ZANZIBAR: Waziri wa Maji, Nishati na Madini wa Zanzibar, Nadir Abdul Latif amesema Serikali inapanga kuanza kununua mchanga kutoka Tanzania Bara kwa ajili ya miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa visiwani humo.
Ameeleza hatua hiyo inalenga kukabiliana na uhaba wa mchanga Zanzibar na pia kupunguza athari za kimazingira zinazoweza kutokea kutokana na uchimbaji mkubwa visiwani humo.
Amesisitiza kuwa Wananchi wa Zanzibar wanaohitaji mchanga kwa ajili ya shughuli ndogo za ujenzi kama nyumba binafsi au utengenezaji wa matofali, hawatalazimika kununua mchanga kutoka Tanzania Bara.
Soma https://t.co/SSg3sxXePd
#JamiiForums #JFMatukio