Nimetoka Central police muda huu, niliambatana na Wakili @AdvMatata . Nimetaarifiwa na ZCO Msaidizi kuwa wanamshikilia Katibu wetu wa Kanda ya Nyasa @GraceShio03 na kwamba ‘taratibu za kipolisi’ zinaendelea. Hawajaturuhusu kumuona na wala kutuambia yuko kituo gani! Tunaendelea kufuatilia kwa usaidizi wa Wakili Matata.
Joseph Mbilinyi
Mkiti- CHADEMA Nyasa
#FREESHIO
Yani inaamua hivi—wapumbavu nao wanakuwa na maamuzi yao.
Nchi inaendeshwa kama familia ya KAMBALE kila mtu ana ndevu.
Safari ndefu na ngumu kinoma hii.🙌🏿
‼️HABARI MBAYA‼️
Katibu wa Kanda ya Nyasa, @GraceShio03 Mabiranga alichukuliwa juzi usiku na watu waliojitambulisha kuwa ni Polisi akiwa nyumbani kwao Kimara, Dar.
Mpaka sasa haijulikani yuko kituo gani na wala haijulikani amekamatwa kwa kosa gani!
#FreeGraceShio
KANISA KATOLIKI LIMETOA MAAGIZO YA TANZAZO LA MISA YA KUWAOMBEA WATU WALIOUWAWA OCTOBA 29.10.2025
Misa nchi zima, Kanisa limeagiza Kesho watangaziwe kwenye jumuiya ndogo ndogo, jumapili tutangaze kanisani, na wiki yote inayofuata Itakuwa ya kutangaziana
Chadema ni platform ni jukwaa la ku-adress haki,amani na kupinga ufisadi,utekaji,mauaji,utawala mbovu na sheria kandamizi, bila kusahau kutetea rasilimali za taifa.
Vijana wengi wanalitumia hili jukwaa ku~adress issues zao na pia vijana wengi wanapata relief kusikiliza hili jukwaa linavyo~adress issues zao!!
Utakapoamua kuifuta chadema isiwepo nchini ni umewapa alternative hawa vijana kwenda kutafuta jukwaa lingine la ku~adress na kusikiliza issues zao!!
Kasheshe ni pale hilo jukwaa lingine likawa ndio 🔥 🔥 🔥 na baya na hatari zaidi kuliko CDM.
Mtakuja kujuta ni kwanini mlimsikiliza aliewashauri muifute CDM!!
Sasa hiyo Tume ya Lila inafanya kazi gani kama wenzetu wanajua na wameshapeleleza watu wanaodai kuwa wahaini?
Polisi walioua raia mnasema wasubiri tume ya Lila ila wengine mnajiokotea na kuwapa kesi za kubumba, mnasema mnataka maridhiano, mtaridhiana na nani?
#29Octoba
Huyu kijana ni Mwenyekiti wa Chaso mkoa wa Mwanza, Manyama eti ameitwa Polisi Mwanza anatakiwa kuripoti saa saba leo mchana.
Msiogope wamebaki na UPUMBAVU wao kukamata na kutisha hawa @tanpol
Ndo maana Chacha alisema Polisi ni mali ya CCM na hakuitwa kujieleza
Ila #TutaelewanaTu
Tutakuwa tunaomboleza nini haswa hiyo siku?
Tunawaomboleza waliouawa na maiti zao kufichwa mpaka leo au waliouwa kikatili lakini mpaka leo wanatamba kwenye majukwaa as if nothing happened?🤔
MAJUKUMU YA CHAMA CHA WANASHERIA TANGANYIKA #TLS @TanganyikaLawSociety
Kifungu cha 4 cha Tanganyika Law Society Act kinaeleza madhumuni ya kuanzishwa kwa TLS. Haya ndiyo majukumu yake na mantiki ya kila jukumu:
1. Kifungu cha 4(a): Kulinda na kuboresha viwango vya maadili na elimu ya taaluma ya sheria.
Mantiki: Kuhakikisha mawakili wanazingatia maadili ya taaluma, wanaongeza ujuzi na kutoa huduma za kisheria zenye ubora.
2. Kifungu cha 4(b): Kuwezesha upatikanaji wa maarifa ya kisheria kwa wanataaluma ya sheria na watu wengine.
Mantiki: Kuendeleza elimu ya sheria, mafunzo na uelewa wa sheria ili wanataaluma na wananchi waweze kuitumia sheria kwa usahihi.
3. Kifungu cha 4(c): Kusaidia Serikali, Bunge na Mahakama katika masuala yanayohusu utungaji wa sheria, usimamizi wa sheria na utekelezaji wa sheria nchini.
Mantiki: Kutoa mchango wa kitaalamu katika maboresho ya sheria na mifumo ya utoaji haki ili sheria ziwe bora na utekelezaji wake uimarishwe.
4. Kifungu cha 4(d): Kuwakilisha, kulinda na kusaidia wanataaluma ya sheria kuhusu mazingira ya utendaji wao wa kazi na masuala mengine yanayowahusu.
Mantiki: Kulinda maslahi halali ya mawakili na kuwezesha wafanye kazi zao bila vikwazo visivyo halali, vitisho au kuingiliwa isivyofaa.
5. Kifungu cha 4(e): Kulinda na kusaidia umma katika masuala yote yanayohusu sheria au yanayohusiana nayo.
Mantiki: Kuhakikisha wananchi wanapata msaada wa kisheria, wanalindwa dhidi ya ukiukwaji wa haki na wanapata fursa ya kudai haki zao kwa mujibu wa sheria.
6. Kifungu cha 4(f): Kupata, kumiliki, kuendeleza au kuuza mali za aina mbalimbali, zinazohamishika au zisizohamishika, na kupata mtaji au mapato kutokana na mali hizo kwa ajili ya kutekeleza madhumuni ya TLS.
Mantiki: Kuiwezesha TLS kuwa na rasilimali na mali zinazosaidia kutekeleza majukumu yake na kuimarisha uwezo wake wa kifedha.
7. Kifungu cha 4(g): Kukusanya au kukopa fedha kwa ajili ya kutekeleza madhumuni ya TLS, kwa njia na kwa dhamana zitakazoamuliwa na Chama.
Mantiki: Kuiwezesha TLS kupata fedha za kuendesha shughuli zake na kutekeleza mipango yake kwa kuzingatia taratibu husika.
8. Kifungu cha 4(h): Kuwekeza na kusimamia fedha za TLS ambazo hazihitajiki kutumika mara moja, kwa namna itakayoamuliwa na Chama.
Mantiki: Kuhakikisha fedha za TLS zinatumika kwa busara, zinalindwa na zinaweza kuleta manufaa ya kifedha kwa taasisi.
9. Kifungu cha 4(i): Kufanya mambo mengine yote yanayohusiana na au yanayochangia kufikiwa kwa madhumuni yaliyotajwa hapo juu.
Mantiki: Kuiwezesha TLS kutekeleza shughuli nyingine halali zinazohitajika ili kufanikisha majukumu yake ya msingi.
Kifungu cha 4 kinaweka msingi wa uwepo na wajibu wa TLS. Kinaonyesha kuwa TLS si taasisi ya maslahi ya mawakili pekee, bali pia ina wajibu kwa taaluma ya sheria, Serikali, Bunge, Mahakama na wananchi kwa ujumla.
Utekelezaji wa majukumu haya unapaswa kuongozwa na sheria, weledi, uwajibikaji na maslahi ya umma.
UKWELI,HAKI NA UWAJIBIKAJI VITALIPONYA
#UKWELI#HAKI#UWAJIBIKAJI#
Women should eat cucumber frequently.
Cucumber contains chemopreventive nutrients which help reduce the risk of getting breast cancer.
Add it to your salads, smoothies or eat them raw. Nature heals.
Mwaka jana mlisema "kuna VYAMA 18 vya siasa nchini hata CHADEMA wakisusa Vingine vikakubali TUTATIKI kama kawa, kwasababu nyie ni wengi CHADEMA ni chama kimoja"
Mkasisitiza VYAMA 18 kweli viyumbishwe na msimamo wa chama kimoja? Mkajidai kwa mbwembwe kuwa mtatiki tuu na hakuna kitu watafanya.
BAADA ya kupata mlichotaka mwaka jana kwa thamani ya damu ya "Maelfu ya watanzania" leo mnarudi tena kuungana na kauli ya CHADEMA ya mwaka jana kabla ya OCTOBER 29 kutaka "Maridhiano".
Leo nyie ndio mnayahitaji MARIDHIANO kwa hali na mali, na mnafikia hatua mnawaona CHADEMA kama kirusi kwenye nchi kwamba hawapendi nchi itulie.
Nyie si mna vyama vyenu 18 ambavyo mlitiki navyo? Kaeni navyo mridhiane kama mnavyofanyaga mambo yenu mengine, na hao wakina ACT.
Kama mnaitaka CHADEMA mezani lazima meza yenye damu za MAELFU YA WATANZANIA isafishwe ing'ae ndio tukae chini. Vigezo vya kusafisha MEZA YA MAZUNGUMZO vilisemwa na vinajulikana acheni kona kona.
Kinyume na hapo, hatupo zama za SIASA ZA MASAJI, endeleeni kuzungusha sketi tumekaa pale.
@mangekimambi Maana halisi ya UZALENDO ndani ya hii nchii imebadilishwa maana, na inatumika vibaya sana.
Wao wanaamini UZALENDO ni kuipigania na kuilinda nembo ya chama na UHAINI ni kusimama katika ukweli.
Inasikitisha sana na safari ni ndefu sana 😥🚶🏾♂️
Kama unafuatilia vizuri Siasa za bongo kwasasa inatumika nguvu kubwa sana kufosi CHADEMA waingie kwenye MARIDHIANO.
Wapo nje ya muda, wanaona kabisa CHADEMA bila nguvu ya ziada hawa wanashikilia bomba.
Kwahiyo utaona press nyingi sana kuelekea November kuihusu CHADEMA kwamba hawaitakii mema nchi.
Wanasahau CHADEMA ndio walikuwa wahubiri wa MARIDHIANO kabla ya MO29 ila wao wakasisitiza wanatiki.
Sasa wamemaliza KUTIKI wanataka wasikilizwe wao. Huo upumbavu ulifanikiwa zamba za MBOWE sio sasa.
MUSIOGOPE!
Yesu ninayemwamini ndiye Njia, Kweli na Uzima. Taifa letu linahitaji UKWELI, HAKI NA UWAJIBIKAJI.
Amani ya kweli haipatikani kwa kuua, kutisha au kutumia vibaya mamlaka ili kumnyamazisha Boniface Mwabukusi. Amani ya kweli hujengwa kwa kutenda haki, kuheshimu utu na kuwajibika kwa matendo yetu.
Kwangu mimi, kuishi ni Kristo, na kufa ni faida. Ni bora nikose vyote, lakini nibaki upande wa wanyonge wanaonyanyaswa, wanaodhulumiwa na kupuuzwa katika harakati za kutafuta haki.
Mungu ninayemtumikia ni Mungu wa haki. Hata tukipita tena na tena katika bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya, kwa maana najua kuwa makusudi ya Mungu yatasimama.
MUSIOGOPE! Ukweli unaweza kucheleweshwa, haki inaweza kuzuiwa, na sauti ya mtu inaweza kutaka kunyamazishwa, lakini hakuna mamlaka ya mwanadamu inayoweza kuishinda kweli ya Mungu.
Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa.” — Mathayo 6:33
UKWELI. HAKI. UWAJIBIKAJI.
Mungu mbele, hofu nyuma, na haki daima!
HAKI ITASHINDA.
BAK MWABUKUSI .
MSHARIFU
Waingereza wanaita “Life plant” maarufu kwa jina la “miracle leaf” kisayansi unaitwa “Kalanchoe pinnata”.
Kuna siri gani katika mmea huu mpaka ukaitwa life plant (mti wa uzima)? Huu ni mmea wenye uwezo wa kutibu maradhi mengi na kwa muda mfupi.
Leo tuangalie faida zake kuanzia majani hadi mizizi yake.
MAJANI YA MSHARIFU
🍃 Hutibu maradhi ya sikio kiujumla
🍃 Hutibu presha ya kupanda
🍃 Dawa nzuri ya watoto waliokunywa maji tumboni wakati wa kuzaliwa.
🍃 Dawa nzuri kwa kukausha vidonda
🍃 Dawa ya watoto waliobemendwa
🍃 Dawa ya vidonda vya tumbo
🍃 Dawa ya kansa; inazuia ukuaji wa seli za kansa
🍃 Hutibu maradhi ya njia za hewa kama vile pumu.
MATUMIZI
Chemsha majani yake kunywa, chuja, kisha kunywa mililita 200 mara tatu kwa siku.
MIZIZI YA MSHARIFU
🌱 Dawa ya uvimbe aina zote tumboni
🌱 Dawa ya kifua kubana
🌱 Dawa ya miguu kuvimba
🌱 Dawa ya miguu kufa ganzi
🌱 Dawa ya miguu kuwaka moto
🌱 Inabalansi kiwango cha sukari
🌱 Hutibu maradhi ya figo (mawe kwenye figo)
🌱 Dawa ya kikohozi
MATUMIZI
Chemsha mizizi tumia kunywa kwa glass moja asubuhi na jioni.