Speed haina maana yoyote kama umepotea njia.. kuongeza speed wakati umepoteza muelekeo unapotea zaidi.
Akili ni kupunguza mwendo, kusoma ramani na kuchukua muelekeo sahihi.
Mwaka 1519 Kapteni wa kikosi cha wapiganaji 500 kutoka Hispania wakiwa na meli 11, kamanda Hernan Cortes walivamia Kisiwa cha Veracruz nchini Mexico.
Akijua fika vita ile itakuwa ngumu sana kapteni cortes aliamua kufanya kitu cha tofauti sana.Aliamuru wanajeshi wote washuke na manahodha pia.Baada ya hapo aliagiza meli zote zichomwe moto.
Zikiwa zinachomwa aliwauliza wanajeshi wake-"Manaona Nini?"
Wakajibu "Tunaona meli zinaungua".
Baada ya hapo akawaambia hii Maana yake ni aidha TUFE WOTE au TUSHINDE VITA lla hakuna kukimbia,Ingawa walikuwa kidogo kwa idadi kuliko maadui wao ila walishinda.
Watu wengi wanafeli kwenye maisha sio kwa sababu hawana uwezo wa Kushinda lla ni kwa sababu HAWAJACHOMA MELI ZAO ZOTE.
Hakuna "Determination" ya hali ya juu kupata wanachotafuta.Kama wewe HAUKO tayari kupoteza kidogo
ULICHONACHO ili upate kikubwa
UNACHOKITAFUTA,utabakia kama ulivyo.
Hii ni kwenye Siasa,mahusiano,biashara, kazi n.k
Kuna meli zinatakiwa zichomwe leo hata kama nikwamaumivu.
JIVIKE UJASIR!!
Uko tayari Kuchoma meli zako zote na uweke 100% ya NGUVU, AKILI na MOYO wako katika ulichochagua?
Have a nice weekend 🙏���
Ujumbe kutoka gerezani Ukonga wa Mh. Tundu Lissu
21/11/2025
Tume za Uchunguzi ni dekio la uchafu wa serikali na Jaji Mkuu Mohamed Chande ndiye msafishaji mkuu wa uchafu huo!!
Alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Mauaji Bonde la Ihefu mwaka 2006. Matokeo yake? Sifuri!!
Alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa Vyombo vya Haki Jinai Mwaka 2023. Matokeo yake? Sifuri!!
Sasa ni Mwenyekiti wa Tume ya Mauaji Makubwa katika historia ya nchi yetu yote. Tutegemee matokeo gani? Sifuri!!
Hakuna Maridhiano bila Ukweli na Uwajibikaji!
Hakuna Amani bila Haki.
TAL, Ukonga Central Prison.
-Admin.