Heshima yako kaka John.
Naitwa Nyantori ni mwana CCM.
Ulikuja Serengeti sikuwa na hela ila naomba nitakutumia elf 25 uje uifikishe kwa mheshimiwa Lissu siku anasomewa hukumu atakunywa hata maji.
Hatuna hela ila tuna upendo na tunathamini mchango wake.
Damu yake
iliyomwagika pale AREA D DODOMA, itaabaki kuwa ukombozi wa taifa hili.
Mwambie tuna muombea sana.
IJUMAA KUU 2026. Mahubiri ya Baba Askofu Stephano yanastahili kusikilizwa na Watanzania sote bila kujali imani zetu tofauti kwani ufafanuzi na ushauri aliotoa unaweza kutusaidia kuleta taifa letu pamoja. UKWELI UTUWEKE HURU. TUJITATHMINI NA KUJIREKEBISHA.
https://t.co/ptTAuNKMpB
Tundu Lissu ni legal mind ya kipekee, anatumia precision ya constitutional law, evidence doctrines & human-rights instruments (ICCPR, African Charter) ku-dismantle kesi yoyote. Master of Legal Strategy; intellect yake ni above conventional jurisprudence. Hard to outsmart legally.
Pamoja na mafanikio makubwa uliyonayo;
Pamoja na elimu kubwa na uanazuoni ulionao; Pamoja na uwezo mkubwa kifedha ulionao;
Mwanao kujua ‘ki-lugha’ —lugha ya wazazi wako— haiwezi kuwa ushamba. Kwenda kusalimia kijijini ulikotoka sio umasikini. Kuitwa jina la ‘kinyumbani’ sio kuendekeza mizimu. Kulima bustani nyumbani sio kujitesa. Kula ugali mbogamboga sio kuishiwa. Kuingia jikoni na kupika sio umasikini.
Kuheshimu wasionacho sio kujishushia heshima. Kusalimia majirani sio kujipendekeza. Kutumwa na wasionacho sio kuidhalilisha familia. Kuomba msaada kwa jirani sio kujidhalilisha. Kuonywa na mtu mzima sio kuidhalilisha familia.
Kukosa anachokitaka haimaanishi huna fedha. Kuishi kwa bajeti sio umasikini. Kwenda ‘supamaketi’ akatoka na penseli na rula sio kukosa hela. Kujua mzazi huna anachoomba sio kujidhalilisha. Kusoma shule za ‘elimu bila malipo’ sio umasikini.
Mtoto kutandika kitanda chake sio ‘ukoloni’. Kufua nguo zake mwenyewe sio umasikini. Kuosha vyombo alivyotumia sio umasikini. Kudeki sio umasikini.
Kutokutumia gari yako kwa mambo yake binafsi sio kumsimanga.
Kutembea kwa mguu sio umasikini.
Kupanda daladala sio kudhalilisha familia. Kupanda bajaji sio hatari kwa usalama wake.
Mtoto kuitafuta hela yake mwenyewe sio kumtesa.
Watu wanapitia mengi sana ambayo hatuyaoni wala hawatuonyeshi usoni mwetu. Ukiwakuta watu wanafurahi ama kushangilia mafanikio yao hata kama ni madogo, ama ungana nao kushangilia, au wapishe washangilie. Kama wewe si sehemu ya maumivu yao, usilazimishe kuwa sehemu ya furaha yao.
Mmeamua kuchagua upande wa kutunyonya,kutukandamiza na kutuua haya ni maamuzi yenu na tumeyaheshimu..Heshimumi maamuzi yetu pia ya kuchagua kapambania haki, maana wanaotulipa ni watu wawili tofauti(mnalipwa na sisiemu tutalipwa na Mungu)
Nimepokea UJUMBE kutoka kwa WAPENDA HAKI mbali mbali ukinitaka NICHUKUE TAHADHARI, kwa kuwa mimi ni miongoni mwa watu WANAOTAKIWA KUPOTEZWA. Sasa, SIKILIZENI, mimi PETER MADELEKA, nawaambia ninaamini kwenye WAFILIPI 1:21. Kwangu, KIFO NI FAIDA.
"IF I DIE IN THE BATTLE FIELD TELL MAMA I DID MY BEST" ~ James Gikonyo, Kijana aliyeuawa katika Maandamano ya Gen-Zs nchini Kenya.
Mabadiliko yoyote yana gharama zake hasa yale ambayo yanahusisha mfanano wa rangi. Ikiwa kweli tunataka mabadiliko basi tusitarajie kama tutayapata kirahisi namna ile; Mzee Ali Mohamed Kibao, amelitimiza kusudi lake, alijitoa kupigania nchi yake na katikati ya vita uhai wake umetwaliwa na watesi wetu. Tuwe tayari kuyaona zaidi haya kwa maana ndiyo mbolea ya mabadiliko yoyote duniani. Tumlilie sana, ila tumwombee na kumpongeza kwa kujitolea kwake kuisema KWELI kwa ajili ya Taifa lake na vizazi VIJAVYO.
#ZuiaUtekaji #ZuiaUtekaji
#ZuiaUtekaji #ZuiaUtekaji
#ZuiaUtekaji #ZuiaUtekaji
Msitu bila miche michanga ni Msitu mfu, “Chinua Achebe” aliwahi kuuliza Swali iko wapi miche michanga itakayo chipukia? Baada ya ile migomba mizee kufariki? Dua yetu uwe Salama ndugu yetu hadi utakapoturudia 🙏
@MariaSTsehai@SuluhuSamia Haya mambo ya namna hii kila siku kwa kweli yanatia hasira na kuumiza mioyo,mbona hapo zamani ilikuwa ni unapewa wito nakwenda kuripoti mwenyewe kituoni.Huu utaratibu mpya wa kumkamata mtu kwa kumvizia namna hii na wengine kupotezwa kabisa haukubaliki na tusiukalie kimya aise
Malezi ya mtoto ni baba na mama. Kama hakuna sababu ya msingi, epuka kulea mtoto peke yako. Utandawazi usikudanganye kuwa unaweza kuwa baba na mama kwa wakati mmoja.
Mara nyingi changamoto kwenye familia zinatokana na mwanaume kukosa sifa ya kuwa kiongozi wa familia. Na hili linaweza kuanzia kwenye malezi, hivyo ni muhimu wazazi tusiwalee watoto kama tutaishi nao milele. Kuna siku nao watatakiwa kuwalea watoto wao.
Umepoteza Simu Hii Hapa njia Rahisi ya Kuipata Simu yako Bila Bila Kumlipa Mtu /Taasisi
Nazani jambo la kupotelewa na vifaa vyetu vya kielektronik linakera sana kwa maana ya thamani ya vitu vilivyomo
Kama umepotelewa twende pamoja katika mbinu hii ya kutumia email yako..