arts in Geography and Environmental Management) na kuhitimu mwaka 2009. Baada ya kuhitimu alitumwa kuwa Mhadhiri Msaidizi (Assistant Lecturer) Chuo Kikuu SAUT, Mwanza.
Mwezi Agosti, 2010 alitumwa Chuo Kikuu cha Vechta nchini Ujerumani kwa masomo ya shahada ya uzamivu katika Jiografia (PhD in Geography). Tarehe 9 Januari 2011 akiwa masomoni nchini Ujerumani, alipokea taarifa kutoka Vatican kwamba Baba Mtakatifu Benedict XVI amemteua kuwa Askofu mpya wa Jimbo Katoliki Dodoma baada ya Askofu Yuda Thadeus Ruwaichi aliyekuwa Askofu Dodoma, kuteuliwa kuwa Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Mwanza.
Alitumikia Jimbo la Dodoma hadi tarehe 17 Februari 2014 ambapo Papa Francis alimteua kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki Mpanda baada ya aliyekuwa Askofu wa jimbo hilo William Kikoti kufariki dunia.
Tarehe 21 Desemba 2018 Jimbo Katoliki Mbeya lilipandishwa hadhi kuwa Jimbo Kuu, na Papa Francis akamteua Askofu Gervas Nyaisonga kuwa Askofu Mkuu wa kwanza wa jimbo hilo. Mwaka huohuo 2018 alichaguliwa kuwa Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) na kuongoza kwa kipindi cha miaka 6 hadi mwaka 2024.
Hatimaye Jumapili tarehe 26 Julai 2026 amechaguliwa kuwa Rais wa Baraza la Maaskofu Afrika Mashariki na Kati (AMECEA). Tumtakie heri na matashi mema Baba Askofu Mkuu Gervas Nyaisonga katika utume wake huu mpya.!
@MalisaGJ_
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, ameihoji Serikali ya Tanzania akitaka itaje wazi ni nani anayekwamisha mchakato wa Katiba Mpya, kutokana na kauli ya Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, iliyowataka Watanzania ‘kupambana’ ili kuipata.
Akizungumza Julai 28, 2026, alipowatembelea na kuzungumza na wafanyabiashara katika Soko la Samaki la Kimataifa la Kirumba Mwaloni mkoani Mwanza, Heche amehoji mantiki ya kauli hiyo iwapo viongozi wakuu wa nchi tayari wanaunga mkono mchakato huo.
"Kutaka Katiba Mpya siyo kosa. Mmemsikia hata Nchimbi alisema tukomae Katiba ije, lakini anatumia lugha ya kutuchanganya; anasema Rais anataka Katiba na yeye pia anataka Katiba. Sasa inakwamia wapi ambapo anataka sisi tukomae?" amesema Heche.
Kauli hiyo ya Heche inakuja kutokana na hotuba iliyotolewa na Dkt. Nchimbi mnamo Julai 24, 2026, wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 15 wa Mwaka wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC).
Katika mkutano huo, Dkt. Nchimbi alisikika akisema: "Nikiambiwa kuna jambo kama Makamu wa Rais niwaambie Watanzania, nitasema pambaneni mpate Katiba Mpya- Katiba ambayo ina makubaliano ya wadau wote, Katiba yenye muafaka katika taifa, Katiba ambayo kila Mtanzania popote alipo atajisikia fahari kujitambulisha, na Katiba inayojali maisha."
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Bw. John Heche amesema tatizo kubwa la Tanzania ni uongozi wa serikali unaotokana na Chama Cha Mapinduzi CCM pamoja na jitihada zinazofanywa za kunyamazisha sauti za wenye maoni, mawazo na hisia tofauti kuhusu mwenendo wa serikali pamoja na matumizi yasiyo sahihi ya rasilimali za Nchi.
Heche ametoa kauli hiyo leo Julai 28, 2026 wakati alipotembelea kijiwe maarufu cha Mbao, Mwaloni, Sabasaba Jijini Mwanza na kuzungumza na wananchi, akisema hofu iliyopo Nchini inatokana na matukio ya utekaji, upoteaji na kuumizwa kwa watu wanaopaza sauti kuikosoa serikali, suala ambalo limewaathiri si tu wapinzani bali pia wanachama wa Chama tawala.
"Kusema tunataka katiba mpya sio kosa na tatizo la nchi hii ni Katiba. Watu wote wanaojitahidi kutoa sauti kwamba sisi ni Nchi ya tatu kwa kutoa dhahabu kwanini watu wetu ni maskini? Kwanini watu wetu wanaumizwa? Kwanini watu wetu hawana matibabu? Kwanini ziwa lipo hapa lakini watu hawana maji? Kwanini wakinamama wanajifungua mazingira mabovu? Ukipaza sauti ni aidha uuwawe, utekwe au upotezwe hata kama ni MwanaCCM, Polepole alikuwa Mwenezi wa CCM Mjumbe wa Kamati kuu CCM, Balozi aiyechunguzwa na Vyombo vya ulinzi na usalama leo amepotea kama kuku. Tutaishi kwa hofu mpaka lini?
... Wengine tuna familia tunaelewa hatari iliyopo lakini nimejiuliza kama sio mimi ni nani? Kama sio sasa ni lini? Mimi nimeamua kuwa mstari wa mbele, tuungeni Mkono, mnataka tumuachie Mungu? Wanatuambia tutaenda kuishi vizuri mbinguni. Mungu ambaye anataka tukaishi vizuri mbinguni, angetupa dhahabu? Angetunyima kila kitu ili tukaishi vizuri mbinguni na kusubiri maisha hayo mazuri mengine. Mungu ambaye anataka tukaishi vizur mbinguni asingetufanya kuwa wamiliki pekee wa Tanzanite duniani, asingetupa mbuga kubwa kuliko zote." Amesema Bw. Heche.
‼️🚨READ THIS‼️
Mmesoma spana ya Profesa Shivji?
https://t.co/sDUz9B1wpq
“No reasonable Tanzanian could imagine that a university lecturer would issue a threat to burn public buildings and police residences.
But there we are! We are being told that even after the unrest around the general elections on 29 October 2025 resulted in the killings of hundreds of youths, and the subsequent all-pervasive fear that reigns over the country, we still have an isolated Tanzanian courageous enough to issue threats to burn public buildings and police residences.”
Tafsiri:
"Hakuna Mtanzania mwenye busara anayeweza kufikiria kwamba mhadhiri wa chuo kikuu angetoa tishio la kuchoma majengo ya umma na makazi ya polisi.
Lakini ndio hivyo! Tunaambiwa kwamba hata baada ya machafuko yaliyotokea wakati wa uchaguzi mkuu wa tarehe 29 Oktoba 2025 yalisababisha mauaji ya mamia ya vijana, na hofu iliyoenea nchini kote, bado tuna Mtanzania mmoja jasiri wa kutosha kutoa vitisho vya kuchoma majengo ya umma na makazi ya polisi."
😁👊����🔥 Washa motoooo Prof!
Msije mkamteka tu maana nyie @tanpol mnaendeshwa na akili za fom fo felia Abdul Halim na siyo sheria! KOMENI!
VIDEO:
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tanzania Bara, John Heche ameeleza kuwa ana taarifa za ndani za uhakika kuwa kuna mpango wa wa yeye kukamatwa.
Akizungumza siku ya Jumatano kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa CHADEMA Mkoa wa Mwanza uliofanyika katika soko la Mbao, Kata ya Igoma Jijini Mwanza, Heche amesisitiza kuwa yeye ni mtu huru anayefanya kazi kwa mujibu wa sheria na hatishiki na hatua hizo, akisema, "Mimi nimezaliwa mara moja, nitaishi mara moja na nitakufa mara moja"
Aidha ameeleza kuwa kuna gari aina ya Toyota Land Cruiser (hardtop) nyeupe iliyofika nyumbani kwake asubuhi ikiwa na namba za usajili T 318 EQJ. Baada ya kufanya uchunguzi na kupiga picha, imebainika kuwa namba hizo ni za kughushi kwani zimesajiliwa kwa ajili ya katapila la kutengenezea barabara na siyo gari hilo
Heche anawataka Watanzania wasikubali kunyimwa amani wala kutekwa katika mazingira yasiyoeleweka, huku yeye mwenyewe akisisitiza kuwa hawezi kukimbia na kuwasihi raia wasikubali kumuacha achukuliwe katika mazingira ya kutatanisha, akisema kuwa ni lazima kukataa kuishi kwa hofu katika nchi yao.
Hii ni picha ya CCTV ya watu waliokuja kunifuatilia nyumbani kwangu.
Wameulizia nyumba yangu, na baadae wakaondoka bila hata kutaka kuingia au kueleza kwanini wanatafuta nyumba yangu.
Tumefuatilia hiyo gari na kugundua kwamba namba za usajili inazotumia sio namba halisi..
Namba hizo T318 EQJ ni namba zilizosajiliwa kwa magari ya kulima barabara sio namba za Land Cruiser hardtop hiyo.
Polisi wanapaswa kutuambia hao ni kina nani na nia yao hasa ni ipi kwangu.
Hatutakubali kuishi kwa hofu kwenye Nchi yetu.
Mambo ya aina hii yanaweza kuingiza Nchi kwenye hatari kubwa sana .
Watanzania sisi tutafanya kazi yenu bila hofu, msikubali kuona viongozi wenu wanatishiwa.
‼️UGAIDI!! UGAIDI!! UGAIDI!!‼️
Anaandika Wakili @AdvMatata
Kuna mtu aliwahi kusema hii nchi yawezakana Mbinguni ni "Channel" ya vichekesho. Sasa naanza kuamini.
Huyu kwenye "Clip video" hii anaitwa Athuman Abdallah Muganda, mzaliwa wa Urambo- Tabora na mfanyabiashara wa Kariakoo- Dar es Salaam.
Video hii alijirekodi tarehe 7/7/2026 siku ambayo baadhi ya watanzania walitangaza kuwa kutakuwa na maandamano, alirekodi kuonyesha hali ilivyo Kariakoo kwa kuonyesha kuwa hapakuwa na watu kitu ambacho kinaweza kuwa kilitokana na watu kuhofia usalama wao siku hiyo.
Baada ya yeye kuweka Video hii mtandaoni kumbe muda haukupita Polisi walienda kumkamata na kumweka ndani katika kituo Cha Polisi Buguruni kwa zaidi ya siku kumi Hadi walipomwachia kwa dhamana tarehe 18/7/2026.
Ilipofika juzi aliambiwa akaripoti na alipofika alipelekwa moja kwa moja mahakamani, katika mahakama ya Wilaya Ilala iliyoko Kinyerezi-Dar es Salaam na kusomewa shitaka la ugaidi.
Mpaka ninapoandika habari hii, Muganda yuko mahabusu ya Segerea kama mtuhumiwa wa ugaidi kwa kurekodi video clip hii.
Swali la kujiuliza ni lini haki ya kukusanya, kupata taarifa na kutoa taarifa au maoni kama katiba yetu Ibara ya 18 inavyoruhusu imekuwa kosa, tena kosa la ugaidi nchini?.
Leo nimemsikia Waziri wa mambo ya ndani akisema hakuna ugaidi nchini. Alichokisema kimenipa picha kuwa hata wao wanajua kuwa hakuna ugaidi "wa kweli" nchini bali ugaidi "magumashi" wenye malengo ya kisiasa nchini.
Anyway;Sisi kazi yetu ni kuwasikiliza wakisema Ugaidi upo sawa, wakisema haupo sawa, wakiwafungulia watu kesi za ugaidi sawa, wakizifuta Sawa, sisi tunasema sawa tu.
Sisi ni wale ambao tumetajwa kwenye maneno ya Mungu yasemayo " heri mwenye njaa na kiu ya haki"
Siku yaja na haiko mbali.
Gaidi Muganda endelea kusota hapo Segerea, Mungu anasikia kilio cha mke na watoto wako wanaokutegemea, anasikia kilio cha wazazi wako huko Urambo wanaokutegemea pia na atajibu kwa wakati dhidi ya kila aliyehusika na dhambi hii.
Russian actor Alexey Yarmushchik published a video criticizing Putin, stating that he no longer wants to remain silent.
According to the 25-year-old Yarmushchik, he does not know a single peer of his who loves and respects Putin — they only fear him.
“I do not want you to be my president. Never in my life. […] I do not want to watch your television. […] I want to listen to my songs. I do not want to use VK. I want to use Instagram. […] I do not believe that Crimea is ours. […] All my acquaintances are leaving. I do not know where these people are who love you as president and respect you. You are not my president.”
Muigizaji wa filamu wa Russia leo kaposti video hii akisema kuwa vijana wenzake hawamtaki na wala hawamuheshimu Putin ila wako kimya sababu wanamuogopa sana Putin. Kijana akaendelea kumwambia Putin, sitaki uwe Rais wangu na wala sitaki kukuona kwenye Tv. Mimi nataka kutumia Instagram bila VPN. Sitaki kuendelea kuonewa na kunyanyaswa na wewe.
Video imeenda viral sababu Russia Putin anaogopwa mpaka na panya. Putin ni kama Mungu huko Russia ukiongea tu ni kifo kinakufata. So msanii huyu mwenye jina kufanya video kabisa na kuposti inaonyesha wa-Russia uwoga umeanza kuwatoka juu ya Putin na wanataka kupambana sasa.
Kwetu Tanzania eti msaniii mwenye jina afanye video kama hii amsema Samia directly hivi bila mafumbo wala kupeleka lawama kwa mawaziri ni Never. Tanzania wasanii wote ni machawa. Stupid kabisa
In Tanzania, during the Hormuz crisis, the government has taken over the fuel supply bidding process, delegating purchase of petroleum to parastatal TPDC in a closed tender.
One provider emerged for TPDC, and is now stronger than ever: Namaro Energy ⬇️
https://t.co/sFCyiNyT2A
‼️TAARIFA MBAYA‼️
Usiku wa leo, majira ya saa kumi, watu wanne waliokuwa na silaha za moto na vifaa vinavyodaiwa kutumika kuvunja mlango, huku wakiwa wameficha nyuso zao kwa vitambaa na bila kujitambulisha, wanaripotiwa kuvamia nyumbani kwa Katibu wa Wilaya ya Shinyanga wa BAVICHA, Alfred Masanja, na kuondoka naye.
Hadi sasa, haijafahamika alipelekwa wapi wala ni akina nani waliohusika na tukio hilo.
Tunafuatilia kwa karibu taarifa za tukio hili na tutatoa taarifa kamili leo Asubuhi
Jackson Mnyawami
Katibu wa Kanda ya Serengeti.