Unadhani unaweza kuwa na marafiki wangapi—watu wa karibu ambao unaweza kweli kuwaita marafiki? Ukiacha marafiki, unadhani unaweza kuwa na mtandao wa watu wangapi mnaofahamiana vizuri—mnapigiana simu, mnakutana, mnazungumza na juhudi nyingine za kuimarisha ukaribu wenu pasipo kujisikia unawekeza zaidi?
Robin Dunbar, mwana-athropolojia gwiji wa Uingereza, aligundua kwa mtu wa kawaida kuwa na uwezo wa kuhudumia zaidi ya marafiki watano wa karibu. Hasemi kila mtu hawezi bali wengi uwezo huo wa kuwa zaidi ya watu watano wanaoaminiana na kushibana hawana.
Lakini pia Dunbar haishii hapo. Haoni uwezekano wa binadamu wa kawaida kuwa na mawasiliano na watu zaidi ya 150 kwenye mzunguko wa watu anaofahamiana nao na hata kukutana nao mara kwa mara. Hawa ni watu ambao tunaweza kuwaita ‘wanamtandao’ unaoweza kuwatafuta hata kama sio watu wa karibu. Tizama mchoro ulioambatanishwa kwa uelewa zaidi.
Kama tarakimu hii ni sahihi, maana yake, kabla hujamlaumu mtu kwa ‘kukusahau’ fikiria kakutana na wengine wangapi na wewe ulikuwa kwenye duara lipi kwenye maisha yake. Dunbar anafikiri kadri mtu anavyokutana na watu wapya, ndivyo anavyolazimika kuwadondosha wengine ili apate muda wa kupumua kidogo—labda kama ana ubongo mkubwa kidogo kuliko sisi wengine, shauri ya mazingira yaliyokukutanisha na wengi tangu ukiwa mdogo.
Je, unakubaliana na namba hii ya Dunbar? Ingawa wapo wengi wasiokubaliana naye, kwa namna fulani, namba yake inasema kitu. Unaweza kuwa na kundi kubwa la watu mnaofahamiana kijuu juu lakini ukashindwa kujenga urafiki wa maana. Kwa upande mwingine unaweza kuwa na marafiki wachache wa maana kwa gharama ya kushindwana na kundi kubwa la watu. Mambo ni mengi na sababu ni nyingi.
Ila Tanzania 🇹🇿 bwana nchi kubwa yenye watu wengi ila sasa bado.
●Hakuna cable 🚡
●Hakuna Hovercraft 🛥
●Hakuna Metro 🚇
● Hakuna Intercontinental Airport 🛫
● Hakuna S&TRC 🏬
● Hakuna Data Center 🪩
Sasa Viongozi huwaga mnaingia madarakani kufanya nini?