@zittokabwe Dah! Ila wewe ndugu yangu, Zito pamoja na mwenzio Kafurila nikiwakumbuka enzi zenu mkiwa upande wa wananchi mkipambania haki na demokasia ya kweli nikiwaangalia sasaivi na mlivyo? Hakika Moto wa Jehnam hatoukwepa maana mme mezwa kanisa na shetani.
@PMadeleka Me nahisi hili neno UGAIDI kwenye Nchi yetu linatumiwa vibaya maana kwakweli mtu anaejua maana ya UGAIDI hakika tusingekuwa tukilitajataja midomoni mwetu.
@royalmediatz Mbona mheshimiwa Waryoba anaishauri vizuri sana Serikali ilipotoka, ilipofikia na ni nini kifanyike ili kunusuru Taifa letu takatifu? Au hujamwalewa nini sasa na hata juzi tu katoka kusema marekebisho muhimu makuu ktk katiba yetu.
Waziri Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapaswa kuheshimu ahadi zake kwa wananchi, akieleza kuwa kauli za kuunga mkono upatikanaji wa Katiba mpya hazipaswi kuchukuliwa kama kosa au fitina.
Warioba amesema hayo akizungumzia hali inayomkabili aliyekuwa Makamu wa Rais, Dk Emmanuel Nchimbi, akieleza kushangazwa na taarifa kwamba bado yupo kizuizini licha ya hatua za kinidhamu kuchukuliwa dhidi yake ndani ya CCM.
โMimi inanishangaza kidogo, nimekuwa kwenye chama, tunachukua hatua za kinidhamu lakini baada ya hapo mtu ni huru. Sasa ninaposikia kwamba yupo kizuizini bado sijaamini kwa sababu sijaona msingi wake,โ amesema Warioba.
Amesema suala hilo linampa wasiwasi kwa sababu CCM imewahi kutoa ahadi kuhusu Katiba mpya, hivyo mwanachama au kiongozi anayezungumzia utekelezaji wa ahadi hiyo hapaswi kuonekana kama anafanya jambo linalopingana na chama.
Kwa mujibu wa Warioba, CCM katika ilani yake iliweka suala la Katiba mpya, lakini baadaye Dk Nchimbi alipokutana na wanaharakati alihamasisha upatikanaji wa Katiba mpya mapema.
โCCM ni mwaka jana imetia Katiba kwenye ilani yake na baadaye Nchimbi alipokutana na wanaharakati akawahamasisha tupate Katiba mpya mapema,โ amesema.
Warioba amesema kinachompa wasiwasi ni taarifa kwamba miongoni mwa tuhuma zinazodaiwa kumkabili Nchimbi ni pamoja na kauli zake kuhusu umuhimu wa kupata Katiba mpya.
โHili linanipa wasiwasi sana na tutafika 2030 hatuna Katiba mpya,โ amesema.
Amesema hali hiyo inaweza kuleta mazingira ambayo viongozi na wanachama wanaogopa kusema ukweli kuhusu utekelezaji wa ahadi ambazo chama chao kimejiwekea.
Warioba amekumbusha pia kauli inayopatikana katika utamaduni wa CCM kwamba, โNitasema kweli daima, fitina mwiko,โ akisema kwa sasa kuna mazingira ambayo kusema ukweli kunaweza kutafsiriwa kama kuanzisha fitina.
โSiku hizi ukisema ukweli umeanzisha fitina, unaweza hata kususiwa,โ amesema.
Amesema Tanzania inahitaji mjadala wa wazi kuhusu Katiba mpya na utekelezaji wa ahadi zilizotolewa kwa wananchi, akionya kuwa iwapo mchakato huo hautapewa kipaumbele, nchi inaweza kuingia mwaka 2030 bila kuwa na Katiba mpya.