WITO MAALUM KWA VIONGOZI WA KIROHO/DINI TANZANIA!!
Mababa wa Imani mko wapi? Mko wapi Maaskofu wangu? Mko wapi Mitume na Manabii? Mko wapi Mashekhe Nchi Hii? Hayawaumi haya yanayotokea, au Hamuyasikii jamani!!
Serikali, @NEC , Polisi @tanpol na WaTanzania, wanawasilikilizia....
#Updates
1. John Pambalu, Mkurugenzi wa Mafunzo, Oganaizesheni na Uchaguzi.
2. Twaha mwaipaya.
3. Lucas Ngoto mwenyekiti wa Chama kanda ya Serengeti.
4. Na wanachama wengine
Wamepigwa na kuumizwa sana na kutupwa Bagamoyo.
Tanzania hii hii? Unamkamata mtu mahakamani Kisuti, kwa kosa la kwenda kusikiliza kesi inayomuhusu Mwkiti wa chama chake, unampeleka porini/msituni badala ya kituo Cha polisi, unamtesa, unampiga, unamjeruhi, halafu unamtelekeza! Like seriously? Si ni utekaji huo?
#UPDATE
Nimepigiwa simu na @Twaha_Mwaipaya anasema yeye na wenzake aliokamatwa nao walichukuliwa hadi Ununio kisha wakaanza kupigwa sana. Baada ya kipigo wameenda kutupwa Bagamoyo. Ameniambia wanahitaji msaada wa haraka kwa sababu miongoni mwao kuna watu wanavuja damu sana.
Mmoja kati ya Viongozi WACHACHE SANA wa Kidini ambao akili zao "hazijalogwa"! Tunamuombea aendelee vivyo hivyo! Hawa watawala wanahitaji "sindano" iwaponye nafsi zilizopigwa ganzi!
Baba Askofu Dr.Benson Bagonza (PhD) ni mmoja tu. Umpende utamuelewa, usimpende utamuelewa. Amenyooka kama rula. Watu pekee wasiomuelewa ni wale waliokosa chanjo ya pepopunda ama kifaduro. Period.!
Kuna uchungu unatengenezwa kwenye nchi Hii! Nani atakuja kiwazuia wasilipize visasi? Kulikuwa na sababu ya kufika huku? Kwanini @tanpol wanamchonganisha @SuluhuSamia na Wananchi wake? Kwamba ndio atapendwa zaidi?
#Updates Waliopigwa na kuumizwa sana na Jeshi la Polisi wakipakiwa kwenye gari na kupelekwa hospitali baada ya kuumizwa sana na Jeshi la Polisi na kutupwa msitu wa Mabwepande.
#UpdatesKutokaMahakamaniKisutu
Rai Wema na Viongozi wa Chadema Waliokwenda Mahakamani Kisutu Kufuatilia Kesi inayomkabili Mkt @TunduALissu Wamepigwa Na Kuumizwa sana Na Polisi bila sababu yoyote wakati, Hakuna Zuio lolote la mahakama kuzuia watu kwenda Mahakamani Kusikiliza Kesi
Msafara wa Makamu Mwenyekiti Bara Mhe. @HecheJohn umezuiwa na Jeshi na Polisi muda huu maeneo ya Selandar Bridge usiende Mahakama ya Hakimu Mkazi kufuatilia mwenendo wa kesi ya Uhaini inayomkabili mwenyekiti wa Chama Taifa Mhe. @HecheJohn leo tarehe 24 Aprili 2025.
Huyu Mtu Amebeba Kusudi la Mungu! Mkono wa Mungu Uko Juu Yake! Kidole Cha Mungu Chamuongoza! Ni Mfano wa Daudi Enzi za Mfalme Sauli! Nachelea Kusema Kushindana/pambana Naye Inaweza Kuwa, Unapambana na Mungu, Nyuma Yake! Inahitaji Uwe Hujui Kabisa Kusoma Alama za Nyakati, rohoni!!
@EduTalkTz Unakosea Sana Ndg @EduTalkTz! Neno la Mungu Linatufundisha Kwamba, Unaweza 'Kumjua Mungu'! Na Mungu Anaweza 'Kujifunua Kwako'. Kiwango Chako Cha Kumjua Mungu Kinategemea 1. Kiu & 2. Bidii ya Kumtafuta. He's Open For All! Kwani Unasoma Biblia Gani Wewe? Soma Dan 11:32b & Jer 29:13
Unakosea Sana Ndg @EduTalkTz! Neno la Mungu Linatufundisha Kwamba, Unaweza 'Kumjua Mungu'! Na Mungu Anaweza 'Kujifunua Kwako'. Kiwango Chako Cha Kumjua Mungu Kinategemea 1. Kiu & 2. Bidii ya Kumtafuta. He's Open For All! Kwani Unasoma Biblia Gani Wewe? Soma Dan 11:32b & Jer 29:13
Binafsi ninaamini hakuna anayemjua Mungu, tunadanganyana na kuliwazana tu.
Tunachokijua na tunachoendelea kujuzana ni story zetu tu tulizozitengeneza kuhusu Mungu na kupashana mara kwa mara mpaka zimegeuka kuwa ukweli.
Hata ile lugha ya โnimesoma neno na kuongozwa na rohoโ ni kauli za kuhalalisha zile story tu, sio vinginevyo.
Unalala mahabusu tena sio kwa sababu wewe ni jambazi isipokuwa kwa sababu umekuwa msitari wa mbele kuibua mateso,utekaji na mauaji ktk kila kona ya jamii yetu.Una heri kubwa sana kwa sababu mateso haya yana thawabu kubwa kwako,familia yako na Nchi yetu. Ukatili huu hauna muda mrefu sana. Jipe Moyo Mkuu sana.
This is alarming! Kwanini Watawala wanakosa utu kiasi hiki? Kwanini msiwarudishe hao waliotekwa na kuzuia utekaji zaidi? Kwanini wahusika wasiwajibishwe kisiasa na kisheria? Kwanini msikubali kuweka mazingira ya usawa kwenye chaguzi? Mbona tuiharibu nchi yetu wenyewe?
ZIFAHAMU SHERIA ZA MSINGI UWAPO MIKONONI MWA POLISI
IMEANDALIWA NA MAWAKILI
1. Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho ni haki yako.
2. Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.
3. Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.
4. Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa hata kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya kukamatwa.
5. Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.
6. Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kutii amri halali.
7. Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.
8. Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.
9. Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.
10. Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.
11. Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.
12. Ni haki yako kumpekua askari kabla hajakupekua ili asipandikize kitu.
13. Usipekuliwa nyumbani bila kuwapo kiongozi wa mtaa.
14. Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.
15. Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki salama.
16. Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.
17. Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.
18. Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.
19. Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.
20. Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.
21. Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.
22. Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo chini ya ulinzi.
SHARE KWA NDUGU, JAMAA NA MARAFIKI ILI WAZIFAHAMU HAKI ZAO
Mfariji Mkuu wa Taifa, Anatakiwa Akizungumza, Hasa Wakati Kama Huu Ambo Watu Wanatekwa, Wanateswa na Kuuawa,.. Raia Wema Wajawe Matumaini ya Usalama Wao na Watekaji Wajawe Hofu!! Hotuba ya Rais Haijafanya Hivyo Kwa Pande Zote Mbili!
โKama wewe ni mtekaji, baada ya kuiskiliza hotuba ya jana, umeingiwa hofu kwamba unatafutwa? Kwamba siku zako zinahesabika? Kwamba utakiona cha mtema kuni kwa uovu unaoufanya?โ amehoji Shangwe
https://t.co/YuadRmxWMi
Kila nikisema SOMENI hamtaki! SOMENI ibara ya 40(4) ya Katiba.
Makamu Rais akichukuwa nafasi ya URAIS kwa miaka 3 au zaidi hawezi kuomba kura kwa term 2 zaidi!
Come on people! SSH kachukuwa urais 2021 March. Ikifika 2025 atakuwa Rais kwa zaidi ya miaka 3.
Acheni kuvunja KATIBA!
Kwa kiapo hiki Cha RCO wa Kinondoni kwamba @ExMayorUbungo kwamba alimwambia ana hofu ya kutekwa na kuuwawa ,hivyo anyimwe dhamana Kwa sababu ya Usalama wake ! Mawakili wa Serikali wakasisitiza kuwa Polisi hawawezi kumlinda Kila alipo hivyo sehemu salama kwake ni Magereza!
Kama Mahakama ikikubaliana na hoja hizi ni wazi kuwa mtu akihofia Usalama wake hawezi Tena kwenda kuripoti polisi kwani POLISI watapeleka kiapo Mahakamani na kuzuia dhamana ili mtu huyo aende Gerezani !
Nasubiria kuona Mahakama ikiandika sheria mpya !
Jambo hili lilianzia kwenye kesi ya Kombo Mbwana Kule Tanga !
Viongozi wa Chadema wanaandikiwa utaratibu mpya wa kuwekwa mahabusu !
Ukihofia Usalama wako utaenda wapi ili uwe salama ?
Mahakama haikutakiwa kabisa hata kusikiliza hoja ya kiapo kwani haipaswi kuwa hivyo !
Long walk to freedom!
Tunaambiwa tusiseme kama unahofia Usalama wako ,ukisema sehemu Yako salama ni kuwa Gerezani !
Mahakama zetu zinatia aibu sana.Sishangai watu wakisema zinatumika na serikali. Mfano; kesi ya Kombo-Tanga; mpaka leo yuko ndani kwa kesi yenye dhamana. Kesi ya akina Soka mahakama kuu na maamuzi yake. Kesi ya Boniface mahakama imeshindwaje kutoa maamuzi leo eti mpaka jumatatu?