Tangu Mwenyekiti wetu akamatwe mwezi wa nne,
Leo ni miezi 11.
Watanzania wanajua na Dunia inajua kwamba Lissu hajafanya kosa, kesi hii ni ya uongo kwaajili ya kulinda Utawala usio na ridhaa, kutishia watu na kutaka tusitimize wajibu wetu kama chama kikuu cha siasa Tanzania.
Tangu mwezi wa 10 mwaka 2025, Mwenyekiti alikaa Magereza kwa zaidi ya miezi minne bila kesi kuendelea huku akiteseka bila sababu yoyote.
Tunajua hii kesi imefunguliwa kumtesa kiongozi wetu ili abadili msimamo wake kuhusu mambo ya Nchi yetu… kuhusu ufisadi wa serikali ya Samia , mauaji, utekaji, wizi wa mali za umma, maisha mabovu na uchumi wa hovyo kwa watu wetu… Tunajua anateswa kwasababu yetu Watanzania.
Rufaa ya juzi kwa mambo yasikatiwa rufaa ni ushahidi mwingine kwamba hakuna kesi bali kumpotezea Mwenyekiti muda wake na kumtesa..
Huu ni mwezi sasa Mahakama iko kimya, tunajiuliza kesi yenye uzito kama huu kwa mtu ambae amekaa ndani mda wote huu.. inakuaje mahakama isione urgency kwenye jambo hili..
Mahakama iliyotegemewa kutoa haki na kumaliza jambo hili kwa haraka, inapokaa kimya kunakua na mashaka makubwa..
Sisi hatuwezi kuendelea kunyamazia suala hili.
Tunataka huu uhuni ukome haraka , Mwenyekiti wetu aachiwe arudi kufanya wajibu wake.
Wanachama wetu na Watanzania hawataendelea kukalia kimya uonevu wa wazi kwa mtu asiye na hatia.
Mungu mwenyewe ana penda sifa na Kupendwa .
Daa enewei ...kama haiku uumi ungenyamaza ni vema tuheshimu dhamana na tuheshimu hisia za wananchi wanao tusikiliza hata kama hawatuelewi na hatuamini kuwa walituchagua.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo February 18, 2026
Jana tuliishia Part 191 so leo tunaendelea na-;
Part 192
Kesi inaanza muda huu Majaji na Mshitakiwa wamefika.
Mawakili wa Serikali pia wapo tayari.
Hali ya hewa ilikuwa ya mvua kwahiyo mahudhurio sio makubwa ya watu hapa Mahakamani.
Tupo hapa kuwaletea updates kama kawaida.
Anasimama Renatus Mkude anasema wanae shahidi mmoja lakini shahidi mwingine anayefuata amefiwa na Mkwe wake kwahiyo leo tunae shahidi mmoja.
Anasimama Lissu anasema kama amepata msiba ni wazi hawezi akaja.
Mimi niko tayari kuendelea na shahidi aliyepo lakini tulikubaliana angalau waje mashahidi watatu kwa siku.
Nasema hayo sio kwasababu sitaki watu waende msibani ila nasema ili tujue ni muhimu tukatumia muda vizuri ili wasio kwenda msibani tubaki nao kufanya kesi.
Anasimama Renatus Mkude anasema hili ni jambo la kibinadamu tunaomba na sisi mawakili wa serikali twende pale kumcomfort mwenzetu.
Jaji Mshitakiwa unasemaje?
Mhe. Tundu Lissu sijawahi kuwa na roho mbaya kiwango hicho kukataza watu wasiende msibani, kama wao wameona kuna umuhimu huo wa kwenda.
Jaji anasema basi tuendelee.
Renatus anasema shahidi tuliyenae ni P7 na ataongozwa na Thawabu Issa Wakili wa Serikali.
Shahidi analetwa anaingizwa kwenye kibox chenye joto. 😂
Jaji anauliza una miaka mingapi?
26 ninayo.
Dini yako?
Mkristo.
Anaapishwa hapa Shahidi.
Wakili wa Serikali Thawabu Issa anaanza kumuhoji shahidi hapa.
Wakili: unajishughulisha na nini?
Shahidi wa kificho P7 : Dereva bajaji nafanyia kwa Morombo kule Arusha toka 2023 nafanya kazi hiyo.
Wakili: Hapo kwa morombo pakoje?
Shahidi wa kificho : Kuna watu wengi sana. Kuna maduka na watu wanafanya biashara hapo. Ikiwemo maduka ya mahitaji ya nyumbani.
Wakili: Tarehe 03/04/2025 kuna nini kilitokea?
Shahidi wa kificho : hiyo tarehe majira ya jioni nilikuwa kijiwe cha kwa morombo Arusha. Tulikuwa hapo kijiweni na tunafanya mazungumzo ya kawaida.
Wakili: Ikawaje?
Shahidi wa kificho : Kuna mwenzetu akasema hamjasikia Chadema wamesema watazuia Uchaguzi wa Mwaka huu. Wamesema watakinukisha mbaya. Alikuwa anatuelezea huyo mtu.
Wakili: kingine ni nini?
Shahidi wa kificho : Akasema kuwa Polisi wanaiba kura hata ukienda Mahakamani hautapata haki.
Wakili: Kikaendelea baada ya mtu huyo kusema?
Shahidi wa kificho : Akasema pia Majaji ni vibaraka wa CCM, akasema pia mwaka 2024 tume ya Uchaguzi ilipewa maelekezo ya kukata wajumbe wa Chadema. Tukiwa tunaendelea na hayo mazungumzo nilipata hamasa kupitia hayo maneno niliyosikia akisema yule Bajaji mwenzangu.
Wakili: Sasa weka vizuri, wewe ulifanya nini?
Shahidi wa kificho : Niliingia kwenye mtandao wa youtube na mimi niweze kujionea hayo maneno. Nilitumia simu yangu na kuingia channel inaitwa Jambo. Simu ya janja.
Wakili: Nini kiliendelea?
Shahidi wa kificho : Nikafungua channel ya Jambo na kukuta yale maneno kama nilivyoambiwa hapo kijiweni.
Wakili: Nini kikaendelea?
Shahidi wa kificho : Baada ya dakika chache kuna watu wakaja wakajitambulisha kama wao ni maaskari na baadae watu walikimbia tukakamatwa mimi na P4.
Wakili: kilichoendelea hapo?
Shahidi wa kificho : Tukapelekwa kituo cha Polisi Murieti. Tulikaa kama Dakika 45 tukapelekwa kituo cha Polisi Central Mjini.
Wakili: baada ya kuwa umepelekwa Central ikawaje?
Shahidi wa kificho : Tukaingizwa Ofisi ya RCO nikaambiwa nashitakiwa kwa kosa la kutaka kufanya fujo, niliandikwa maelezo na kuingizwa Mahabusu na asubuhi yake ndugu zangu walinifuata nikazaminiwa na kupewa tarehe za kuwa naenda kuripoti kwenye hicho kituo cha Polisi.
Wakili: Nini kilifuata?
Shahidi wa kificho : Nikawa naripoti kwa mujibu mpangilio wa hiyo ratiba na ilipofika Tar. 17/04 2025 baada ya kufika kuripoti kama kawaida, nikaambiwa naandikwa maelezo upya.
Part 193 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba repost yako.
Rais ambae unajifanya umechaguliwa na unapendwa na wananchi unatekwa na Taifa jingine..
Alafu hao wananchi uliokua unadai wanakupenda wanatoka kwa mamilioni kushangilia wewe kutekwa…
Ulinzi wa uhakika wa kiongozi ni ridhaa ya wananchi na kukubalika kwa umma wala sio bunduki.
X Familia, kelele kwa Buyobe hazitoshi, tuongeze nguvu ya kupaza sauti na kumpigania haki ikatendeke kwake!!
Huyu ni ndungu yetu kabisa!!
Be safe chafu yangu @fbuyobe damu ya Kristo ikakufunike!! Nakuombea🤲
Bwana Jaji mkuu Masaju, Mahakama ikiwa huru itajisemea kwa matendo yake na hukumu zake..
Mahakama huru inazuia chama cha siasa kufanya kazi zake Nchi nzima kwasababu mtu anadai mali!!!!!!
Naona unahangaika kusisitiza Amani!!! Wewe unapaswa kusisitiza haki kwasababu muhimili wa mahakama ni kwaajili ya haki… Acha siasa za Amani tena haki Amani itakuwepo yenyewe.