Huyu Johari ndo chanzo cha kuwapa watu mashtaka ya uhaini na ugaidi na kesi ya Lissu - ye ndo anaisukuma kisheria kupitia ofisi ya DPP!
Ila mwisho wake umefika pia!
Mungu aendelee kukulinda Dada wa Taifa @mangekimambi
Na hawa walioenda na Johari - Kombo na Nyalandu - mtalipa haya maovu!
Mungu atutangulie katika yote but we have to fight 👊🏽🔥
#SamiaMustGo
Stop whatever you are doing! Listen up #Tanzania
Vita hii tutashinda - #KatibaMpya ni ile inayotokana na Rasimu ya Warioba!
Tupo tayari tumejipanga✊🏽🔥
Hatutaruhusu uhuni wa Samia Suluhu na genge lake! Asante kwa taarifa Dada wa Taifa 🙏🏽
‼️JAJI NDUGURU HAKUAZIMISHWA, ALISHIRIKI KWA HIARI KUANDIKA HUKUMU‼️
Taarifa niliyopata ni kuwa Jaji Ndunguru alizunguka kuulizauliza kuhusu cognate offense (yaani kosa dogo) la uhaini. Aling’ang’ania kuwa South Africa treason yaani uhaini Ina makosa madogo. Kwa SA ni kweli kosa linaendana na sedition na incitement lakini aliambiwa na kila aliyemwuliza kuwa kwa Tanzania hakuna kitu kama hiki. Akagoma kusikiliza sasa KAUMBUKA! 🙄
Sasa shida yeye ni mwenyekiti wa jopo na shida kubwa kwa sasa Tanzania hamna dissenting opinion, la sivyo hivyo kuna jaji au majaji wangeweka hukumu tofauti. Na ndiyo maana hukumu zilikuwa mbili. Ile inayomwonyesha Ndunguru peke yake ilivuja kabla ya kupandishwa Tanzilii, ilikuwa ni ya mfumo wa ndani wa mahakama. Hiyo ndo ilikuwa nakala yake aliyotii maelekezo ya Abdul!
Ila uzuri Haki itashinda na washiriki wote wa dhulma watajulikana na kuwajibishwa!
#FreeTunduLissu
UCHAWI UPO:
HUKUMU rasmi ya Mahakama Kuu👇, inaonesha kuwa; Kesi ya UHAINI dhidi ya TUNDU LISSU ilisikilizwa na JAJI MMOJA TU. Angalieni AKIDI (Coram) hapo chini. Kumbe wale MAJAJI wengine WAWILI waliokuwa WAKIONEKANA pale Mahakamani ilikuwa ni “EIAI”. 😂😂
DPP Mwakitalu na mahakama ya Tanzania chini ya Jaji mkuu Masaju.
Mnafuta mfumo wa vyama vingi vya kisiasa Tanzania, kwa kutumia ofisi ya DPP na mahakama za Tanzania.
Mnawafungulia wapinzani wa kweli wa ccm na Samia, kesi za uongo za Ugaidi na uhaini na kuwafunga kwa hila.
Ni wajibu wetu Watanzania kukataa kurudishwa kwenye mfumo wa zidumu fikra za Mwenyekiti wa ccm.
Kikubwa zaidi historia itakuandika Mwakitalu na Masaju mnavyopaswa kuandikwa.
MAJAJI WANOJIELEWA 👇:
Tanzania tuna MAJAJI WANAOJIELEWA SANA 👇 ambao WALISEMA kosa dogo (COGNATE OFFENCE) ni lazima LIWE NA UHUSIANO NA KOSA KUBWA). Sasa, kwani UHAINI una uhusiano wowote na UCHOCHEZI? Jamani, UCHAWI UPO.😂
‼️EXCLUSIVE‼️
Wale ambao hamkuweza kufika Mahakamani November 6, 2026 na mlitamani kumsikia Mhe. Lissu wakati anawashona Majaji kabla hawajasoma “Hukumu waliyopewa”.
Nimewaletea full clip ya Dakika 56 za Mhe. Lissu aisee ni noma na nusu.🙌
#FreeTunduLissu
@raiyajenerali , najivunia sana kuwa mke wako!!! ❤️😘💕 Umejitokeza na kusimama kidete kuhesabiwa kudai haki, ukweli na uwajibikaji. Hapa hakuna uchawa chawa!!! Najivunia kwamba wewe si kama wale majaji wa Mahakama Kuu wanaouza utu na heshima yao kwa vipande thelathini vya fedha… Hao tuwaogope kama ukoma!!!
Ni suala la muda tu. Tutarudi tulikotoka na kuwa tena taifa lenye utu na heshima, linalosimamia ukweli, ambako haki ni ya kila mtu na kila mwenye mamlaka anawajibika kwa wananchi.
TUNDU LISSU ATUZWA NA ULIMWENGU KWA
KUPIGANIA DEMOKRASIA.
Bunge la Ulaya limemtunza Mwenyekiti wa Chama cha
CHADEMA nchini Tanzania Tundu Lissu, tuzo la mwaka huu la
SHAKHAROV.
Lissu ambaye Kwa Sasa anatumikia kifungo cha 4 jela amepewa Tuzo hilo kutokana na juhudi zake za kutetea
Demokrasia na usawa nchini mwake.
Thanks so much the @europeanunions@Europarl_EN 🙏
DAKTARI Aliyeongea Leo Kwenye Msiba Wa ALUTE MUGHWAI Huyu Hapa.
DAKTARI Aliyempokea TUNDU LISSU Akiwa Mahututi Baada Yakupigwa Risasi Nyingi Sana “LISSU Alikua Na DAMU 3”
Week Kadhaa Mbele DAKTARI Huyu Akafukuzwa Kazi.
Msikilizeni Doctor Akimsimulia TUNDU LISSU Tukio Zima 👇
VIDEO:
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, ametoa wito kwa viongozi wa dini kuacha kuwapa sakramenti watu wanaojihusisha na ukandamizaji na badala yake waanze kuwafukuza kanisani na misikitini.
Mwabukusi ametoa wito huo leo mkoani Singida alipokuwa akitoa salamu za rambirambi katika msiba wa Alute Mughwai Lissu.
Ameeleza kuwa kanisa limekuwa mwepesi kuwahukumu watu wanaotenda dhambi zingine kama vile uzinzi, lakini wanaowakandamiza wenzao wamekuwa wakiachwa wakiendelea kupata huduma za kiroho bila kukemewa.
Katika hatua nyingine, Mwambukusi amesema chama hicho kinashirikiana na mawakili wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu kwa kuzingatia maelekezo ya Lissu mwenyewe ili kushughulikia kwa haraka maombi yake ya dhamana na usikilizaji wa rufaa dhidi ya hukumu yake.
"Sisi kama TLS tutaendelea kuwasiliana na familia yake kwenye hatua zingine zinazofuata lakini vilevile tutashirikiana na mawakili kwa kuzingatia maelekezo ya Tundu Lissu mwenyewe. Sisi Baraza la Uongozi na mawakili wake Tundu Lissu kushughulikia swala la rufaa kwa haraka lakini vilevile maombi yake ya dhamana huku tukisubiri usikilizwaji wa rufaa," ameeleza.