Soma kisa cha Nabii Musa AS ambaye katajwa zaidi katika Qur'an Kutokana na aina ya watu aliokutana nao hizi ni baadhi ya Surah na aya za kusoma Visa na Historia nzuri na zenye mafunzo makubwa toka kwa Nabii Musa AS,
1- AL KAHF
Hii ni surah ya 18 katika Qur'an surah hii iwapo mja ataisoma siku ya Ijumaa basi mja huyo atapata nuru kuanzia Ijumaa hiyo na ijayo, lakini pia inatajwa kuwa ni surah ambayo mja akiisoma mara kwa mara basi atalindwa na moto wa Jahannam, katika Surah hii kuanzia aya ya 60 hadi 83 tumeelezewa Namna Musa AS alivyoweza kutana na Mwalimu wake ambaye alitakiwa kumpa elimu aliitwa Khidhr na wengine wanamtaja kama Nabii Khidhr AS, utapata kujifunza mengi ikiwemo kuwa na uvumilivu katika kutafuta elimu na kufuata maelekezo ya mtoa elimu.
2- TAHA
Hii ni surah ya 20 katika Qur'an, ndani ya surah hii kimeelezewa sana kisa cha Nabii Musa AS, Allah anaanza kwa kuuliza "Na je! Imekufikia hadithi ya Musa?" Kisha anahadithia kuanzia pale Musa AS alipoona Moto na hapo ndipo alipopata utume wake, na baadaye Anapewa miujiza na amri ya kwenda kumuonya Firauni na watu wake, na kisha Allah SW anamkumbusha Musa AS kwa zile neema alizompatia ikiwemo kumlinda kutokana na adui yake na kulelewa na adui yake. Unaweza soma zaidi kuanzia aya ya 9 hadi 97.
3- ASH- SHUURA.
Ni surah ya 26 unaweza msoma pia Nabii Musa AS, kwa masimulizi yaleyale na ambayo yameelezewa kwa sehemu fulani zaidi kuliko surah nyingine iliyopita Allah SW, Kaanza kwa kumhadithia Musa AS pale alipofika katika bonde na kupewa utume na kumuomba Allah SW ampatie msaidizi ambaye ni ndugu yake kwa Jina la Harun AS, unaweza kupata kisa chote katika Qur'an kuanzia aya ya 10 hadi 67.
4- AL QASAS.
Hii ni surah ya 28 katika Qur'an na kuanzia aya ya 3 Allah SW alianza Kumhadithia Nabii Musa AS na makutano yake ma Firauni na kusimulia zaidi jinsi Musa AS alivyowekwa katika maji na kuingia katika nyumba ya adui yake na kulelewa humo na hadi kua kwake mkubwa na ikahadithiwa ni kipi kilitokea hadi Musa AS kukimbia mji wa Firaun na kwenda kuishi mbali na pale, na kwenda kuishi katika mji wa Madyaan.
Je ungependa kumsoma Nabii Musa AS? Basi fungua surah hizo tajwa na umsome zaidi.
@NakupendaAllah
@RevocatusMagum1 Hawa VIONGO ZI wa mpira baadhi utadhani wapo dunia nyingine au sayari nyingine, hapo nyuma ligi hii hii YANGA alikuwa anacheza yeye mwanzo halafu siku ya pili SIMBA anacheza na walikuwa hawasemi wala kuliona