Hafla ya ufunguzi Mkutano wa 31 wa Baraza Kuu la Shirika la Viwango Afrika (ARSO), Mgeni rasmi alikuwa ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Hemed S. Abdulla na kuhudhiriwa na viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi, uliofanyika Hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar.
Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Bi. Fatma M. Khamis akiongoza kikao kati ya Wizara na Maafisa kutoka Benki ya Equity ya Tanzania waliofika kwa lengo la kuimarisha mahusiano na mashirikiano katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Wizara Kinazini Zanzibar
Aidha Tamasha hilo, lenye kaulimbiu “Ni Wakati wa Pemba” ikiwa ni jukwaa muhimu lenye lengo la kukuza Biashara na Viwanda kupitia fursa zilizopo nchini.
@ya_idara@zstcznz
Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar, Mhe. Omar S. Shaaban atashiriki Tamasha la Uwekezaji Zanzibar 2025 (ZIS) linaloandaliwa na ZIPA litakalofanyika Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba kuanzia tarehe 15 hadi17 Juni, 2025
Aidha ziara hiyo, Bi Fatma aliambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Mngereza Mzee Miraji, Mkurugenzi Idara ya Utumishi na Uendeshaji Kassim S. Ally na Watendaji kutoka Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda.
Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Bi. Fatma M. Khamis akiwa katika ziara ya ukaguzi wa Kiwanda cha kuzalisha mafuta ya nazi Saateni, Ghala la kuhifadhia Saruji Saateni na amekagua eneo la kuzalisha Organic Spice(ZATOP) lililopo Mwanakwerekwe Wilaya ya Mjini
Akitoa taarifa Mkurugenzi Idara ya kumlinda Mtumiaji na Udhibiti wa bidhaa bandia nd. Aliyah E. Juma amesema, baada ya ukaguzi katika maghala wamegundua bidhaa zilizoharibika na wameziteketeza kwa mujibu wa sheria. Pia, Tume imewataka Wananchi kuwa makini wakati wa kununua bidhaa
Tume ya Ushindani Halali wa Biashara (ZFCC) imelazimika kuziangamiza tani 15 za bidhaa za vyakula vilivyomaliza muda wake ikiwemo Backing Powder, Chumvi, Maharage, na bidhaa nyengine zenye thamani ya TZS. Milioni 10 katika Jaa la Kibele, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
Mhe. Dkt. Hussein A. Mwinyi katika uzinduzi wa sera ya Biashara 2024 na tathmini ya uimarishaji wa mazingira ya biashara 2025, ukumbi wa New Amaan Hotel na alikabidhiwa kitabu cha sera hiyo kutoka kwa Waziri wa Biashara Mhe. Omar Said Shaaban na kuahidi kuitekeleza kwa vitendo
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imedhamiria kuifanya Zanzibar kuwa Kituo bora cha biashara katika Sekta ya huduma Afrika Mashariki na Kusini ikizingatia mifumo ya Kitaifa, kikanda na kimataifa
Hayo yamesemwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Mkurugenzi Mtendaji wa ZNCC, Bw. Hamad Hamad amesema Sekta Binafsi hasa Sekta ya Utalii, Uchumu wa Buluu, Viwanda, na Sekta ya Kilimo zitashiriki katika maonesho ya Biashara ya Expo 2025 yanayofanyika Mjini Osaka Nchini Japan kuanzia Aprili 12 hadi Oktoba 13, 2025.
Akizungumza katika kikao cha Maandalizi ya Japan Expo 2025, Ukumbi wa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu Mazizini , Bw. Hamad amezihamasisha Sekta nyengine hasa wakulimwa wa Mwani, wafugaji wa majongoo na wanaojihusisha na Uchumi wa Bahari kushiriki maonesho hayo ili kuongeza thamani.
Wakati akitoa taarifa kwa Waandishi wa habari kuhusu ushiriki wa Tanzania katika maonesho hayo yaliyoanza 12 Aprili hadi 13 Oktoba,2025, Dkt. Hashil amesema fursa za Maonesho haya yana faida kubwa sio kwa Tanzania tu bali duniani kote na zaidi ya nchi 160 zimethibitisha kushiriki
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara wa Tanzania Dkt. Hashil T. Abdallah amesema ushiriki wa Tanzania katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara, 2025 nchini Japan kutachochea fursa mbalimbali za Wajasiriamali, Wafanyabiashara na Wawekezaji kuimarisha ukuaji wa uchumi nchini.