Chama cha Wananchi - CUF kinaamini Mabadiliko sahihi ya Mfumo wa nchi hii ni #KatibaMpya.
Kwetu sisi Tunaamini Katiba Mpya chini ya maoni ya Rasimu ya 2 ya warioba ndio hitajio la msingi kuelekea ulinzi wa mabadiliko ya kweli ya nchi hii ikiwemo suala la Tume huru ya Uchaguzi.
Leo tarehe 25 Septemba 2023 Mwenyekiti wa #TCD, Mhe. Prof. Ibrahim Lipumba ameongoza Kikao cha Faragha Cha Viongozi Wakuu wa vyama vya Siasa kujadili marekebisho ya Sheria za vyama kuelekea Uchaguzi wa serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu katika Hoteli ya Madinat Al Bahr Zanzibar.
Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Chama cha Wananchi CUF Wilaya ya Kasulu wakati wa uzinduzi wa Jukwaa la Majadiliano ya Vyama vya Siasa Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma.
Lengo la majadiliano haya ni kukuza, kuimarisha na kudumisha demokrasia ya siasa ya vyama vingi nchini.
Katibu wa Vijana Wilaya ya Kigoma Mjini kutoka Chama cha CUF, Bw. Victor Raphael Sakejo leo tarehe 24 Julai 2023 ameshiriki uzinduzi wa majadiliano ya vijana kuhusu #Sheria ya Vyama vya #Siasa, Sheria ya #Uchaguzi na Mzunguko wa Uchaguzi.
Majadiliano haya yameandaliwa na TCD
Chama cha Wananchi #CUF kinakupongeza Mwenyekiti wa chama Taifa kwa kuchaguliwa kushika madaraka ya Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) @TCDemokrasia
Uongozi na Wafanyakazi wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) unapenda kutoa pongezi kwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Mhe. Prof. Ibrahim Lipumba kuwa Mwenyekiti mpya wa TCD pamoja na Mwenyekiti wa NCCR - MAGEUZI, Mhe. Haji Ambar Khamis kuwa Makamu Mwenyekiti wa TCD.
Mh. Rais @SuluhuSamia na Waziri @MbarawaM , Prof. Lipumba ameuliza swali la msingi sana kuhusu mkataba wa bandari. Kama lengo lilikuwa kuimarisha uendeshaji wa bandari ya Daresalaam, ni nini kilichosababisha kukawa na mkataba baina ya Serikali ya Dubai na Tanzania? 🤔
Kwa nini hapakuwekwa zabuni ya wazi kisha makampuni mbalimbali yanayoendesha bandari yakashindana kisha tukampata mmoja, hata kama ni DP World?🤔
Chama cha wananchi
#CUF kimeishauri serikali kuunda timu ya waaalamu mbambal ambao ndani yake kutakuwa na wanasheria kwa ajili ya kupitia upya mkataba baina ya serikali ya Tanzania na Kampuni DP World unaolenga kuendeleza bandari ya DSM.
Prof #Lipumba ametoa ushauri Leo
"Mipango iliyoelezwa kwenye bajeti ya mwaka jana kama,Mapitio ya utekelezaji wa bajeti haijaeleza ulimaji wa alizeti Mtanana umefikia wapi?.Hotuba inarudia rudia sana kumsifia Rais Samia mpaka inaleta ukakasi kuwa ni kejeli kuliko sifa.Sifa hizo ni pamoja na Mama ameupiga mwingi
"Ukitumia kigezo cha kimataifa cha Umaskini,43.4% ya Watz ni masikini. Kwa kigezo za nchi yenye kipato cha kati cha chini 73.2% ni maskini na kwa kigezo cha kipato cha kati cha juu 90.8% ni maskini. Wimbo wa kuwa Tanzania ni nchi yenye kipato cha kati ni mzaha kwa Watanzania"
Mh. Rais @SuluhuSamia na Waziri @MbarawaM , Prof. Lipumba ameuliza swali la msingi sana kuhusu mkataba wa bandari. Kama lengo lilikuwa kuimarisha uendeshaji wa bandari ya Daresalaam, ni nini kilichosababisha kukawa na mkataba baina ya Serikali ya Dubai na Tanzania? 🤔