Kuna wakati mamlaka huogopa zaidi wazo kuliko mtu. Na hofu hiyo hujificha nyuma ya nguvu, sheria, na vifungo lakini kiini chake ni kile kile woga wa ukweli usiodhibitika. Wanasema wanaogopa misimamo yako. Labda si wewe binafsi wanayeogopa bali kile unachowakilisha uhuru wa fikra, ujasiri wa kusema, na kukataa kuishi kwa masharti ya hofu.
Hata kupona kwako baada ya kupigwa risasi kwao lilikuwa kosa kwa sababu uliikataa simulizi ya mwisho waliyoitaka. Ukaendelea kuwa ushahidi hai kwamba si kila nguvu hushinda haki.
Sasa mwaka mmoja jela. Na ndani ya ukimya huo kuna kelele kubwa kuliko hotuba nyingi kelele ya dhamira isiyouzwa.
Ktk siasa nimejifunza kwamba wakati mwingine kuna biashara kubwa ya kuuza maneno. Lakini mara chache unakutana na mtu anayechagua gharama ya ukweli kuliko faida ya uongo.
Wewe ni mmoja wa wachache hao.Kwa sababu uhuru si kutoka gerezani tu bali ni uwezo wa kukataa kuusaliti ukweli hata unapouzwa kwa bei ya kuachiliwa. Basi jipe moyo mkuu. Historia huwa na kumbukumbu ndefu kuliko hofu za leo.
Na siku zote haki inapochelewa haifi.
God bless you.
The International Democracy Union (IDU) expresses its grave concern on the occasion of the first anniversary of the arbitrary arrest on April 9th, 2025 and the continued detention of Tanzanian opposition leader and IDU Bush–Thatcher Award for Freedom recipient Tundu Lissu.
Mr. Lissu’s arrest following a peaceful political rally, and the subsequent charges brought against him, lack a credible legal foundation and reflect a troubling pattern of political persecution aimed at silencing democratic opposition. Read more here:
https://t.co/Yuis75vRk3
#FreeTunduLissu #StandWithTundu #Tanzania
Today marks one year since Tundu Lissu was arbitrarily detained and denied his fundamental rights. Please share this and visit https://t.co/xskhqPZgUd for more information.
#FreeTunduLissu
—Admin