Politics Mwenyekiti wa Kamati ya Chadema Ni Msingi Kanda ya Serengeti. Katibu Chadema jimbo la kahama ,Mjasiliamali,Mpambaji wa shughuli za Harusi na Sherehe
KAHAMA — SHINYANGA.
Wananchi wameamua kwa uwezo na nguvu zao wenyewe kuchangia harakati za kisiasa za CHADEMA. Wananchi wanasema CHADEMA itaendeshwa kwa gharama za UMMA. TONE TONE tumepata kiasi cha TZS 2,700,700. Changia TONE lako kupitia 0744446969 – CHADEMA HQ
Msajili wa vyama, Sisty Nyahoza.
Mpango wowote muovu mnaoletewa na jaribio la kutaka kuzia chadema kufanya kazi zake au kukifuta chama chetu utabackfire vibaya.
Hatutakubali Chama chetu kiwe kibaraka wa ccm..
Tunajua Kesi ya Said Issa na vibaraka wengine ni ya kwako..
mahakama imetuondolea zuio umekuja tena.
Kauli ya Mwenyekiti wa vijana ccm kupoteza watu, na kweli watu wanapotea Popole, Mdude na wengine wamepotezwa.
Kauli za kina Makala za Mpox na Ebora.. kauli za mauaji na kuchinja watu za viongozi wa ccm .. Zipo nyingi
Je umewahi kuwaandikia ccm barua kuhusu hayo?
Acheni tushindane kwa hoja na ccm…
Ndio maana miongoni mwa mabadiliko, ambayo lazima yafanyike ni kufuta hii ofisi ya msajili inayotumiwa na ccm kudidimiza demokrasia.
NJIA RAHISI YA KUIFUTA CHADEMA: AANDIKA ASKOFU BAGONZA
Watu wengi uraiani, vijiweni na serikalini wameniuliza nitoe maoni juu ya hatua ya Msajili wa Vyama Vya Siasa kuiandikia barua Chadema. Barua hiyo inatafsriwa kuwa ina lengo la kuifuta CDM au kuifungia. Maoni yangu yanapendekeza njia rahisi na SALAMA ya kuifungia au hata kuifuta Chadema.
1. Niliwahi kusema kuwa “uchaguzi mkuu bila CDM ni sawa na kufikiria uchaguzi bila CCM”. Tumekuwa na uchaguzi bila CDM. Kila mtu anauhoji. Asiye mtu ndiye anaona ni kawaida.
Je twaweza kujaribu uchaguzi bila CCM? Nashauri tusionje sumu.
2. Wazo la kuifuta Chadema lipo. Nashauri twende njia ile ile ya uchaguzi lakini tubadili formula au mpangilio. Tuifute CCM na kubakiza CDM. Halafu tuishauri CCM kwa siri ili iombe radhi. CCM isamehewe na kurudi uwanjani.
3. Halafu tuifute CDM. Kwa “kiburi” chao watakataa kuomba radhi. Ifutwe moja kwa moja. Kwa njia hiyo CDM watakula jeuri yao na CCM watavuna matunda ya unyenyekevu wao.
4. Mpangilio huu unazingatia ukweli kwamba, CCM na CDM wote ni wababe. Mmoja ana bunduki na risasi, mwingine ana manati na mawe. Na hatuna utawala wa sheria ulio na miwani ya kuona madhambi ya CCM. Chadema inasaidiwa na dola ijione kuwa inaonewa. Ofisi ya Msajili-kipofu inahujumu maridhiano na amani ya nchi kwa kudhani inaikomoa CDM.
5. Tuliwahi kuvifuta TANU na ASP na kuzalisha CCM. TANU haikuwa na historia ya kumwaga damu lakini ikaungana ASP iliyokuwa na damu mikononi mwake. Mtoto CCM aliyezaliwa ana nini? Tukiifuta CDM itazaliwa ipi?
6. Mnaonaje tuifute TEC tubakize CCT!? Au tuifute BAKWATA tubakize Shura ya Maimamu au Answar Sunna?! Nayasema haya kwa sababu tumefeli kuishi kwa amani na tofauti zetu. Narudia kushauri WASAJILI WETU wafanye kazi ya kusajili siyo kuendesha taasisi wanazozisajili.
7. Tatizo siyo CCM, Wala CDM. Na tatizo siyo Rais SSH. Anaweza kuwa anaonewa na kuhujumiwa. Atazungumzaje maridhiano wakati watu wake wanakazana kufungia, kuteka, kukata vichwa, kuzuia mijadala nk? Tutagundua tumechelewa.
8. Tuna matatizo makubwa mawili: Fedha na hofu ya ukweli. Kwamba fedha zinunue utu, uhai, haki, teuzi, heshima, ukweli, chaguzi, na ajira. Halafu, kila mtu aogope kuonana wala kusikilizana na Ndugu UKWELI. Kuogopa ukweli kunatibiwa na kukubali ukweli.
9. Fedha/Rushwa imeingizwa katika vyombo vitakatifu mpaka mahekaluni. Ni tamu. Utamu huu unavifanya vyombo hivyo vitamani madaraka ili vilinde rushwa. Nashauri tuchore msitari, tuache rushwa. Tusipoacha, atainuka mtu anayekula rushwa lakini ameichukia. Atatutapisha hiyo rushwa. Mbona mnasahau upesi?!
10. Namba 1 mpaka 9 hapo juu yaweza kusababisha walio madarakani waogope kuondoka kwa kuhofia kulipwa kisasi. Wanaotafuta madaraka wanaweza kuwa wanapania wakiingia walipe kisasi. Hakuna mwisho bila kuweka msitari. Kisasi kina risasi.
Wajomba wa Kijaluo wana hekima isemayo, “Mwanamme mkalimu kupita kiasi husababisha watoto wa majirani wazaliwe wakimfanana”.
@YerickoNyerereT Tuzo ya haki hutangazwa Ila wewe Uko busy kujitamgaza kila siku. Tunajua umehongewa hela ili wakupe sasa pumzika Omba hata kazi za ndani ikilu sasa.
@Stany_Midea27@Jambotv_ Tuko imara sana ninyi mlikula Hela ya mwamba bila kumwambia ukweli kuwa watz wamekuchoka na michongo yako jiondoe kabla hawajakuondoa. Hata mama angemsikiliza Polepole leo asingepitia hapa
@Jambotv_ Kaka yangu Odero hebu tulia kwanza sisi hapo mezani harurudi bila kurudi na uchaguzi huru na haki.
Sisi hatuna viongozi tuliowachagua kwa sasa.