@capitanpapilon Shemasi alijichanganya alivyounga juhudi,vijana wa 4MC wakaanza kumnyuka wakiongozwa na Martin ...ile league ilikuwa moto,bado vijana wa hovyo wakaruka naye usiku na mchana..shemasi kilibaki kichwa tu mwili ulizorota sanaa!
Tatizo askari wetu wanahisi kama yakifanyika mabadiliko ya kiutawala au upinzani ukichukua nchi basi wote wataachishwa watakosa kazi!!
Upinzani hauji na askari wake jamani, upinzani hauna askari polisi wa kucover nchi nzima, askari mtaendelea kuwa nyie nyie na kazi yenu hamtapoteza.
Kinachopambaniwa hapo ni mabadiliko ya kimfumo, ili tuwe na mfumo bora unaosimamia na kutoa haki kwa raia na mali zake!!
Mfumo wenye maslahi na watanzania wote, watoto na wajukuu zenu na sio kikundi cha watu wachache!!
Ungeni mkono tulete mabadiliko na kwenu hamtapoteza ajira zenu!!
Power concedes nothing without a demand. It never did and it never will.
Kitendo cha hawa watu kukimbiza na kupeleka magari, hata kama ni kihuni bila mipango wala uendelevu wake.
Kinatufundisha mambo kadhaa wananchi wa Tanzania.
1. Tukiamua na tukawa na nia moja hakuna nguvu yoyote inaweza kutushinda.
2. Wananchi mkiamua kudai maisha bora, kukomesha wizi, ajira, maji, umeme, ulinzi na hata kukomesha utekaji hakuna anaeweza kuwazuia.
3. Wananchi tukiamua kudai mfumo huru wa uchaguzi na mahakama zinazotenda haki, tutafanikiwa na watawala watapiga magoti.
Tuendelee kudai Nchi yetu kwa nguvu zote kwasababu ni yetu sote, tudai haki ya maisha mazuri kwasababu dhahabu ni zetu weight, tanzanite ni yetu wote.
Hakuna anaestahili maisha mabaya na wachache maisha bora.
Tuamke.
#MAREKANI: KAMATI YA SENETI YA MAREKANI YAIONYA TANZANIA KUHUSU UKANDAMIZAJI KABLA YA UCHAGUZI
Kamati ya Mahusiano ya Kigeni ya Seneti ya Marekani imeeleza wasiwasi wake kuhusu ukandamizaji unaoendelea nchini Tanzania, ikisema hali hiyo inahatarisha imani ya wananchi katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29.
Katika taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa X, kamati hiyo ilitaja kesi ya uhaini inayomkabili kiongozi wa upinzani Tundu Lissu pamoja na msukumo mpana dhidi ya wakosoaji wa serikali na vyombo vya habari, ikionya kuwa hatua hizo zinadhoofisha uaminifu katika haki ya mchakato wa uchaguzi.
“Ukandamizaji na vitisho kabla ya uchaguzi Mkuu nchini Tanzania inapunguza imani katika haki ya mchakato huo, sawa na kesi ya uhaini dhidi ya kiongozi wa upinzani Tundu Lissu. Tanzania ni mshirika muhimu wa Marekani katika Afrika Mashariki, na maadili yetu ya kidemokrasia ndiyo msingi wa uhusiano huo.”
Hivi ndivyo watu wetu wanavyohangaika kupata hata sh 100 ya Kitanzania.
Alafu anatoa hapo visenti kidogo, kodi kila mahali, then kwenye bidhaa kodi.
Mtoto mdogo kama huyo anahangaika na mama yake kupata hata chakula, katika mazingira magumu, bila vifaa wala kinga.
Huyu binti ndoto zake zinaharibiwa, haendi shule sio kwasababu hapendi. Bali kwasababu watu waliotakiwa kuandaa future yake, wanapora future hiyo, kesho yake inaporwa na watu wachache Dar kwa jasho kubwa analotoa hapo.
Mtoto wa kiongozi amekaa mjini anacheza na pesa ya umma kwa anasa, hawezi hata kueleza hizo pesa anazochezea amezipataje!!!
Tutakomesha hii impunity.
Hakuna hila wala mpango wa giza utakaopangwa dhidi yangu utakaofanikiwa. Mimi sio mtakatifu mbele za Mungu hata kidogo,lakini angalau ninamjua Mwenyezi Mungu ninayemwamini. Kikao chochote mtakachokaa dhidi yangu kuanzia sasa, mtaadhibiwa na kufa. Kuanzia anayewaza, anayepanga na anayefikiri kutekeleza.
Baada ya Kupambana na Ma IT kurudisha Account ikashindikana tulishauriana na mwanangu kwamba hii kazi sio ya mtu mmoja Elon Musk inabidi apelekewe Nyuki ( Kikosi Kazi ).
Kikosi Kazi ni nyie Ma Familia kwasababu hamjawahi Shindwa jambo, moto mliopeleka Kuhakikisha hii Account inarudi sio tu Msaada ni Love kubwa kinoma na mmekuwa mkifanya hivi Many times.
Account ya Rasta imerudi ila anamalizia process za Verification kasema nije niwaambie Shukrani wanangu Love ni kubwa sana akirudi atawapa Gwala.
Alicho ahidi ni ataendelea alipoishia Fire ni lile lile. Tunajua wengine kabla hamjapost Biashara zenu, Post zenu, Memes zenu mli post kuhusu Account ya mwana kwanza, Bure kabisa.
BLESSED WAZEE Ngoja tutengeneze Mkeka wa Booom la Give Away Na Matreni Mitaa ichangamke.
Polepole anasemaga usidharau nguvu ya Umma.
TUTAKUWEPO🫵
One month to go hadi Oktoba 29
#Maandamano ya wananchi waliyopanga ikiongozwa na vijana imeamsha hisia nyingi
Nina jumbe nyingi za maaskari wa polisi na jeshi wakisema nao wamechoka 😓
Niliona awalli ni mmoja wawili na si watu niliowahi wasiliana nao - ila kwa sasa hadi watu ninaojua wako ktk mfumo
Ushauri uko wa kutosha na nimewaachia hapa msome!
Mi ninaamini kwa dhati kuwa watanzania walivumilia mengi chini ya @SuluhuSamia wakijua 2025 uchaguzi watamtoa kwa sanduku la kura!
Ila sasa hakuna uchaguzi ni uchafuzi tu na mifumo imebakwa!
Kila mtu amekata tamaa na Mama yao hapendwi! Nilionya zaidi ya mwaka mkasema ni chuki @ccm_tanzania
Sasa hii ghadhabu si yangu au ya watu wawili - nyie wenyewe mnaona
#TutaelewanaTu #NoReformsNoElection
Muuza matairi mtaa wa Livingstone alipataje pesa ya kununua vifaa vya sakafu na bafu kwa shs bilioni 2.4 🙄
Hii kuitetea haiwezekani ndo maana hadi QR code wame disable 😀
Machawa msilete ujinga na sarakasi! Nyie toshekeni na vijisenti semeni mitano tena acheneni na hii ishu - it is above your pay grade!
Huyu muuza matairi atakuja kujibu mengi!
Alafu vyombo vya ulinzi na usalama wahangaike na hawa wahujumu uchumi na si vijana maskini waliokuwa frustrated!
Eniwei #TutaelewanaTu
Wanatishia kutuua utadhani bila kupigania Mabadiliko hatutakufa.
Ukweli ni kwamba,kwa mujibu wa Website ya IndexMundi,watanzania 1075 wanafariki kila siku kwa Maradhi,Ajali na Umri.
Zaidi ya watu 30,000 watakufa kabla ya 29.10.2025 si kwa maandamano.
UKIZALIWA LAZIMA UFE,PERIOD!
🚨‼️WANAJESHI WALIOPO DRC WANAOMBA KILIO CHAO KISIKIKE‼️🚨
@gcumod mjumbe hauwawi nimepokea ujumbe huu na wanajeshi wamelia sana DM sina njia nyingine ya kuwafikishia
Wanajeshi huko DRC wamekwama wanashindwa kurudi zaidi ya mwaka - wanaomba wapewe haki ya kutembelea wapendwa wao!
Hawa wazalendo wasiteseke tunawathamini sana! Najua wahusika mtapata ujumbe na kufanyia kazi - ila msisubiri hadi hali ifike kuwa mbaya mpaka wanakosa pa kusemea wanajeshi wetu
Imeniuma sana 😭
Tujenge Taifa la wote na si la wanafamilia wanamtandao!
#WenyeNchiWananchi